Robot la Matope
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 6,990
- 13,603
Papa Francis amemvua madaraka
Kardinali wa zamani, ikiwa ni tukio la kwanza kwa Kanisa Katoliki kuchukua hatua baada ya Mmarekani huyo, Theodore McCarrick kutuhumiwa kumbaka mtoto miaka 50 iliyopita, taarifa ya Vatican imesema jana.
McCarrick, 88, ambaye alijitoa kutoka Taasisi ya Makardinali ya Vatican mwezi Julai, ni Kardinali wa kwanza duniani kutengwa kutokana na tuhuma za ngono.
Mahakama ya Vatican ilimkuta na hatia ya
kosa la kumbaka mtoto mwenye umri chini
ya miaka 20, uamuzi uliothibitishwa na Papa mwezi huu, na hivyo hauwezi kupingwa zaidi, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Ilisema McCarrick alipatikana na hatia ya
“kuzini kinyume na amri ya sita kwa kufanya uzinzi na mtoto pamoja na watu wazima, na tatizo kubwa zaidi ni kutumia vibaya madaraka”.
Taarifa hiyo inahitimisha kuanguka kwa aina yake kwa kardinali huyo aliyekuwa na
ushawishi mkubwa na kumekuja kabla ya
mkutano wa Vatican utakaofanyika Februari 21-24, ukihusisha maaskofu kutoka kila kona ya dunia kujadili namna ya kulinda watoto ndani ya kanisa.
Kashfa za ngono duniani, na hasa hivi
karibuni katika nchi za Marekani na Chile
zimeyumbisha Kanisa Katoliki na kumfanya Papa Francis kuahidi kuwa na sera isiyovumilia makosa hayo, hata kwa viongozi wa juu wa kanisa.
McCarrick, askofu mkuu wa zamani wa
Washington, alizuiwa kufanya shughuli za
kipadri Julai mwaka jana, baada ya kujivua
ukardinali wake wa heshima. Kwa sasa
anaishi Kansas.
McCarrick anajulikana kwa kufanya ngono na waseminari ambao ni watu wazima kabla ya kukumbwa na kashfa hiyo ya kumbaka mtoto mdogo.
Mwaka jana, waendesha mashtaka wa jimbo la Pennsylvania, Marekani walibaini kuwa viongozi wapatao 300 wa dini walihusika katika kashfa za kubaka watoto kuanzia miaka ya arobaini, lakini kashfa hizo zilifunikwa na maaskofu kadhaa.
Waendesha mashtaka katika majimbo
mengine wameahidi kufanya uchunguzi kama huo.
Mwaka jana, Papa alikubali kujiuzulu kwa
maaskofu kadhaa wa Chile baada ya
uchunguzi kubainisha vitendo kadhaa vya
uzinzi vilivyofanywa na viongozi hao wa dini.
Machi mwaka 2015, Papa alimruhusu Keith O’Brien kuendelea na ukardinali baada ya askofu huyo wa zamani wa Edinburgh na kiongozi wa zamani wa Kanisa Katoliki nchini Scotland kujiuzulu kwa tuhuma za uzinzi.
Chanzo: Mwananchi