Papa ateua maaskofu wasaidizi wawili Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Papa ateua maaskofu wasaidizi wawili Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SubiriJibu, Jan 29, 2010.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Hata miezi miwili haijapita tangu kuhamishwa kwa askofu Methodius Kilaini kwenda kuwa askofu msaidizi wa Bukoba, Papa Benedict XVI amewateua mapadri wawili kuwa maaskofu wasaidizi wa jimbo kuu la D’Salaam. Wawili hao ni Padri Salutaris Libena na Padri Eusebius Nzigilwa.

  Wakati askofu Kilaini alikuwa na Phd. Sasa jimbo limempata professa kwani mmoja wa hao watakaokuwa maaskofu wasaidizi ni Professa (Padri) Salutaris Libena ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa na ni mhadhiri kwenye seminari kuu ya Kipalapala iliyoko nje ya mji wa Tabora. Vilevile alikuwa mkurugenzi wa kiroho au spiritual director wa seminari hiyo. Yeye (Libena) alikuwa ni padri wa jimbo la Mahenge kule kwa askofu Ndorobho nadhani na nimzaliwa wa Itete.

  Mwenzake Padri Eusebius Nzigilwa ni padri wa jimbo la D’Salaam na ni mzaliwa wa Mwanza na amewahi kuwa rector wa seminary ndogo ya Visiga iliyoko mkoa wa Pwani karibu na Kongowe.

  Hivyo jimbo kuu la D’Salaam sasa linakuwa na maaskofu watatu yaani Kadinali Polycarp Pengo na hawa wasaidizi wake wawili. Aliondoka mmoja yaani Kilaini sasa wameletwa wawili kwa mpigo.

  Chanzo: RADIO TUMAINI
   
 2. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba ufafanuzi hapo....
   
 3. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hongera Fr. Libena.
   
 4. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Labda utoe ufafanuzi wa ufafanuzi unaoutaka...
   
 5. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Fr. Nzigilwa pia alikuwa ni paroko msaidizi Makongo majuu hadi anateuliwa na ni mwanafunzi wa masters degree(Education) pale mlimani!
   
 6. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nakumbuka wakati tunajadili suala la Askofu Kilaini kwenda Bk hapa JF, wengi walihoji iweje apelekwe Bukoba amako si hata jimbo kuu kwa qualification na experience aliyonayo? Tukapata majibu kwamba kanisa katoliki aliendeshwi kisiasa/kidunia zaidi. Wana taratibu zao na kanuni zao kwamba kondoo wa bwana wanaweza kuchungwa popote pale, na mchungaji hachagui wapi yalipo malisho!

  Hili limejithibitisha kwa kummteua Fr. Nzigilwa ambaye ndio kwanza anaitafuta Masters degree! Wangapi wenye elimu zaidi ya hiyo wameachwa?
   
 7. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani qualification za mapadre tofauti sana na serikalini,acheni kuanza kulinganisha usomi wa mapadre eti ndiyo wanastahili kuwa kwenye jimbo kuu.
   
 8. Akami

  Akami Member

  #8
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuna wakaribisha sana hao maaskofu wapya,tuwaombee Amani,afya njema,na maadili mema waweze kuifanya vema kazi ya Bwana.

  Tutakukumbuka sana Askofu Kiliani,ulifanya mambo mengi mazuri,Mungu Akubariki
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  All in all naomba nipongeze sana kanisa Katoliki kwa kuwaweka viongozi wa kiroho wasomi kwa kweli wanaongoza na nadhani wanasimamia sana suala la elimu ya juu ambayo ni zaidi pia ya theolojia; hii inawapa ufahamu zaidi na upeo mkubwa zaidi katika kuwachunga Kondoo wa bwana!

  Jina la Bwana libarikiwe!
   
 10. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Interesting. Yaani askofu bado yuko shule. Sasa atafanya uaskofu au itabidi aahirishe hiyo masters degree. Mapadre hawaeleweki, msishangae akaamriwa na mkuu wake kuwa aache shule, maana nasikia huko kwa wakatoliki ukishakuwa padre unasarenda akili na utashi wako wote kwa mkuu wako!
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Nonsensical!
   
 12. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli kaka. Kama una jamaa yako unamfahamu ni padre, mwulize. Ndivyo wanavyoapa.
   
 13. nyaunyau

  nyaunyau Senior Member

  #13
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  uongozi wa kanisa katoliki wanawaencourage watumishi waende shule,Askofu huyo ataendelea na masters na kazi ya utumishi kama kawaida.
   
 14. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45

  MTU B

  hapo umekosea sio kweli kabisa, ni kwamba wana miongozo yao ukiona padre anasoma akaacha ujue labda kazidiwa na shughuli za kikazi, ninao marafiki wengi mapadre wako free tena saana tu,
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Jan 29, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hongera sana kwa mapadre hao, na Mungu awaongoze vema katika kazi yao ya kuchunga kondoo!
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Nawapongeza wachungaji wapya na kuwatakia kila la kheri....naamini papa kuna move anayoikusudia maana kama kawaida, Vatican haina papara kwenye mambo yake.Pengine safu ya uongozi wa kanisa la Tanzania inaapangiliwa upya, taratibu taratibu. Who knows!
  Ila yote ni heri tu!
   
 17. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  `Utopian` ideas!!!!!!! usipende kusikia na kukonkludi wangapi wako kazini na wanasoma?:rolleyes::rolleyes::rolleyes:
   
 18. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45

  nakubaliana na wewe kwani hawa wajamaa wanavyofanya kazi hawaendi papara hata kidogo,,,,nakumbuka hata Kilaini kwenda Bukoba kuna kitu kwani hicho kituo chake cha kazi nasikia mambo hayaendi kabisa, kuna kanisa limeanzwa kujengwa tangu kipindi kile alipokufa kadinali Rugambwa mpaka leo halija kamilika kapelekwa kwa maksudi kabisa huko
   
 19. p

  paulk JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache. Ingefaa kila jimbo liwe na askofu msaidizi
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wow hongera Padre Libena...you deserve it....MUNGU ambariki sana na ampe mafanikio mema katika kazi zake mpya.
   
Loading...