Paradox: Mgomo wa MDs unawadhuru Wangonjwa; Kufutia Usajili MDs kunasaidia wagonjwa!

Kwanza mtoa mada kasema ni tetesi so naomba mwenye habari za kuaminika atumwagie jamvini kama kuna ukweli wowote katika hili.Pili nadhani ni uamuzi mzuri sana na wenye busara ameuchukua huyo Dr (Kama kweli) kuliko kushawishi wenzake wagome halafu mwisho wa siku kila mtu anakufa kivyake kama hali wanayoi-face ma-intern kwa sasa.
 
na wengine wanaenda kazini lakini hawatoi huduma. Wanazunguka corridor hadi muda wa kutoka kazini. Mwingine anasimulia hospitali ya mkoa haina chumba cha upasuaji, kazi yake kuandika rufaa, amekata tamaa ya kazi,

Si waache kabisa wasiende kazini. Sasa unaenda kazini halafu hufanyi kazi maana yake nini si unawatesa raia wasio na hatia. Wapambane na serikali siyo kupambana na raia wasio na hatia.
 
Mimi nadhani viongozi wetu wana ubia na hospital za Private ndio maana hawajali watu watatibiwa wapi, Kwa ni i Aghakan iwe na vifaa vyote na Muhimbli ikose ? Kwa nini huduma za Aghakhan ziwe ghali sana na serikali isiitoze kodi kwa nini ? Mimi naona kuna mshiko kwa viongozi na ndio maana wanapenda kutoboresha huduma za afya hili wakatibiwe nje na humo kuna percentage yao.
W
achovu nachelea kukinzana na hoja yako hapo juu! Kama viongozi hao hao wameweza kupeana mirahaba ya 97% to 3%, sio rahisi waweze kugeuka nakufanya biashara nzuri na ambayo ni very strategicaly na Private entities. wasiwasi wangu ni huu, Kama karne tuliyoko waweza kuulizia bei ya maandazi ulaya ukiwa nyumbani kwako hapo dar, ni kipi kisichowezekana kuhusu kitanda cha kumpuzisha mgonjwa?
 
I respect maamuzi and absolutely was perfect, there were two choices! Kuacha kazi mwenyewe kwa sababu malipo hayatoshi au kufanya kazi kwa terms na malipo yaliyowekwa. Kama umekiuka, lazima sheria ichukue mkondo wake. Tutabembelezana hadi lini sasa.
Unafahamu ratio daktari mmoja hapa Tanzania anapaswa kuhudumia watu wangapi?
 
Hoja kubwa ambayo imekuwa ikitolewa na wale wanaopinga mgomo wa madaktari ni kuwa mgomo una madhara ya moja kwa moja kwa wagonjwa na hasa upatikanaji wa huduma ya afya. Wanaopinga mgomo wa madaktari wanasema "madaktari hawana uzalendo" na wanafanya hivyo kwa kuendekeza "pesa" na siyo "wito wao". Wanatuambia - ndugu zetu hawa - kuwa mgomo wa madaktari una madhara ya moja kwa moja kwa wagonjwa na kuwa "madaktari wanawatoa kafara wagonjwa" kwa kuamua kugoma. Hoja zao tunazielewa hata kama hatuzikubali baadhi yetu sisi.

Hoja yao hiyo ingekuwa na nguvu na kuonesha ukweli kama ndugu zetu hawa hawa wangekuwa wa kwanza kulaani kitendo cha serikali kuanza kuwafutia usajiri madaktari na hata kuwaondoa kazini. Mtu mwenye hekima anajiuliza kuna tofauti gani basi kati ya mgomo wa hiari wa madaktari na amri ya nguvu ya kuwaondoa madaktari kazini? Kuna tofauti gati ya kimatokeo (consequential difference) kati ya daktari kugoma kutokwenda kazini na daktari kufutwa usajili wake na asiende kazini? Mgonjwa anaona tofauti gani?

Utaona hoja inayotolewa ni ya kuwakomoa madaktari. Kwamba "kwa vile serikali ilitaka mrudi kazini katika mazingira yale yale na kwa masharti yale yale nanyi mkakataa basi tunawakomoa ili tuone mtatumia elimu yenu wapi!". Sasa hili ni zuri kwenye kulipiza kisasi lakini kiakili halina mantiki, ni woga, na matumizi ya ubabe wa serikali (the tyranny of the government). Lengo ni kutaka kupigiwa magoti, kubembelezwa na hatimaye kuwafanya madaktari hawa - wengi vijana - wawe katika hali ya kukata tamaa (desperation) ili hatimaye mmoja mmoja waje kuomba msamaha na wakubali kurudishiwa usajili kwa masharti makubwa zaidi! Ni mbinu hii hii kwa wale waliosoma Boarding school wanaikumbuka hutumiwa na shule kuwarudisha wanafunzi walioleta vurugu; pale ambapo shule inawafukuza halafu ili warudi basi wanatakiwa kuweka sahihi makaratasi ya kutojihusisha na vurugu au masharti mengine magumu. Wanafunzi wanaokubali masharti hayo kimsingi wanajifunga utumwa; hawawezi kulalamika - bila kujikuta wanakumbushiwa walichotia saini!

Hivyo basi tunaweza kuona pia tofauti nyingine kubwa; madhara ya kuwafutia madaktari usajili au kuwatimua kazini ni makubwa zaidi kuliko madhara ya mgomo wa madaktari. Nitarudia sentensi hiyo na ninatumaini watu itawafikirisha kidogo: madhara ya kuwafutia madaktari usajili au kuwatimua kazini ni makubwa zaidi kuliko madhara ya mgomo wa madaktari. Madhara haya kwanza ni kwa wagonjwa na pili yanaingiza mchakato mwingine kabisa. Lakini zaidi ni madhara ya hatari kwa sababu kama madaktari wakiwa majasiri na kuamua kujiuzulu na kutojali usajili waliokataliwa na wakaamua bora warudi kulima kuliko kulazimishwa kufanya kazi kwenye mazingira magumu serikali haitokuwa na jinsi isipokuwa kurudi nyuma na kuwa itakuwa imepoteza hazina kubwa na kwa hakika itaingia gharama kubwa zaidi kuwa-replace hawa kuliko kama ingekaa na kukubali madai yao ya msingi!

Hoja ya kwamba madaktari wangeendelea kurudi kazini wakati "serikali inashughulikia matatizo yao" ni hoja yenye kuvutia dhaifu wa fikara. Matatizo ya madaktari siyo sawa na kero za muungano ambazo kwa miaka hamsini zimekuwa zikishughulikiwa kwa uvivu. Matatizo ya madaktari na hasa changamoto ya sekta ya afya ni wazi sana - maslahi, vitendea kasi na mazingira ya kazi. Kimsingi hayo matatu tu yanahitaji sera inayoeleweka na ambayo inazingatia unyeti wa sekta hii. Kufikiria sekta ya afya na fani ya udaktari kama fani nyingine ni kukosa kabisa kuelewa vitu vinavyoitwa "vipaumbele".

Binafsi ninaamini mgogoro mkubwa wa sekta yetu ya afya unasababishwa kwa sababu serikali imeng'ang'ania kujihusisha na utoaji wa huduma ya afya na hasa uajiri wa madaktari. Sielewi kwanini bado serikali inataka kuendessha hospitali nyingi hata za chini. Binafsi naamini mojawapo ya vitu ambavyo serikali ingeweza kuvifanya vizuri ni kuendesha hospitali za rufaa tu na vituo vya afya ya msingi na kuachilia huduma zote za katikati na mahsusi kufanywa na sekta binafsi. Serikali ingeweza kabisa kutengeneza mazingira mazuri kwenye afya ya msingi na mazingira mazuri kabisa kwenye rufaa. Madaktari na taasisi bbinafsi zingeweza kutoa huduma ya afya nyingine - isiyohusisha rufaa (na hata rufaa) lakini ikipunguza mzigo mkubwa wa serikali.

Leo serikali inapata mzigo mkubwa kwa sababu inajaribu kuendesha mambo mengi kutoka serikali kuu; halmashauri, polisi, magereza, maji, elimu, ulinzi, tawala za mikoa vyote vinaendeshwa toka serikali kuu. Matokeo yake serikali kwa kweli haiwezi kuhudumia sekta nyeti kama ya afya kwa uzuri zaidi. Na kuamua kuwafuta usajili madaktari hakusaidii kabisa kuondoa tatizo lilipo bali kunalichochea kwani kunajengwa katika hoja kuwa - madaktari watasalimu amri na kuja kuomba radhi. Sasa kama madaktari hawaombi radhi na baada ya kuona serikali inaamua kuwafutia wenzao usajili wakaamua kujiuzulu ili kulinda haki zao serikali itafanya nini?

Ikumbukwe kuwa punda hubeba mizigo kwa muda mrefu na huweza kwenda umbali mrefu na mizigo mingi tu. Lakini punda naye ambaye husifiwa kuwa ni "mnyama wa kazi" naye huchoka. Na kuna wakati - kwa wale waliowahi kufuga punda wanajua hili - punda hugoma. Haendi kwa fimbo, upinde au ulimbo! Sasa punda akigoma hata umtukane vipi au umshawishi kwa fimbo haendi! na akitaka kukuudhi zaidi - na sijui wanawajuaje - punda hukaa chini kukuonesha tu kuwa haendi unakoktaka aende hadi umpunguzi mizigo.

Madaktari wetu wamekuwa kama punda; wameenda na kwenda na kubebana na kubeba na sasa nina wasiwasi kuwa wanaweza kukaa chini na kusema "screw this!". Na wakifanya hivyo, siyo usajili wala udahili utakaoweza kubadilisha na kimsingi kulazimisha serikali kuanza upya.

Vyovyote vile ilivyo, uamuzi wa kuwafutia madaktari usajili ili kuwalazimisha kurudi kazini ni uamuzi wa kiwoga, wa kibabe na ambao umejaa kushindwa ndani yake. NI uamuzi unaoonesha upeo wa uwezo wa watawala wetu kutatua matatizo yetu. NI uamuzi ambao unahitaji kupingwa na kulaaniwa kwani unakwepesha matatizo. Kwani, hata madaktari wakiamua kurudi na kufanya kazi kwa kuhofia usajili wao kufutwa bado matatizo ya msingi yatakuwepo pale pale na bado yataendelea kuchemka chini kwa chini (simmer).

Na kwa kadiri matatizo bado yanafurukuta basi bado migogoro itatukuta.

Na. MMM
MMM, serikali imejaa vibonde wasio kuwa na akili za kufikiria. Mimi nilipata kuwa hayo mazingira. Wewe fikiria ni wangapi (vijana) wenye moyo na uwezo wa kusoma masomo ya udakitari (Anza na Biology O level, uje PCB A level (Na hapo kuna vitabu vinaitwa mikate, bado kuna boook kubwa BS=Biological science, au jingine understanding biology n.k.; then chuo uanze na cadaver (dead body) na hapo unacheza nazo mwaka mzima na mi chloroform kibao ina kununukia, then uje uanze magonjwa na wagonjwa bila kuasahu biochemistry na physiology). Jamani ni mlolongo mrefu sana. Ndiyo maana vijana wengi kwa sasa hawataki PCB wala PCM, maana ni ujinga mtupu, na ukichaa kusoma hayo masomo halafu unakuja kuishia kukamatwa na kuteswa msitu wa pande, kisa unahitaji mwajili wako akusikilize ili muelewane. Yaani mi Drs nawasikitikia sana maana sisi huku kwenye masomo ya biashara tunahama kila siku, yaani ukiona mwajili anakuzingua unahama, ukipata maslahi makubwa unahama, lakini leo Dr anafutiwa usajili, mtu ambaye alijitoa kwa moyo wake kusomea u Dr, serikali ya kipumbavu sana hii.
 
Dr1,Dr2,Dr3 yaani 3Dr JK huyu anaonyesha jinsi alivyozipata hizo 3Dr anaona amepatia kuongoza nchi,dhaifu+legelege mimi naomba kadi yake ya clinic ya utotoni niangalie maendeleo yake ya ukuaji pengine mwenzetu alikuwa kwenye mstari mwekundu nasio kijivu au kijani tunaweza mlaumu bure.
 
I respect maamuzi and absolutely was perfect, there were two choices! Kuacha kazi mwenyewe kwa sababu malipo hayatoshi au kufanya kazi kwa terms na malipo yaliyowekwa. Kama umekiuka, lazima sheria ichukue mkondo wake. Tutabembelezana hadi lini sasa.

And that is the SOLUTION??? now? this won't come to pass before we see the consequences! imefika mahali sasa basi! washenzi hawa hawawezi kutuambia hawawezi kuboresha huduma za afya kwa watanzania walio wengi ilhali tunaona pesa zikitumika katika mambo mengi yasiyo ya msingi!! au kwa vile wao wanatibiwa India tena kwa kodi zetu wenyewe! wameanzisha wao kuwa LITAKALO KUWA NA LIWE wajiandae vya kutosha na sisi wananchi tutakapoamua kuwa liwalo na liwe,so far WE HAVE NOTHING TO LOSE EXCEPT OUR OWN LIVES WHICH WE SHALL LOSE ANY WAY IF NOT TODAY THROUGH THEIR SECURITY AGENCIES THEN IT WILL BE TOMMOROW THROUGH THE POOR HEALTH SERVICES WE ARE CRYING ABOUT! tuchosheni tu,si mnajiona mko sayari nyingine!?
 
Madaktari hawapiganii vitanda vya kutosha maodini ili wavilalie wao!, hawatafuti dawa za kutosha ili watibiane wao na familia zao!, ni lini mtaacha kuwekeza india na kujenga kwenu? vilivyoko India vilijengwa havijadondoka kutoka juu jengeni kwenu bwana!.

Well said!
 
Hakuna mtu(kiongozi) wa hovyo kama ile handsome boy ya kifipa-mzee wa kulia
 
Si waache kabisa wasiende kazini. Sasa unaenda kazini halafu hufanyi kazi maana yake nini si unawatesa raia wasio na hatia. Wapambane na serikali siyo kupambana na raia wasio na hatia.

wasiwasi wangu siku wagonjwa wenye hasira wakiwatoa meno na kucha!
 
Mwanaharakati wa kweli utamtambua kwa matendo yake. Kuresign kwao kunaonyesha UDHAIFU wao katika kutetea wanyonge. Kama wao ni wanaharakati/watetezi wa wanyonge iweje leo wakaresign na kuwaacha wanyonge wao wakifa au ndo kupoteza mwelekeo? walidhani serikali inaathirika kwa mgomo wao? Hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya mgomo na hilo limewafikisha hapo. Kutumia wagonjwa kama bomu ktekeleza ugaidi si sahihi. Kumbe ule usemi wa the end justifies the means ni sahihi

You sound like a nanny!
 
Mimi siichukii serikali ila nawachukia wanaoiongoza serikali. Yani watz milioni arobaini tunanyanyaswa na kichwa kimoja jk? Kwani hii nchi ya jk, ni Mali yake?
 
Madaktari kwa kweli wana nafasi hii tu kuweza kubadilisha mwelekeo wa sera ya afya nchini. Leo nimeshinda kuzungumza na mmoja wa wahusika wa hili hapo nyumbani na kwa kweli hali katika sekta ya afya ni mbaya sana.
 
Mnyampaa kweli we kilaza wa vilaza yaani hujui mambo yanavyokwenda? Anyway ivi mtu ukiwa kilaza huwa hujijui? Maana unatupa tabu kuangalia utumbo unaoupost.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom