Paper ya form MWEMBETOGWA SEC:Akamatwa akimfanyia paper ya English mdogo wake.

Pawaga

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
1,330
964
Kijana mmoja anayesoma form 6 mbeya(jina la shule halijapatikana) amekamatwa jana akimfanyia mdogo wake mtihani wa form 4 hapa mwembetogwa sec-iringa. Inasemakana alishafanya Geography,kiswahili na mathematics sasa jana alikuwa anamalizia english na ndipo msimamizi alimtilia shaka akamfuata na kumtaka atoe kitambulisho chake,hakuwa nacho na alipobanwa akakiri kuwa yeye si mwanafunz wa hapo ila anafanya kwa niaba ya mdogo wake. Polisi walichukua nafas yao kwa kumpga pingu na kuondoka nae... Hii inakaaje wadau. Source:mimi mwenyewe nimeshuhudia tukio zima
 

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,851
863
Tukaaminije kwamba ni kweli,na sio habari ya kuzusha?
WELL, hapo ni uzembe wa usimamizi,hawakukagua vitambulisho mlangoni wakati wa kuingia kwenye chumba cha mtihani kwa wanafunzi, wangekuwa wanakagua, asingeweza fanya mtihani hata mmoja.uzembe ni wa shule hiyo na usimamizi wote!
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,550
5,688
Kwanza shule inapaswa ifungiwe, wasimamizi wote+viongozi wa shule wafungwe.
 

Moesk

Member
Aug 15, 2011
13
0
da uzembe uliokisiri 4sure jamaa.dogo.na wasimamizi wachukuliwe hatua kwa kwenda kinyume na sheria wasimamizi hawakuwa makini na kazi yao na huyo jamaa baada ya kumfundisha dogo anaona njia ni kumfanyia paper
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,772
6,531
inawezekana dogo hakuwahi kufanya pepa toka shule aianze au hakutoa mlungula kwa awamu ya siku hiyo..
 

papachu

Member
Apr 16, 2011
29
1
yaani kama kunauwezekana na likazibitishwa hili inabidi azabu kali itolewe kwa muhusika na wasimamizi na uongozi wa shule inabidi nao waadibishwe inaonekana ni kamchezo cha shule hilyo,au kama vipi shule ifutiwe usajiri hapo tunaandaa mafisadi wa taifa la kesho
 

tz1

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
2,122
526
Hiyo siyo sec mwembetogwa haileweki.Haina kiwango cha maana.Ilipo anziswa late 80s sisi tulilkuwa wanafunzi wa kwanza The highlands High school.Ambaye mwalimu mkuu wa mwembetogwa alikuwa Mh kibasa.(Mp aliepita ).Alitufundisha somo la biashara Highlands sec na alikuwa mwalimu mzuri sana darasani na michezoni mkoa mzima wa iringa.
Highlands tulikuwa tunashinda mechi zote za mpira wa kikapu nyanda za juu chini ya mwalimu Kibasa.Waulize tosamaganga tulilkuwa tuwapa vikapu vingapi kisha wanarusha mawe na ngumi.
Lakini shule ya mwembetogwa ina ulakini.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
220,033
728,531
Akamatwa akimfanyia mtihani mwenzake
Send to a friend
Friday, 07 October 2011 19:34


Tumaini Msowoya, Iringa
WAKATI mitihani ya kidato cha nne ikiendelea nchini, mwanafunzi wa kidato cha sita Sekondari ya Tosamaganga, wilayani Iringa, amekamatwa akijiandaa kumfanyia mtihani huo mwanafunzi wa Sekondari ya Mwembetongwa, Kata ya Makorongoni, Manispaa ya Iringa.

Mwanafunzi huyo ambaye namba yake ya usajili Tosamaganga ni TSS 191226, aliamua kuingia kwenye chumba cha mtihani wa kidato cha nne, shule ya Mwembetogwa akiwa amevaa sare za shule kama wanafunzi wengine, ili kufanikisha lengo lake kwa kumsaidia mtihani wa kidato cha nne, mwanafunzi mmoja (jina tunalo).

