Papa Francis atoroka Vatican usiku

ngojeni kama haijaja habari kuwa anaendaga club kujirusha basi watoto wa vatican wapo kwenye wakati mgumu kama yale mambo ya seya wa mivalo
 
Huu ni ushenzi na utampatia shida sana siku za karibuni. Huwezi kuwa mkubwa na mdogo kwa pamoja. Hapa kuna jambo limejificha. Beware Francis!
 
Ni nzuri na mbaya at the same time. Anyway, hatujui nadhiri yake alomwekea Mungu wake ni nini.
 
View attachment 124761
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.


Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.

Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.

Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.

“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo Papa aliwahi kwenda naye nje ya mji kwa ajili hiyo, Askofu Krajewski, alisita kujibu swali hilo.

Wakati huohuo, gazeti la Huffington Post limeripoti kuwa walinzi wa Uswisi, wamethibitisha kuwa Papa amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali usiku akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya wachungaji na kuwapa misaada, wanaume na wanawake wenye shida mbalimbali.

Tangu kuteuliwa kwake, papa Francis amevipamba vichwa vya habari duniani baada ya kuonekana akijaribu kuvaa kofia za polisi wa zimamoto, kuwaruhusu vijana wadogo wa kiume kuibusu miguu yake na kuwapigia simu waumini wake na kuzungumza nao.

Hivi karibuni, aliripotiwa katika vyombo vya habari akiwabusu na kuwafariji waumini walemavu katika Kanisa la Mtakatifu Peter, huku taarifa nyingine zikionyesha kuwa ametuma fedha zake binafsi kwa wahamiaji na wanaohangaikia mafao yao.

Alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis alifahamika kwa kutoroka usiku na kuwatafuta watu, kuzungumza nao na wakati mwingine kuwanunulia chakula.

Mapapa wengine waliopita pia wametajwa kutoroka usiku, kwa mfano papa John wa X111 alikuwa na tabia ya kutoroka usiku na kwenda mitaa ya Rome kufurahia uzuri wa jiji hilo, wakati Papa Pius wa X11alivalia kama Mfaransa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kwenda mipakani kuwasaidia Wayahudi wa Kirumi kisha kuwaweka katika sehemu salama.

nina shaka...maana huyu ameanza kwa kutaka kanisa lisi wanyanyapae mashoga...sasa huku kutoroka usiku mmmhhh maswali mengi bila ya majibu
 
Vatican hamna masikini, utajiri umekufuru kwa Raia wake mia tisa tu wasiolipa kodi kila kitu bei nusu ya wanaulaya
 
vatican kuna masikini,ombaomba,duh?

Mkuu kusema ukweli hakuna masikini anayeishi Vatican. Kwa wale waliowahi kufika Vatican, Vatican ni sehemu ndogo sana ndani ya mji wa Roma ambayo imezungushiwa ukuta. Ukitoka nje ya huo ukuta, tayari upo nje ya Vatican na huko kumejaa masikini na omba omba na hasa wale wa kabila la ____(nimeasahau jina) lakini hawa sio waitaliano na hawana makazi maalumu. Kwa hiyo inaposemekana Pope anatoroka kwenda kuwasaidia masikini sio ndani ya Vatican, ni nje ya hapo.

Tiba
 
Back
Top Bottom