Mbonea
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
Tuesday, October 13, 2009
Mmoja wa makardinal wanaoheshimika barani Afrika toka Ghana amesema kwamba hakuna shaka kuwa Papa wa kanisa katoliki atakayefuatia atatoka barani Afrika.
Baada ya kuchaguliwa kwa Barack Obama kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani, kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson toka Ghana ambaye amepewa jukumu la kuongoza vikao vya kanisa katoliki vinavyoendelea mjini Vatican amesema kwamba hakuna sababu yoyote itakayozuia Papa wa kanisa katoliki atakayemfuatia Papa Benedict kutoka barani Afrika.
Akiongea na waandishi wa habari jumatatu, Turkson alisema kwamba wakati umefika wa kuwa na Papa mweusi toka Afrika.
Akitolea mfano wa aliyekuwa katibu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ambaye naye anatoka nchini Ghana, Turkson alisema kwamba Annan alikabiliwa na matatizo mbali mbali lakini alifanikiwa kumaliza muda wake kwa mafanikio.
"Kwa kuwa makanisa ni ya Mungu, kama Mungu atataka tuwe na Papa mweusi, tutamshukuru sana".
Suala la kuwa na Papa kutoka barani Afrika limekuwa likizungumziwa kwa miaka mingi sasa na sababu kubwa ni kwamba Afrika ndiko ambako kanisa katoliki linapoonyesha uhai.
Kati ya mwaka 1978 na mwaka 2007, idadi ya wakatoliki iliongezeka barani Afrika kutoka milioni 55 hadi milioni 146.
Kinyume chake idadi ya waumini wa kanisa katoliki barani ulaya imekuwa ikizidi kupungua siku hadi siku.
Mwaka 1978, Papa John Paul aliyezaliwa nchini Poland, ndiye aliyekuwa papa wa kwanza kutoka nje ya Italia baada ya miaka 455.
Alipofariki, mwaka 2005 makardinal walimchagua Papa Benedict XVI aliyezaliwa nchini Ujerumani kuwa Papa.
Pamoja na Afrika kuwa na waumini wengi wa kanisa katoliki, makardinal wengi wanatoka barani ulaya na haijulikani kama kweli wataweza kufumbua macho yao na kulipa nafasi bara la Afrika.
Hata hivyo Papa Benedict mwenye umri wa miaka 82 anaoneka ni mwenye afya njema hivyo itabidi waafrika wasubirie kidogo kuanzisha mjadala wa ujio wa Papa toka Afrika.
Papa mpya huchaguliwa baada ya Papa aliyepo kufariki dunia.
Source: NIFAHAMISHE.com