Papaa Msofe naye yamkuta. Afikishwa Mahakamani akituhumiwa na makosa matano likiwemo ya Utakatishaji fedha

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Mfanyabiashara maarufu Marijan Msofe maarufu 'Papaa Msofe' na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo utakatishaji wa fedha wa zaidi ya TSh.Mil 900.

Si mara ya kwanza kwa Papaa Msofe kufikishwa Mahakamani hapo kwani aliwahi kukabiliwa na kesi ya Mauaji mwaka 2012 kisha alifunguliwa kesi ya Kughushi mwaka 2015.

Mbali na Msofe, washitakiwa wengine ni Wakili wa Kujitegemea, Mwesigwa Mhingo,Fadhil Mganga, Wencelaus Mtui na Joseph Haule na miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni Kuratibu Genge la uhalifu,utakatishaji fedha na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi, hivyo haina dhamana ambapo shauri hilo limehairishwa hadi December 16, 2019.

FB_IMG_1575294102451.jpeg


12E5D2BB-D627-45A4-80A1-0E0D33D2EA8F.jpeg

0154C262-884B-4679-86B7-C4AB1B7909A2.jpeg


-----

MFANYABIASHARA Marijan Msofe (53) maarufu kama Papa Msofe, Wakili wa Kujitegemea Mwesigwa Mhingo (36) na wenzao watatu, wamefikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi ikiwamo kuratibu genge la uhalifu na kutakatisha Dola za Marekani 410,000.

Washtakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Maternus Marandu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya na Wakili wa Serikali, Glory Mwenda.

Wakili Komanya akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, aliwataja washtakiwa kuwa ni Papa Msofe, Mhingo, Wenceslaus Mtui (49), Josephine Haule (38) na Fadhili Mganga (61).

Alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Desemba 2018 na Septemba, mwaka huu washtakiwa wote kwa pamoja na wenzao ambao hawajakamatwa walifanya mpango wa kuongoza genge la uhalifu.

Katika shtaka la pili, alidai kati ya Desemba 2018 na Septemba, mwaka huu washtakiwa wote, mahali tofauti walitakatisha Dola za Marekani 300,000 (sawa na Sh milioni 690) kutoka kwa Pascal Jean Camille.

Shtaka la tatu, inadaiwa kuwa siku ya tukio la pili, washtakiwa wakiwa na nia ovu, walijipatia kwa njia ya udanganyifu Dola za Marekani 300,000 kutoka kwa Camille baada ya kumdanganya kuwa wangemuuzia kilo 200 za madini aina ya dhahabu na kuyasafirisha kwenda nchini Ureno huku wakijua si kweli.

Upande wa Jamhuri ulidai katika shtaka la nne, tarehe tofauti Desemba 2018 na Septemba, mwaka huu washtakiwa walitakatisha Dola za Marekani 110,000 (Sawa na Sh milioni 253) kutoka kwa John Mahsson wakati wakijua ni zao la uhalifu.

Wakili Komanya alidai katika shtaka la tano, washtakiwa walijipatia Dola za Marekani 110,000 kutoka kwa Mahsson baada ya kumlaghai kwamba wangemuuzia kilo 20 za madini aina ya dhahabu na kuyasafirisha kwenda Ureno huku wakijua si kweli.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi haujakamilika na waliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo na kupangwa itajwe Desemba 16, na washtakiwa walipelekwa mahabusu.

Chanzo: Mtanzania
 
Mbali na Msofe, washitakiwa wengine ni Wakili wa Kujitegemea, Mwesigwa Mhingo,Fadhil Mganga, Wencelaus Mtui na Joseph Haule na miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni Kuratibu Genge la uhalifu,utakatishaji fedha na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

********************

Unapotaja jina lenye utata kama hilo la Joseph Haule Ni vyema ukaongeza kuwa si Mbunge wa Mikumi.

Ili kuonyesha weledi na ubobezi wako katika uandishi.
 
Back
Top Bottom