Parking zaondolewa jijini Arusha kifisadi

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Kabla ya uboreshaji wa barabara za katikati ya jiji la Arusha haujafanyika kulikuwepo maegesho ya kutosha ya magari na barabara zoote zikawa zinapitika bila kuleta bughudha kwa magari au watumiaji wengine wa barabara.

Ukarabati wa barabara ulipofanyika kwa lengo la kuboresha jiji kwa makusudi kabisa Injinia wa mkoa au wa manispaa akafanya madudu kwa kuzibana barabara na kuondoa parking na hivyo kufanya magari kupita kwa shida zaidi katika barabara hizo kuliko mwanzo. Alichokifanya Injinia ni kuwa aliamua kwa makusudi kuweka ka ukuta pembeni ya barabara na kuzuia kabisa uwezekano wa magari kupaki nje ya barabara kama mwanzo. Matokeo yake ni kwamba magari baada ya kukosa sehemu za kupaki( haswa magari ya wenye maduka) kutokana na hizi kuta yakapaki pemebeni mwa barabara mpya pande zote na hivyo kusababisha barabara kuwa nyembamba na kupitika kwa magari kusubiriana. Yaani inakuwa ngumu magari mawili kupishana kama mwanzo. Hali hii iko kwa kiasi kikubwa katika :
Barabara inayotoka St. James kutokezea Annex Hotel, {stendi ya vifodi}
Barabara ya St. Thomas Hospital kutokezea langu kuu la soko kuu Arusha,
Barabara inayoanzia General Pharmacy kutokezea ilipokuwa Image Motors na nyingine nying
i.

Harufu ya ufisadi

Baada ya watu kuhoji utashi na uwezo wa Injinia wa mkoa kiutendaji imebainika kuwa haikuwa bahati mbaya kubana barabara wala kufuta parking bali ni fursa ya kuwatengenea ulaji vigogo fulani ambao wamebuni mradi wa Parking maeneo ya ilipo ofisi ya Christopher Mwakasege na eneo lililokuwa baa maarufu ya Baracudda karibu na Jengo la mkuu wa Mkoa.

Compound zilizoko maeneo hayo mawili inasemekana ndizo zitakazotumika kama parking za kulipia. Sijadodosa bei za kupaki magari humu lakini itakuwa ni tofauti na ile inayochajiwa kwa gari shs 200 kwa saa kwa sisi wenye magari binafsi.
Kwa bahati mbaya parking hizi haziwezi hifadhi hata magari 100 jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa sana kwa wakazi wa Arusha kwani msongamano mjini umeongezeka baada ya barabara za katikati ya mji kuwekwa lami bila kupanuliwa wala kuweka sehemu za parking.

Mi nafikiri kuna wadau wengi walioathirika na jambo hili na kama kweli kama nia ni kusaidia kuboresha mji basi hata suala la kupanua parking badala ya kuziondoa lingepewa kipaumbele.
Injinia kama hajui aangalie barabara ya kutoka Mnara wa azimio hadi metropole ilivyojengwa kwa kuzingatia umuhimu wa wenye maduka kuegesha magari yao bila kubughudhi wanaopita barabarani ikiwa ni pamoja na magari kupishana bila shida.
Injinia au wa manispaa au Mkoa watueleze kwa nini wameondoa parking hadi traffic wanalalama?.
Kuboresha jiji ni kuongeza au kupunguza msongamano wa magari? Iweje yeye afikiri tu kujenga lami bila kuwaza kuwa magari yataegeshwa kivipi na wapi?
Hiyo sehemu ya pembeni aliyoiacha anataka kufanya biashara gani humo au makusudi tu ili watu wakalipe kwenye parking zao ambazo hata hazitoshi
 
Tatizo hapa mkuu MVUMBUZI hatuna mbunge wala madiwani. Hao magodi fadha nao kama ni kukomoana ndio muda wao wa kutumia ombwe hili. Nothing we can do, we just sit and watch. At the same time tunachapa kazi.
 
Last edited by a moderator:
Hii hali tumesubiri mtu wa kuliongelea na mpaka sasa hivi ni kimya ili hali kila kitu kikionekana hakijakaa sawa. watendaji wako wapi wakemee kwani jamani kujengwa lami kumekuwa kama laana kwa wenye magari jijini Arusha. Msongamano katika mitaa ya kati ni mkubwa na huu ni wa kutengeneza kwa maslahi ya watu wachache.
 
Tunateseka saaan hapa arusha kutokana na barabara kujengwa lami na tulifikiri ujenzi huu ungepanua mji . Hili ni kosa la Mainjinia wetu waliosimamia kazi hii ambayo lengo lake ni kujinufaisha
 
hata hivyo watu walikuwa wanapark magari vibaya mjini..... na watu wa parking system walikuwa wananyanyasa sana watu na kufungia matairi vyuma..... bora kuwe na sehem maalum kwa ajili ya kupark magari..... ambao hawana magari mdebwedo tu.
 
Back
Top Bottom