Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali
Utajisikiaje kama JF itafungwa kwa kuwa kuna watu wanatukana wengine? Au ni halali kutukana upande mmoja tu na kwingine haramu?
 
Kukataa majalala si mwanzo wa kukataa uchafu duniani, ila ili kuondoa uchafu ni lazima kusafisha sehemu ilo chafuka.
Twitter ni kama jalala tu, uchafu ukizidi unasafisha jalala linakua safi kisha unasubiri uchafu mwingine uletwe.

Kuifungia twitter siyo suluhisho, ila suluhisho ni kuyajibu yale yanayotolewa twitter kuwa ni ya kweli au si ya kweli, lakini kuyakimbia ni kuonyesha kuwa unataka ukweli usisemwe.

Kwani kuna ugumu gani wao kuwa na account ya twitter na kujibu hoja zote.
 
Twita ni mwendo wa kujiachia. Paskali buuuuuwana kha hebu punguza mihemko Kule hawafuti ukiandika inaenda kama ilivyo hawachuji kihiiivyo.

Uhuru wa. Vyombo vya Habari ni upi mnaoutakaga ninyi waandishi? Ukweli mchungu Paskali wenye dhamana warekebishe tabia wanakera
Twitter sio mali ya bongo Trump kashindwa itakuwa huku kwa mtogole.

Ukweli utawaweka huru Watanzania. Pascal Mayalla kuya huku ujisomee mwenyewe

Ushauri kama unaumia kwa yanayoandikwa Twitter futa account utakuwa salama kwa moyo
Huku kunakufaa maana siku hizi wanachuja hatari
 
P.
Kuna wakati unashindwa kuwaza sawasawa kama mwanahabari na mwanasheria nguli! Ni Kama Kuna nguvu kutoka mahali Fulani inakusukuma na au imekurushia hoja hii uiongee bila kukupa wewe nafasi ya kuijengea mashiko! Yaani umegeuzwa mpiga filimbi kwa tcra ilihali wao wanashinda huko Twitter kusaka maarifa mapya!

Na kwanini uone kuwa kuufungia Twitter itakuwa suluhu? Hao watumiaji wengine ambao naamini ni wengi wasioichafua serikali yako pendwa umewatafutia jukwaa lingine mbadala?

Hebu fika mahali ujitathimini na uyathamini mapenzi ya wanatwiter na uache kuwa biased kwa haki za wengine!!
Ikikupendeza pambana nao hukohuko hao unayodhani wanaipaka matope serikali yako pendwa!
 
Wakifunga Twita watu wanahamia platform nyingine na wanaendeleza wanachokijua wao. Ni ujinga wa 4G kuamini kufungia platform ndio suluhisho.

Naamini hao TCRA wawatafute wanaotukana na kuwajibishwa na kama wameshindwa hiyo kazi waondoke ofisini wapishe watu wengine wafanye hiyo kazi.
 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali

Na usisahau kuwa unaweza kukuta hao Wanaokutukana na Kukudhihaki ndiyo wakawa Wanakupenda Kiukweli kuliko Wanafiki ambao wanakutetea.
 
Tukianza kufungia vyombo tutaishia na magazeti ya CCM tu. Hata JamiiForums watafunga. Kuweni makini sana msije kitumika vibaya
 
Pascal Mayalla alishaapa kuwa " ameshajikomboa" hivyo hawezi tena kutafuta ajira hapa duniani.

Ana kampuni kubwa na ameajiri vijana wa kutosha!

Hauwezi kuwa ktk Hali moja Wakati wote hata kama wewe ni Tajiri kupindukia , Setti na Rugemalira (pamoja na Utajiri wao) hawaku tarajia Siku moja kwenye Maisha yao kuwa katika Wakati walio nao kwa sasa.

Wapo walio jiapiza kupitisha iliyo kuwa Rasimu mbovu iliyo kosa Maoni ya Wananchi ya Katiba; na sasa hawapo /hawana Mamlaka waliyo kuwa nayo mwanzoni.
 
Back
Top Bottom