Pope Francis abusu miguu ya viongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir na Riek Machar, akiomba wasitishe vita

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,639
33,414
Pope Francis has kissed the feet of South Sudan's previously warring leaders during a two-day spiritual retreat at the Vatican.
"I am asking you as a brother to stay in peace. I am asking you with my heart, let us go forward," the 82-year-old pontiff said after he performed the rare gesture.
President Salva Kiir and his rival, the former rebel leader Riek Machar, clashed in 2013 leading to a civil war that left 400,000 people dead.
But they signed a peace agreement last year that brought the war to an end.

My take:

Hao viongozi wakitoka hapo na kuendeleza vita badala ya amani watakuwa na mwisho mbaya sana.

Usiombe mtumishi wa Mungu kushuka kwako kwa kiwango hicho ili ubadilike!

jamesmartinsj-1555011964775.jpeg

Pope_Francis_South_Sudan_2019_04_12_01_21_38.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app


======

Papa Francis abusu miguu ya Salva Kiir na Machar kuwasii waache vita
"Nipo chini ya miguu yako" Unaweza kutafsiri hivyo baada ya Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis kufanya kitendo cha unyenyekevu na kisicho tarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, kuwahamasisha kuuendeleza mchakato wa amani.

PAPA FRANCIS AKIINAMA KUBUSU MIGUU VIONGOZI HAO.



Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Mwishoni mwa ziara ya kiroho ya siku mbili ya viongozi hao wa Afrika mjini Vatican, Papa Francis alimuomba rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na hasimu wake Rieck Machar kuendeleza mazungumzo ya amani, licha ya kuongezeka kwa ugumu, na kisha alipiga magoti na kubusu miguu yao, pamoja na ya makamu wa rais Rebecca Nyendeng Garang.

Papa Fransic hufanya tendo la kitamaduni la kiimani la kuwaosha miguu wafungwa siku ya Alhamisi kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kama hili kwa viongozi wa kisiasa.

Alisema mwishoni mwa ziara hiyo kwamba anataraji kusitishwa kwa uadui, mapigano, mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.
 
Aisee, mbona hatari sana, bado wakitoka hapo wakarumbane kwa issue binafsi, sijui nini kitatokea zaidi
 
This is too much, mimi sio wa dini ya ndugu zangu ila hawa wa Sudan kusini viongozi wao Mungu atawalaani sio kwa tukio hili tu maana ni kama mzazi akupigie magoti lakini nchi yao watu wamepigana miaka mingi wapate uhuru mwisho wa siku mnauwa watu wenu kwa ajili ya power? wale watu walipoteza maisha yao kupigana ndio hichi walichopigania. hapana this is too much na hawa wakiendelea kuuwa watu wao ni nchi za EA kuingia na kuwatoa wote hawa na family zao lakini na mashaka na hili sababu sisi wenyewe EA sio wasafi japo ninependa kuona Tanzania na Kenya kuact kama Germany na France huko EU kusimamia mambo ya msingi ila sijui kama itatokea. Naomba nchi irudi katika amani hakuna zaidi.
 
Inaelekea hujaelewa maudhui ya habari. Jinsi ulivyoelewa ni kwamba Wasudan (blacks) wamemlazimisha Pope Francis (white) kubusu miguu yao, ndio maana unasema 'umewakubali'. Hali halisi si hivyo, soma uelewe
Acha kunilisha maneno..
nimeelewa habari kuliko unavyofikiri.

Ni kwamba papa aliwasihi Amani na mapigano vikome na pande mbili kinzani siafikiane,na akaenda mbali zaidi akasujudu na kuwabusu miguu.
(Hi ni ishara ya unyenyekevu na kusihi)

swala ambalo nimelikubali Ni kuona unafiki wa Vatican unadhihirika wazi pasipo ramuli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kunilisha maneno..
nimeelewa habari kuliko unavyofikiri.

Ni kwamba papa aliwasihi Amani na mapigano vikome na pande mbili kinzani siafikiane,na akaenda mbali zaidi akasujudu na kuwabusu miguu.
(Hi ni ishara ya unyenyekevu na kusihi)

swala ambalo nimelikubali Ni kuona unafiki wa Vatican unadhihirika wazi pasipo ramuli

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni Msabato sitii neno ila
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom