Papa Francis atoroka Vatican usiku

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
papa+f.jpg
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.

Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.

Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.

Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.

“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo Papa aliwahi kwenda naye nje ya mji kwa ajili hiyo, Askofu Krajewski, alisita kujibu swali hilo.

Wakati huohuo, gazeti la Huffington Post limeripoti kuwa walinzi wa Uswisi, wamethibitisha kuwa Papa amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali usiku akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya wachungaji na kuwapa misaada, wanaume na wanawake wenye shida mbalimbali.

Tangu kuteuliwa kwake, papa Francis amevipamba vichwa vya habari duniani baada ya kuonekana akijaribu kuvaa kofia za polisi wa zimamoto, kuwaruhusu vijana wadogo wa kiume kuibusu miguu yake na kuwapigia simu waumini wake na kuzungumza nao.

Hivi karibuni, aliripotiwa katika vyombo vya habari akiwabusu na kuwafariji waumini walemavu katika Kanisa la Mtakatifu Peter, huku taarifa nyingine zikionyesha kuwa ametuma fedha zake binafsi kwa wahamiaji na wanaohangaikia mafao yao.

Alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis alifahamika kwa kutoroka usiku na kuwatafuta watu, kuzungumza nao na wakati mwingine kuwanunulia chakula.

Mapapa wengine waliopita pia wametajwa kutoroka usiku, kwa mfano papa John wa X111 alikuwa na tabia ya kutoroka usiku na kwenda mitaa ya Rome kufurahia uzuri wa jiji hilo, wakati Papa Pius wa X11alivalia kama Mfaransa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kwenda mipakani kuwasaidia Wayahudi wa Kirumi kisha kuwaweka katika sehemu salama.
 
Very dangerous. Anaweza kutekwa au kukumbwa na kashfa. Pili mimi sio muumini sana wa kutoa misaada kwa maskini. Tushughulikie matatizo yanayosababisha watu kuwa maskini hasa umaskini wa kulazimishwa. Sina uhakika kama Vatican kuna vijiji. Ni nchi ya wakazi kama 1000 fu
 
Pengine kuwa too simple nako ni tatizo, kwa kawaida wakubwa hulindwa na wanatakiwa kuwa watii kwa taratibu na sheria na pale inapotokea kufanya kinyume cha taratibu za kiusalama anatakiwa kushikishwa adabu vinginevyo italeta madhara makubwa siku za mbele. Asiendelee kufanya kama alivyozoea huko Agentina, sasa yuko Vatican na wadhifa mkubwa kuliko anavyochukulia binafsi.
 
View attachment 124761

Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.

Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.

"Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda kufanya kazi hiyo," alisema Padri Krajewski.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo Papa aliwahi kwenda naye nje ya mji kwa ajili hiyo, Askofu Krajewski, alisita kujibu swali hilo.

Wakati huohuo, gazeti la Huffington Post limeripoti kuwa walinzi wa Uswisi, wamethibitisha kuwa Papa amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali usiku akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya wachungaji na kuwapa misaada, wanaume na wanawake wenye shida mbalimbali.

kumbe anamsindikiza kutoroka kumetoka wapi tena!
 
SAfari za wakubwa hupangwa, na pale anapochomoka bila utaratibu wa safari ya kupangwa ni kutoroka
 
Hapati usingizi akifikiria maskini mitaani wanavyotaabika kwa kiu, njaa, anaamua kuacha usingizi kwenda kuwasaidia maskini, maana mchana yuko busy na ratiba za kiofisi.
Pamoja na kashfa zisizo na ushahidi hata Lowassa amekuwa na dhamira hiyo.
 
Huyu Pope anatesa kweli walinzi.Anataka kuwa mtu wa kawaida huku akishika nafasi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom