Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Parachichi

JF-Expert Member
Jul 22, 2008
510
102
RUNCLUB(1).png


Wakuu poleni na shughuli!

Ee bana kuna ndugu yangu ameniahidi kunitoa kwenye umasikini,kaniahidi kunikopesha USD 15,000 ili nifungue biashara ya kuuza vifaa vya majenzi.

Sasa nauliza wakuu kwa kiasi hicho kinatosha kuanzia?au ntakua najitia pressure tuu manake hela ndogo?

Maeneo ninayotarajia ni tegeta,Boko,Bunju.

Naombeni ushauri tafadhali wenye ujuzi na hii kitu manake naamini JF ni zaidi ya mtandao.

NAWASILISHA WAKUU

WADAU WENGINE WANAOHITAJI UFAHAMU WA BIASHARA HII
Habari JF members,

Naomba msaada kwa anayejua jinsi ya kuwa wakala wa uuzaji wa vifaa vya ujenzi na vinginevyo vinavyohusiana na ujenzi. Hapa namaanisha mfano: cement, tanks, mabati, sink, bathtub, .n.k

Mwenye taarifa zinazohusu swala hili naomba mchango wako, kujua vigezo, masharti, n.k.

Asanteni.
Habari wakuu,

Naombeni ushauri kati ya biashara ya vifaa vya ujenzi (hardware), na mradi wa daladala. Katika biashara ya vifaa vya ujenzi naomba kujua changamoto zake na jinsi ya kununua vifaa na faida zake kwa ujumla. Na kwa upande wa mradi wa daladala ambao mimi mwenyewe ndo ntakua kondakta naomba kujua faida na changamoto zake na jinsi ya kuuanzisha huu mradi.

Ahsanteni nawasilisha.
Habari Wapendwa!

Nahitaji kupata ufahamu angalau kidogo kuhusu biashara ya vifaa vya ujenzi ninaweza kuanza na mtaji kiasi gani kwa kuanzia tu yaani kiwango cha mwanzo kabisa.

Niko maeneo ya Nzega Tabora.

USHAURI NA MAONI YA WADAU
USHAURI WA BURE
Mara nyingi mwanzo ni mgumu sana na hukatisha tamaa pia. Na hasa hii mifumo yetu ambayo unatakiwa ulipe mapato kabla ya kuanza biashara. Lakini kwa maoni yangu mimi naona 15,000,000 to 18M ambayo ndio makadirio ya pesa unayotegemea kuwa kama initial capital sio mbaya kwa sababu ukishaanza biashara ndipo utajua wateja wako wanahitaji bidhaa gani kwa wingi kwa hiyo uwingi wa bidhaa katika fani ya ujenzi kama alivyochangia mdau mmoja hapo juu isikutishe.

Pia ukishaanza biashara kuna kitu kinaitwa mali kauli (maana yake kwa kuaminiwa na mtu ambaye wewe hufanya whole buy kwake anaweza kuwa ana kukopesha mzigo kiasi fulani nje ya cash yako) hii husaidia sana watu wanaoanza shughuli kwani ghafla tu tutakuona una duka kuuubwa ajabu kumbe mali zingine ni ada ya uaminifu wako na sio lazima ziwe zako, ingawa faida ni yako na ndio itakayo kutoa mapema kwenye shughuli uliyo buni.

Kaza buti anza shughuli hakuna kisichowezekana chini ya jua, naamini utapiga bao hasa kwa maeneo uliyo yalenga kwa sababu bado ni endelevu ki ujenzi.
MAMBO YA KUZINGATIA KUFUNGUA HARDWARE
Kwa ufahamu na mtazamo wangu Hardware ni moja ya Biashara ambayo haitakiwi kukurupuka na ni moja ya Biashara ambayo haitaki uwe na mtaji mdogo. Sio biashara ya kubahatisha kwa kuweka mtaji mdogo kwa malengo ya kuongeza as time goes on kama zengine.

Ukijaribu kuangalia utakuta kuwa wale ambao walifungua hardware ndogo wengi sana huishia njiani na kushindwa kuendelea huku pesa ikiwa imepotea. Waliofanikiwa katika hardware ni wenye mitaji mikubwa Kila kitu kinakuwepo hapo, kiasi kwamba anaingia hata contracts za vifaa na building Contractors, wateja wao hujirudia dukani kwao wakianza ujenzi wa nyumba zao hadi kumaliza (coz everything is there) na kwa kiasi kikubwa flow ya mzigo kutoka ni kubwa.

Ukitaka Biashara ya Hardware haya ndiyo ya kuzingatia;

1. Hakikisha una mtaji mkubwa walau milioni 30 ndiyo iwe minimum.
2. Hakikisha kuwa hiyo hardware yako ina variety ya vifaa sababu hio ndio huvuta pawe na wateja. Wateja wengi wa hardware anataka kila kitu akikute mahala pamoja hasa vya msingi.
3. Kama uwezo wako ni mdogo usiguse vitu vikubwa kama nondo, mabati, cement, Chokaa n.k sababu vinahitaji mtaji mkubwa na hivo duka lako linaweza kupwaya.
4. Kama unaipenda saana biashara na una mtaji mdogo basi jitahidi u-specify katika vifaa vya umeme na mabomba tu! Ili ionekane bidhaa zako ni hizo huku wewe ukihakikisha kuwa unavyo kila kifaa kinachohusiana na umeme na mabomba (yaani ya maji toka PVCs, taps, Stabilizer rs n.k)


P.S: Zingatia kuwa haya ni mawazo yangu hivo pia naweza kuwa nimekosea Wazoefu katika hii biashara waweza kutudadafulia zaidi. Kila la kheri mkuu
UNDANI WA BIASHARA YA SARUJI (CEMENT)
Biashara ya cement hususan kama utakuwa unauza kwa bei ya rejareja inatoka zaidi ikiwa inauzwa na vifaa vingine vya ujenzi. Hii ni sababu wateja wengi wa ujenzi huka tayari una duka la hardware, hata kama halina vifaa vingi, unaweza kuanza na hata mifuko 100-200.

Ila kwa kiasi hiki kidogo cha cement, hutaweza kununua moja kwa moja kiwandani na kunufaika na bei ya kiwandani ambayo kwa sasa kwa mfano Dangote ni sh 9500/mfuko wa grade 32.5 na 10000/mfuko wa grade 42.5. Kiasi cha chini unachoweza kuagiza kiwandani ni tani 30 (mifuko 600) ambayo ni kati ya sh mil 5.7 - mil 6 kutegemea na grade. Kwa Dangote haultalipia usafiri na utaletewa hadi mlangoni. Kwa baadhi ya makampuni inabidi ujitegemee gharama za usafirishaji kutoka kiwandani hadi kwako.

Kwa mtaji wako wa mil 3, itabidi ununue kwa watu wa kati ambao wananunua kiwandani ambao wao huongeza faida ya kati ya sh 500-1000/mfuko. Kama utanunua zaidi ya mifuko 50, wauzaji wengi watakuuzia kwa bei ya jumla (10,000 au 10,500) kulingana na grade. Cha muhimu ni kuzungumza nao vizuri, maana mwingine anaweza hata kukuuzia chini ya hapo kama utachukua mzigo mkubwa kwa mara moja.

Ikija swala la faida, faida kwa mfuko wa cement ni ndogo sana (sh 500-1000) kulingana na soko na ushindani ni mkubwa. Ukinunua huo mfuko wa sh 10,000, ili kushindana na soko hutaweza kuuza zaidi ya sh 11,000 kutegemeana na eneo ulipo. Kama wauzaji ni wengi zaidi basi tegemea kuuza chini ya hapo. Biashara ya cement ni biashara ambayo inategemea "volume sale" ili uweze kuona faida ndio maana wafanyabiashara wengine wanaoagiza kutoka kiwandani wako tayari hata kupata faida ya sh 300/mfuko ili kuvuta wateja na kuhakikisha mzigo wa mifuko 600 au zaidi unaisha siku moja.

Kwa uzoefu wangu, biashara ya cement inahitaji mtaji mkubwa ili kuona faida nzuri. Fikiria mzigo wa tani 30 ambao ni sh mil 6 utazalisha faida ya laki 3 (sh 500/mfuko), ambayo si ndogo sana kama utaweza kuuza angalau tani 30/wiki lakini kama huo mzigo utakaa zaidi ya wiki 4 dukani (na hii inatokea kwa hali ya soko hivi sasa), utaona ni faida ndogo sana kwa uwekezaji huo. Maana kumbuka hapo kuna gharama za ushushaji wa cement ambayo kawaida ni sh 100/mfuko na kama umemweka mtu akusaidie naye inabidi umlipe. Kwa watu wenye mitaji mikubwa kidogo wanaongeza mzunguko wao cement kwa kuagiza mzigo mkubwa zaidi na kuisambaza kwa wafanyabiashara wadogo kwa faida si zaidi ya sh 500/mfuko. Lengo kuu ni kuhakikisha mzigo haukai dukani na unauzika kwa haraka.

Kwa uzoefu wangu changamoto kubwa kwenye cement ni kwamba wakati mwingine uzalishaji unakuwa si wa kuaminika, na hii ni kwa viwanda vyote (mara chokaa imeisha, makaa yameisha au malori ya kusafirishia hayatoshi n.k). Unaweza ukawa umelipia mzigo, halafu zikapita zaidi ya wiki mbili unazungushwa kupata mzigo. Sasa hii inaumiza especially kwa wenye mitaji midogo, maana hela umeshatoa kwenye mzunguko na wakati mwingine unakuwa umeshamwahidi mteja kwamba cement yake atapata kesho na hela yake ushachukua...

Pia kama unauza aina moja tu ya cement hio pia itakuwa changamoto, maana kuna wateja kwa mfano hawatumii brand yoyote zaidi ya twiga, kwa hio ni muhimu kuwa na angalau aina mbili au zaidi ya brand. Sasa kama mtaji mdogo itakuwa changamoto kuweza kuwa na brand tofauti za cement kwa wakati mmoja.

Changamoto nyingine hivi sasa ni soko. Kwa kweli soko limeshuka sana, lakini nafikiri hio si kwa cement tu, bali hata kwa bidhaa nyingine.

Ushauri wangu kwako:
1. Kama una duka la hardware na unataka kuongeza cement, basi anza na mifuko 100-200. Ingawa faida si kubwa, lakini uwepo wa cement kwenye duka la hardware inasaidia sana vitu vingine kuuzika kwa vile mteja wa cement mara nyingi atataka vitu vingine vya ziada zaidi ya cement.

2. Kama huna duka la hardware na unataka kufanya biashara ya cement peke yake nakushauri uongeze mtaji ili uweze kuagizia kiwandani. Hii itakusaidia kwenye ushindani wa bei ambayo itakuwezesha kuvuta wateja. Kumbuka wenye maduka ya hardware wana bidhaa nyingi ambazo humvuta mteja, lakini kwa upande wako itakubidi bei yako iwe ndo kigezo kikuu cha kumfanya mteja aje kwako kununua cement tu kwako, halafu atoke aende duka jingine kununua mahitaji mengine ya ujenzi badala ya kufanya manunuzi yote kwenye duka moja.

3. Kama ushindani si mkubwa eneo lako, unaweza ukaanza na mifuko 200-300 kwa biashara ya cement pekee, lengo lako la awali likiwa ni kutengeneza soko na kujifunza biashara huku ukikuza mtaji ili kuweza kuagiza kutoka kiwandani.
 
Ukitaka kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kwa ufanisi mtafute mtu ambaye amefanikiwa katika biashara hiyo. Mimi ninaye rafiki yangu ambaye amefanikiwa sana katika biashara hiyo anaweza kukupa basics. Kama uko serious nipigie simu 0755394701 nikuunganishe naye.
CHARLES.
 
Mara nyingi mwanzo ni mgumu sana na hukatisha tamaa pia. Na hasa hii mifumo yetu ambayo unatakiwa ulipe mapato kabla ya kuanza biashara. Lakini kwa maoni yangu mimi naona 15,000,000 to 18M ambayo ndio makadirio ya pesa unayotegemea kuwa kama initial capital sio mbaya kwa sababu ukishaanza biashara ndipo utajua wateja wako wanahitaji bidhaa gani kwa wingi kwa hiyo uwingi wa bidhaa katika fani ya ujenzi kama alivyochangia mdau mmoja hapo juu isikutishe.

Pia ukishaanza biashara kuna kitu kinaitwa mali kauli (maana yake kwa kuaminiwa na mtu ambaye wewe hufanya whole buy kwake anaweza kuwa ana kukopesha mzigo kiasi fulani nje ya cash yako) hii husaidia sana watu wanaoanza shughuli kwani ghafla tu tutakuona una duka kuuubwa ajabu kumbe mali zingine ni ada ya uaminifu wako na sio lazima ziwe zako, ingawa faida ni yako na ndio itakayo kutoa mapema kwenye shughuli uliyo buni.

Kaza buti anza shughuli hakuna kisichowezekana chini ya jua, naamini utapiga bao hasa kwa maeneo uliyo yalenga kwa sababu bado ni endelevu ki ujenzi.
 
We jaribu tu bahati yako, biashara ni risk na ukitaka kufanikiwa lazima ukubali kurisk hiyo pesa kidogo utakayo azimwa anza na bidhaa ndogondogo then uongeze zile kubwa kadri mtaji unavyoongezeka! Nakutakia mwanzo mzuri.
 
Anahitajika mtu ambaye yupo tayari kuingia ubia katika kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kwa Dar es salaam.
 
That is great I am expecting to come to Dar Sept 06 will cantact you
 
Anahitajika mtu ambaye yupo tayari kuingia ubia katika kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kwa Dar es salaam.
Enny. just like the other guys, I'm more than interested. Ukija dar we need to talk seriously. Actually we can form a partnership and have a chain of stores for that. For you information, this is one of the niche areas in growing cities like Dar-es-salaam. Who knows we might even extend to other cities like Arusha, Mwanza etc. So ukija tuongeeni jamani kwa kina kabisa.
 
I am interested pia, nipo kwenye biz hii kwa muda sasa..... pls tuma details
 
Umeshapata Partners watano, mkiwa wengi sana haina tatizo? mie pia najiongeza kwenye List
 
Thank you for the interested parties we organize and find the convenient time and day.

Tunaweza kujipanga na kufuata taratibu zote zaa kisheria katika kuunda hii partnership business in Hardware.

Myself I am proposing Saturday 10th of September 2010.

Thank you,
 
Ni kweli kabisa umoja ni nguvu na hasa tukiwa serious na business na kufuata maadili ya biashara we can move further
 
Jamani nimepata soko la vifaa vya ujenzi huku DRC Lubumbashi naomba wale ambao wapo serious tujipange na nipate contact zenu kwa mawasiliano zaidi.

Asanteni sana
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom