Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,811
- 4,533
Baba Mtakatifu Francisco ameridhia ombi la Kung'atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu Telesphor Mkude wa Jimbo Katoliki Morogoro.Awali mwaka 2019 Baba Mtakatifu alimteua Monsinyori Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S kuwa msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo akiwa na majukumu ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu ili kutoa nafasi kwa Mhashamu Askofu Mkude kushughulikia afya yake ambayo ilianza kuteteleka. Askofu Telesphor Mkude alizaliwa tarehe 30 Novemba 1945 huko Pinde wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Julai 16 1972 Askofu Telesphor Mkude alipata daraja Takatifu la Upadre wa Jimbo Katoliki Morogoro huku 18 Januari 1988 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga ambapo 26 April 1988 aliwekwa wakfu na Hayati Kardinali Laurean Rugambwa.
5 Aprili 1993 Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Morogoro ambapo amedumu mpaka 30/12/20 Baba Mtakatifu Francisko aliporidhia ombi lake la kung'atuka madarakani.
#Kanisakatolikitanzania