Partner wa biashara anahitajika

Zombi Mweusi

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
842
1,743
Habari zenu wakuu, baada ya kuungaunga visenti vyangu kwenye kazi zangu za uwakala na ukodishaji wa mitumbwi(ngalawa au vikwalukwalu) nimepata wazo la kufungua duka la jumla la urembo.

Duka la urembo nalomaanisha hapa ni uuzaji wa visu,tochi,kamba kifupi pamoja na electronics equipment,partner anahitajika awe dar maana mi nipo dodoma awe anajua machimbo yote kariakoo na biashara naipeleka wilaya moja maana huduma hizo hamna.

SIFA ZA PARTNER ANAEHITAJIKA
-partner atatakiwa kutoa ¼ ya mtaji
-awe na leseni hai ya biashara
-kitambulisho cha taifa
-awe na uelewa hata kidogo wa kiingereza
-umri kuanzia miaka 23
-leseni na kitambulisho cha taifa zifanane taarifa

MGAWANYO WA MAPATO
-Faida itagawanywa kutokana na mtaji wako
-baada ya miezi 3 ya uaminifu ukihitaji kurudishiwa mtaji wako utapata
-kama utarudishiwa mtaji wako utakuwa unapewa posho ya asilimia 4 ya kila mzigo unaoagizwa

Akipatikana kijana itakuwa poa zaidi maana mi pia ni kijana chini ya 30
 
Robo ya mtaji mbona ujaitaja sasa
Mkuu kama mtaji utakuwa laki moja robo ni 25 elfu siwezi kuweka mtaji halisi ila kama tushaelewana kila kitu kitakuwa wazi na nipo tayari kusafiri kuja dar kila mtu kukagua taarifa za mwenzake
 
Back
Top Bottom