Part (II) Kwanini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania bado maskini licha ya kupokea Misaada na Mikopo ya mamilioni ya Fedha kutoka nchi zilizoendelea?

Naomba kujua zaidi kuhusu hili, naona linafikirisha sana!
Nimefanikiwa kuropoka tu, sijui chochote kuhusu hili. Labda kama utafanikiwa kuwapata wataalamu wa madini, mafuta na gas. Wamo wengi tu humu jukwaaani
 
_______________________
Siku chache zilizopita nilizungumzia chimbuko la misaada na Mikopo na kuona kwamba nchi za Ulaya zilipiga hatua kubwa kupitia misaada hiyo na Mikopo ambayo kwa lengo la awali lilikuwa ni kuzijenga na kiziendeleza nchi hizo baada ya uharibifu mkubwa wa vita ya pili ya Dunia na kutokea kwa mdororo mkubwa wa uchumi katika miaka ya 1930's.

Sehemu hii ya pili ya andiko lenye kichwa kimoja cha Habari inalilenga bara la Afrika kwa muktadha ule ule wa misaada na Mikopo na kutoa sababu kwanini Afrika licha ya misaada ya matrilioni ya Fedha lakini bado inaendelea kuwa maskini.

Baada ya nchi za Ulaya kujiimarisha kiuchumi, miaka ya 1960's, wakaona kwamba ili wajiimarishe zaidi ni Vizuri kuzipiga tafu nchi za Afrika kwa kutoa misaada ya kifedha ili kujenga miundombinu kama barabara, reli pamoja na umeme huku lengo lao la nyuma ya pazia likiwa ni kupata unafuu wa ubebaji wa malighafi kwa msaada wa viwanda vya awali (processing industries) kwaajili ya kuchakata malighafi, kuzipunguza uzito kabla ya kuzipeleka ulaya.

Ni kweli wakaanza kumwaga pesa Afrika, na kujenga miundombinu, mfano kati ya mwaka 1960 na 1977 walifadhili ujenzi wa bwawa la Kariba (Kariba Dam) ambalo lipo mpakani mwa Zambia na Zimbabwe. Nchi nyingi pia zilipata ufadhili (msaada) wa projects za Hydroelectric, hata Tanzania bwawa la Kidatu lilifadhiliwa na baadhi ya mashirika ya Ulaya kama SIDA na NORAD.

Ingawa kulikuwa na agenda ya siri, lakini miradi ilikuwa inakwenda na mpaka leo ipo. Kuna kitu kilikuja kuvuruga.

Mwaka 1973, nchi za uarabuni ziliiwekea Marekani vikwazo vya usafirishaji wa mafuta zikiwemo na nchi nyingine za Ulaya, sababu ikiwa ni Marekani kuisaidia Israeli katika vita Kati ya Israeli na nchi za Uarabuni vita ilojulikana kama 'Yom kippur' au vita vya ramadhan.

Baada ya vikwazo hivyo bei za mafuta zilipanda, uzalishaji ukashuka huku Afrika kukiwa na njaa na baadhi ya bidhaa muhimu kuwa adimu na kukosekana kabisa, sasa ili kupambana na hali hiyo, nchi za Ulaya zikakubaliana kuwa Sasa mikopo kwa nchi za Afrika iwe kwa riba na kwa upande wa misaada itolewe kwa masharti na ilenge vitu vya kutumia tu ama kununua (consumable goods) mfano Chakula au ukipewa pesa ya kupambana na malaria, utatakiwa kununua dawa zao lakini pia uwaruhusu kufanya baadhi ya shughuli zao kwa Uhuru, au kuwapa vitu fulani fulani (hapo Sasa ndio utakutana na masuala ya uwekezaji ambao una faida kubwa zaidi upande wao kuliko sisi/mikataba ya kinyonyaji).

Na nchi za Ulaya zilifanikiwa kuitengenezea Afrika mzigo wa deni kubwa sana. Kwa mujibu wa takwimu ni kwamba mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 1980 deni la nchi za kusini mwa jangwa la Sahara lilikuwa ni Dola za Marekani Tilioni 1. Unajua ukitaka mtu awe mtii sana kwako uwe unamdai deni kubwa sana ambalo hawezi kukulipa, anakuwa tayari na anakubali kila kitu hata ukimwambia mi nataka unipe nyumba ya wanao niweke duka na watoto wako wawe wanalala kwa majirani.

Lakini pia kilichochangia kulikomoa bara la Afrika kwa misaada kandamizi mpaka Afrika tumepoteana ni vita baridi iliyofanya Dunia kugawanyika yaani Ujamaa dhidi ya Ubepari/Socialism vs. Capitalism. Hapa mataifa makubwa yalinoa visu ili mwenye kisu kikali akate keki ya Afrika. Tumefikia mahali ambapo mpaka wanatuchagulia Marais wa Afrika wanaoona wao kwamba wanafaa kutuongoza.

Katika kuhitimisha ni kwamba Misaada na Mikopo ni Kirusi ambacho sisi Waafrika tumeaminishwa kwamba ni dawa ya kuondokana na umaskini, kumbe kinazidi kututafuna pasipo kujijua.

Unapewa mkopo kwa masharti, unapewa msaada kwa masharti, unaambiwa kaboreshe afya, hizo pesa zikanunue microscopes au vifaa tiba (medical equipments) ambazo zinatengenezwa kwao, na deni la hiyo pesa na riba yake iko palepale.

Lakini Pamoja na hayo yote tatizo lipo pia kwa nchi za Afrika, pesa hizo hizo zenye masharti ya mabeberu unakuta zinaangukia kwenye mikono ya kifisadi, mikono ya wenye tamaa na wasiowajali wengine.

NINI KIFANYIKE ILI KUKATA MINYORORO HII ILIYOFUNGWA KWA KUFULI NA FUNGUO ZIKATUPWA BAHARINI?View attachment 1934812
Kuanzia kule juu njaa ndio shida, kila mtu anataka akistaafu asiwe na shida yoyote pamoja na vitukuu vyao maisha yao yote
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom