Papua New Guinea Wafungwa wapigwa risasi walipokuwa wakitoroka

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Maafisa wa magereza nchini Papua New Guinea, wamewapiga risasi na kuwauwa wafungwa 17, ambao walivunja gereza na kutoroka siku ya Ijumaa.

Polisi wamewatia mbaroni wafungwa watatu, huku wakiendelea kuwasaka wengine 50 ambao bado hawajulikani waliko tangu kutokea kwa kisa hicho katika gereza la Buimo liliko mji wa Lae.

Polisi wanasema kuwa, wengi wa wafungwa waliotoroka walikuwa wahalifu sugu.

Idara ya usalama nchini humo imewatahadharisha raia kuwa macho na watoe taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wakiwaona wafungwa hao.

Gereza hilo la Buimo, huwa na msongamano mkubwa wa wafungwa na uchafu na mwaka jana wafungwa 12 waliuawa baada ya kujaribu kutoroka.
 
Hivi huwa kuna kuzimu nyingine zaidi ya hii dunia? maisha ya watanzania tu ni kuzimu tosha, sasa inakuwaje wale waliopo ktk magereza ya mateso?
 
Back
Top Bottom