Party Caucus ya CCM ni Kuwahujumu Wananchi

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika utaratibu wa kawaida wabunge wa vyama vya siasa wanakuwa na mkutano uitwao Party Caucus. Lengo la mkutano wa aina hii ni kwa ajili ya pengine kupendekeza na kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali kulingana na mahitaji au kujadili namna ya kupitisha sera iliyo katika mchakato. Lakini katika hali isiyo ya Kawaida, Party Caucus ya CCM imekuwa ni kwa ajili ya kupanga mikakati ya kupitisha na kuunga mkono hotuba za bajeti ambazo hazina maslahi kwa wananchi mfano ile ya wizara ya elimu. Tunawaomba ndugu wabunge mnapokuwa bungeni jaribuni kutetea maslahi ya wananchi zaidi kuliko serikali na vyama vyenu. Tafadhali rejeeni majukumu ya Bunge: Kutunga sheria na kuisimamia serikali.
 
CCM imekuwa ni kikundi cha kijangili na wauwaji.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hii tume ndo inaamua tembo wangapi apewe kinono!,watu wangapi wang'olewe kucha na meno bila ganzi..nk hayo ndo majukumu yao

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
huu ni ukweli , haiji kichwani mbunge anachangia utafikiri matatizo ya watanzania na wapiga kura wake hayajui au anatokea kenya.Anajitahidi kutetea na kupotosha ukweli kama mwiguru kwenye bajeti, mwisho analalamika matatizo kwenye jimbo lake .wabunge hasa waccm waelewe watanzania wa sasa si wa zamani ,kiasi kwamba kama kuna ujinga unasemwa wanaelewa.NI WAO WAPIME KAMA WAPO KUWATETEA WATANZANIA WENYE KERO NA SHIDA ZAO.Nakumbuka komba na mbunge mwijage anadiriki kusema," tutakubeba kwa gharama zote";maanake hata kama kuna ujinga yuko tayari kutetea bila kuwajali watanzania.
 
Hakuna chama pendwa kama ccm hapa nchini..vingine ni makundi ya wahalifu, wahuni,wapiga dili na waendesha madanguro mfano lile la bilicanas ambapo ushoga unafanyika
 
mi siwapendi wabunge wenye matatizo ya akili ambao kila siku wao wanawatetea wahalifu mahakamani kama lissu anayemtetea diwani wa chadema aliyefyeka mifugo miguu na mashamba ya mazao, anamtetea lwakatare ambaye ni gaidi wa kulisha watu sumu...ni wa kulaaniwa hasa
 
Hakuna chama pendwa kama ccm hapa nchini..vingine ni makundi ya wahalifu, wahuni,wapiga dili na waendesha madanguro mfano lile la bilicanas ambapo ushoga unafanyika

Ndg yangu maswaswa jaribu kuwa mkweli waa nafsi yako. Naamini hata wewe hupendi hayo unayoyashuhudia kwa wabunge wa CCM.
 
Jamani, mnaivumisha sana ccm, yaani unakurupuka kitandani hata ujatandika shuka, unawaza niseme nini kuhusu ccm au mwigulu ni kapost jf, mbona tunamaswala mengi tu ya kuzingumzia, kila saa ccm imefanya hiv, mara wako mbeya, mara green guard, mara imeanguka, mara wanapita
 
Naona mwaka huu CCM wameleta vipandikizi kibao hapa JF kutetea hoijaza kijinga za kina Mwigulu.
 
Jamani, mnaivumisha sana ccm, yaani unakurupuka kitandani hata ujatandika shuka, unawaza niseme nini kuhusu ccm au mwigulu ni kapost jf, mbona tunamaswala mengi tu ya kuzingumzia, kila saa ccm imefanya hiv, mara wako mbeya, mara green guard, mara imeanguka, mara wanapita
Sio CCM tu hata CDM na CUF,,,,,,,,,,, watu wakiamka tu ni kuzungumzia vyama tu badala ya kujadili mambo ya msingi.
 
Sio CCM tu hata CDM na CUF,,,,,,,,,,, watu wakiamka tu ni kuzungumzia vyama tu badala ya kujadili mambo ya msingi.

Utakemea mapepo bila kumtaja bosi wao shetani!Utazungumzia matatizo ya nchi yetu bila kuitaja Ccm?
 
Back
Top Bottom