Kwa mujibu wa Ofisa Elimu Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi, tukio hilo lilitokea juzi wakati wanafunzi hao wakijiandaa kufanya mtihani wa somo la Kiingereza.

"Kilichotokea ni kwamba, alijifanya mwanafunzi wa Mwembetogwa, hivyo akaingia kwenye chumba cha mtihani kama kawaida, akiwa amevaa sare kama wenzake. Akakaa kwenye kiti na kupewa karatasi ya kujibia ambayo aliiandika namba ya mtihani ya (mwanafunzi mhusika), aliyetakiwa kufanya mtihani huo, ndipo akakamatwa," alisema Mnyikambi.

Akisimulia tukio hilo, Mnyikakmbi alisema dakika tano kabla ya kuanza kwa mtihani huo, msimamizi mkuu wa mitihani shuleni hapo, alipita kwa watahiniwa kuhakiki namba na picha zao, kupitia fomu maalumu inayoitwa ‘Photo entry Form' kuthibitisha kama wanafunzi waliopo ndiyo wanaostahili kufanya mtihani.

Hata hivyo, alipofika kwenye kiti alichokuwa amekaa mtuhumiwa, alibaini picha iliyopo kwenye fomu yenye namba tofauti na sura ya mtahiniwa na kwamba, baada ya kuchunguza akabaini kuwapo kwa udanganyifu.

Ofisa elimu huyo alisema baada ya kubaini hilo, alipewa taarifa na kwenda shuleni hapo haraka kujua ukweli wa jambo hilo, kumtambua mwanafunzi aliyetaka kumfanyia mwenzake mtihani huo kinyume cha Sheria za Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

"Mara ya kwanza alijifanya anasoma Tukuyu, lakini baada ya kubanwa zaidi ilibidi aseme ukweli kwamba, yeye ni mwanafunzi wa kidato cha sita Tosamaganga, akichukua masomo ya Fizikia, Kemia na Bailojia (PCM) na kwamba, ameamua kumsaidia mwenzake baada ya kuombwa," alisema Mnyikambi.
Hata hivyo, Mnyikambi alisema mwanafunzi halisi aliyepaswa kufanya mtihani huo alikuwapo kwenye mazingira ya shule, aliyekamatwa hakuwa ameanza kujibu maswali, aliruhusiwa kuendelea na mtihani wake wakati suala hilo likishughulikiwa ngazi nyingine.

Alisema katika maelezo yake, mwanafunzi huyo wa Tosamaganga alisema hakupewa kiasi chochote cha fedha kumfanyia mwenzake mitihani, bali ni kutokana na urafiki uliopo baina yao.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa saa kadhaa, kabla ya kuachiwa kwa dhamana."Ni ajabu mwanafunzi wa PCM kumfanyia mwenzie mtihani wa Kiingereza, suala la kuingia kwenye chumba cha mtihani ni kosa. Tayari tumetoa taarifa Baraza la mitihani na masuala mengine ya kisheria yatafuata...kwa sababu tumezuia uhalifu, labda angekuwa amemjibia," alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Sekonsari ya Mwembetogwa, Mbatta alipofuatwa kutolea ufafanuzi jambo hilo, alikataa kuzungumzia akitaka apatiwe barua itakayowatambulisha waandishi wa habari na jambo wanalolitaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangala, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba, taarifa rasmi itatolewa baada uchunguzi kukamilika.

 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
:poa

Kilichonifurahisha ni kusikia tu hilo jina MWEMBETOGWA.....

Linanikumbusha chocho nilizokuwa napita kutokea makanyagio nisije gongana na Mzee Tende and Company on the way back to "Complex"
 

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Ni jambo la kwaida. Kama mzee Mwinyi alishawahi kulambwa vibao hadharani je, litashindikana la kumfanyia mtihani mwanafunzi mwingine? Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo woooote, nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,735
9,119
Duh! Hizi papers zina mambo. Kuna wengine wamepandisha mashetani kwenye chumba cha mtihani.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom