Papa ataka madini yanufaishe wananchi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,849
Posted Date::12/30/2007
Papa ataka madini yanufaishe wananchi
*Ni katika salamu zake za mwaka mpya
* Kilaini naye ashauri vijana kuingia katika siasa

Na Kizitto Noya
Mwananchi

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict wa XV1 ametaka rasilimali za dunia hasa madini na nishati, zitumike kwa faida ya watu wote badala ya kunufaisha kikundi cha watu wachache.

Papa Benedict amesema hayo katika salamu zake za mwaka mpya wa 2008 alizotoa kwa waraka maalum aliousaini mwenyewe, kuitakia dunia amani na upendo. Alisema kama vile Mungu alivyoumba dunia na kuwapa watu haki sawa katika kuitawala, kila mtu ana haki sawa kunufaika na rasilimali zilizoko duniani.

Kitendo cha nchi tajiri kutumia uwezo wake wa kiteknolojia kuchukua nishati iliyoko katika nchi maskini ni udhalilishaji kwa nchi hizo na ni hatari kwa uchumi, alisema Papa Benedict XV1.

Alisema kuna haja ya kufanya mazungumzo ya kina kuhusu matumizi ya rasilimali za dunia kati ya nchi tajiri na zile maskini ili kuweka uwiano sawa wa faida ya rasilimali zilizoko duniani na kuondoa unyonyaji.

Kwa mujibu wa Papa Benedict XV1 kitendo cha nchi tajiri kutumia fursa ya umaskini wa nchi zinazoendelea kuwekeza katika nchi hizo na kujilimbikizia mali kinapaswa kujadiliwa upya ili kutoa fursa sawa katika mgawanyo wa rasilimali hizo.

Alisema nchi maskini zinakubali kutoa rasimali hizo kwa nchi tajiri kutokana na kukosa uwezo wa kuziendeleza jambo ambalo nchi tajiri inatakiwa kuliangalia na kuziwezesha nchi maskini ili ziweze kunufaika na rasilimali zake.

Kadiri muda unavyosonga nchi tajiri zina njaa ya kujiongezea utajiri na njaa hiyo ni hatari kwa nchi maskini ambazo zinalazimika kuuza rasilimali zake kwa kushindwa kuziendeleza na hatimaye kuuza uhuru wao kisiasa� alisema.

Katika hatua nyingine Papa Benedict wa XV1 amezitaka nchi tajiri kupunguza masharti ya misaada yake inayotoa kwa nchi maskini ili kuzisaidia kuondokana na umaskini na kujenga umoja na amani duniani.

Alisema watu wenye madaraka katika jamii pia wanatakiwa kudumisha amani kwa kutumia vizuri madaraka yao na kuweka mazingira sawa ya upatikanaji wa haki mbele ya sheria.

Papa aliyataja mambo mengine yanayohatarisha amani duniani kuwa ni mashindano ya nchi zinazoendelea katika utengenezaji wa vifaa vya kivita hususan mabomu ya atomiki na nyuklia. Alizitaka nchi hizo kuacha kufanya mashindano hayo ili kuiondolea dunia hofu inayotishia amani na kuongeza machafuko katika dunia ambayo Mungu aliiumba iwe na amani.

Alisema mataifa yanapaswa kutambua kuwa amani ni kitu muhimu katika maendeleo yake na watu wake hivyo kuwa na msimamo wa pamoja kuitafuta kwa jitihada zote ili kuifanya jamii iishi kwa amani na iweze kuwa huru kutafuta maendeleo. Aliwataka wanandoa kufanya kazi kwa bidii na kuishi kwa upendo ili kuwa mfano kwa jamii katika kuenzi na kudumisha amani.

Ujumbe huo wa baba mtakatifu umekuja wakati kukiwa na mjadala mkali nchini juu ya manufaa inayopata Tanzania kutokana na rasilimali zake, huku walio wengi wakidhani kuwa yananufaisha wageni na Watanzania wachache badala ya wananchi wote.

Wakati huo huo, Boniface Meena anaripoti kuwa; Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amewataka vijana kuingia katika siasa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani dunia ya sasa inahitaji viongozi vijana wenye moyo, nguvu na uwezo.

Askofu Kilaini aliyasema hayo jana katika misa ya vijana iliyofanyika ufukweni, eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, ambapo aliwahimiza vijana kutokujali miaka waliyonayo.

"Hata kama una miaka 25 na unao uwezo na unajiamini gombea kwani nyie ndiyo taifa la kesho na siyo la keshokutwa," alisema Kilaini. Aliongeza kuwa, "Siasa, uchumi na uongozi ndio dira yenu baada ya masomo na siyo kusubiri kubebwa, huu ndiyo wakati wenu hivyo msingoje kupewa."

Alisema kuwa vijana wanatakiwa watafute kwani hivi sasa hakuna anayetoa, hivyo kujituma ndiyo njia pekee ya kujikwamua kimaisha hivyo wale wanaojiweza kimaisha wasibweteke kwani safari bado ni ndefu.

Kilaini alisema kuwa hayo yote yatawezekana kama nidhamu ipo, kwani bila kuwa na nidhamu ni vigumu kufikia malengo kijana au mtu yeyote aliyejipangia.

"Ushirikiano ni muhimu kwani dunia hii ya utandawazi bila kufanya hivyo vijana wengi watakuwa wakiishia vijiweni kitu ambacho hatutaki kuona," alisema Askofu Kilaini.

Kuhusu suala la ukimwi Kilaini amewataka vijana kutokufanya ngono kabisa kwani kondomu ni ulevi na zinaongeza ufuska unaoendelea kuteketeza vijana kila leo.

"Kondomu ni kama kilevi, ni za kuongeza ufuska, ni upuuzi zile ni kifo hivyo hazifai kutumiwa," alisisitiza Kilaini.
 
Huyu Papa mnafiki .Nataka kwanza arudishe ile zawadi ya gold aliyopewa an JK siku zile yenye zaidi ya kilo 20 ndipo tuanze kuongea lakini kwamba kachukua leo anaanza story hapana .
 
Unafiki wake uko wapi?
Umesema kapewa zawadi1 sasa asichukue?
angekataa ingekuwa shida, kachukua amekuwa mnafiki.
Nampongeza kwa kutamka hayo!
 
In the typical modern papacy tradition of John Paul II pope Benedict uses his insurmountable clout to address isues.Nilifurahi sana alivyoongea kupinga current trend ya capitalism kutotoa permanent employment instead kupendelea short term consultancy,with highlights on the effect of this trend on the family.I am not much of a religious person but if this is the role of the clergy and papacy then thats a good thing.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom