Papa amvua Kardinali Theodore McCarrick madaraka kwa kubaka mtoto miaka 50 iliyopita

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
5,025
2,000
Papa Francis amemvua madaraka
Kardinali wa zamani, ikiwa ni tukio la kwanza kwa Kanisa Katoliki kuchukua hatua baada ya Mmarekani huyo, Theodore McCarrick kutuhumiwa kumbaka mtoto miaka 50 iliyopita, taarifa ya Vatican imesema jana.

McCarrick, 88, ambaye alijitoa kutoka Taasisi ya Makardinali ya Vatican mwezi Julai, ni Kardinali wa kwanza duniani kutengwa kutokana na tuhuma za ngono.

Mahakama ya Vatican ilimkuta na hatia ya
kosa la kumbaka mtoto mwenye umri chini
ya miaka 20, uamuzi uliothibitishwa na Papa mwezi huu, na hivyo hauwezi kupingwa zaidi, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Ilisema McCarrick alipatikana na hatia ya
“kuzini kinyume na amri ya sita kwa kufanya uzinzi na mtoto pamoja na watu wazima, na tatizo kubwa zaidi ni kutumia vibaya madaraka”.

Taarifa hiyo inahitimisha kuanguka kwa aina yake kwa kardinali huyo aliyekuwa na
ushawishi mkubwa na kumekuja kabla ya
mkutano wa Vatican utakaofanyika Februari 21-24, ukihusisha maaskofu kutoka kila kona ya dunia kujadili namna ya kulinda watoto ndani ya kanisa.

Kashfa za ngono duniani, na hasa hivi
karibuni katika nchi za Marekani na Chile
zimeyumbisha Kanisa Katoliki na kumfanya Papa Francis kuahidi kuwa na sera isiyovumilia makosa hayo, hata kwa viongozi wa juu wa kanisa.

McCarrick, askofu mkuu wa zamani wa
Washington, alizuiwa kufanya shughuli za
kipadri Julai mwaka jana, baada ya kujivua
ukardinali wake wa heshima. Kwa sasa
anaishi Kansas.

McCarrick anajulikana kwa kufanya ngono na waseminari ambao ni watu wazima kabla ya kukumbwa na kashfa hiyo ya kumbaka mtoto mdogo.

Mwaka jana, waendesha mashtaka wa jimbo la Pennsylvania, Marekani walibaini kuwa viongozi wapatao 300 wa dini walihusika katika kashfa za kubaka watoto kuanzia miaka ya arobaini, lakini kashfa hizo zilifunikwa na maaskofu kadhaa.

Waendesha mashtaka katika majimbo
mengine wameahidi kufanya uchunguzi kama huo.

Mwaka jana, Papa alikubali kujiuzulu kwa
maaskofu kadhaa wa Chile baada ya
uchunguzi kubainisha vitendo kadhaa vya
uzinzi vilivyofanywa na viongozi hao wa dini.

Machi mwaka 2015, Papa alimruhusu Keith O’Brien kuendelea na ukardinali baada ya askofu huyo wa zamani wa Edinburgh na kiongozi wa zamani wa Kanisa Katoliki nchini Scotland kujiuzulu kwa tuhuma za uzinzi.

Chanzo: Mwananchi
 

Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,466
2,000
Kila binadamu ana mapungufu yake. Kuwa Kasisi haimaanishi wanakuwa wakamilifu. Watu wangapi wanaingia kwenye ndoa, tena wengine zile za wake wengi, lakini bado wanakuwa na michepuko, nyumba ndogo, walawiti, n.k?

Tunapongeza Kanisa Katoliki kuwachukulia hatua za wazi wale wote wanaokiuka viapo vyao, amri na sheria za Kanisa. Hata hivyo, lengo la adhabu hizi ni kuwarekebisha ili watambue makosa yao na wamrudie Mungu, sio kuwakomesha na kuwadhalilisha kama wengi mnavyodhani.

Tunawaombea Makasisi wote ili waishi viapo vyao na wamtumikie Mwenyezi Mungu kwa moyo mmoja na kwa Uaminifu. Mwenyezi Mungu bariki Kanisa Katoliki, Mwenyezi Mungu mbariki Baba Mtakatifu Francis.

Amina.
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
2,639
2,000
"kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Ilisema McCarrick alipatikana na hatia ya
“kuzini kinyume na amri ya sita kwa kufanya
uzinzi na mtoto pamoja na watu wazima"

Biblia gani hiyo inayosema amri ya sita ni USIZINI au mwandishi kapotoka?
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,295
2,000
Hili kanisa ni uozo, mwingine huyu hapa rafiki ya Papa Francis kafanya kweli Australia. Huyu ni namba tatu kutoka papa na papa yupo kimya! Wanangoja ipite miaka 50?

World
Australian court convicts once-powerful Vatican official on sex-abuse-related charges
Cardinal George Pell walks to a car in Melbourne on Monday. (William West/AFP/Getty Images)
By Chico Harlan
December 12, 2018
VERONA, Italy — Cardinal George Pell has been found guilty in Australia of charges related to sexual abuse, according to two people familiar with the case and other media reports, becoming the highest-ranking Vatican official to face such a conviction.
The conviction provides one of the clearest examples of how the sexual abuse scandal has eroded the church’s credibility while ensnaring figures in the upper echelons of power. Pell, who has categorically

Soma zaidi: https://www.washingtonpost.com/worl...ory.html?noredirect=on&utm_term=.b699500bf2ef
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,295
2,000
Kila binadamu ana mapungufu yake. Kuwa Kasisi haimaanishi wanakuwa wakamilifu. Watu wangapi wanaingia kwenye ndoa, tena wengine zile za wake wengi, lakini bado wanakuwa na michepuko, nyumba ndogo, walawiti, n.k?

Tunapongeza Kanisa Katoliki kuwachukulia hatua za wazi wale wote wanaokiuka viapo vyao, amri na sheria za Kanisa. Hata hivyo, lengo la adhabu hizi ni kuwarekebisha ili watambue makosa yao na wamrudie Mungu, sio kuwakomesha na kuwadhalilisha kama wengi mnavyodhani.

Tunawaombea Makasisi wote ili waishi viapo vyao na wamtumikie Mwenyezi Mungu kwa moyo mmoja na kwa Uaminifu. Mwenyezi Mungu bariki Kanisa Katoliki, Mwenyezi Mungu mbariki Baba Mtakatifu Francis.Amina.
Hivi unalitetea kanisa katoliki, unatetea Makasisi, unatetea nafsi yako?

Unafahamu maana ya 85% ndani ya makao makuu ya ukatoliki kuwa mashoga? Na hauoni tatizo lolote hapo?

Unafahamu maana ya mpaka Rais wa nchi (Duterte wa Ufilipino) kulalamika kuwa alishafanyiwa mambo ya kishoga na mapadri wa kanisa katoliki? Na huoni tatizo lolote hapo?

Unafahamu maana ya Umoja wa Mataifa kulilalamikia kanisa katoliki kuwa linaharibu maelfu ya watoto duniani kwa liwati?

Dah! Kama yote hayo unafahamu na hauoni tatizo lolote nikuweke kundi lipi?
 

TOEDSLOTH

JF-Expert Member
Nov 3, 2018
793
1,000
Hivi unalitetea kanisa katoliki, unatetea Makasisi, unatetea nafsi yako?

Unafahamu maana ya 85% ndani ya makao makuu ya ukatoliki kuwa mashoga? Na hauoni tatizo lolote hapo?

Unafahamu maana ya mpaka Rais wa nchi (Duterte wa Ufilipino) kulalamika kuwa alishafanyiwa mambo ya kishoga na mapadri wa kanisa katoliki? Na huoni tatizo lolote hapo?

Unafahamu maana ya Umoja wa Mataifa kulilalamikia kanisa katoliki kuwa linaharibu maelfu ya watoto duniani kwa liwati?

Dah! Kama yote hayo unafahamu na hauoni tatizo lolote nikuweke kundi lipi?
Makombo ya waarabu katika ubora wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,295
2,000
UBAKAJI NA USHOGA NI TUHUMA ZA KWELI NDANI YA KANISA. HII DINI ACHA TU,BORA UWE KIPOFU WA MACHO KULIKO KUWA KIPOFU WA MOYO.
Qur'an 2:
Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. 10

11. Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. 11

12. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui. 12

3. Na wanapo ambiwa: Aminini kama walivyo amini watu. Husema: Tuamini kama walivyo amini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu. 13

14. Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao na mashet'ani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi tunawadhihaki tu. 14

15. Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo. 15

16. Hao ndio walio nunua upotofu kwa uwongofu; lakini biashara yao haikupata tija, wala hawakuwa wenye kuongoka. 16

17. Mfano wao ni kama mfano wa aliye koka moto, na ulipo tanda mwangaza wake kote kote Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawawacha katika giza, hawaoni. 17

18. Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. 18
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,608
2,000
Mapadri na maaskofu wa kikatoliki sehem kubwa wamekua ndio chanzo cha ushoga, wamekua wakilawiti wale vijana wahudumu wa madhabahuni na kubaka watoto wadogo.

Kama kijana wako anafanya kazi chini ya padri kua makini, inawezekana ameanza kutafunwa. Hakikisha mwanao wa kiume hakaribiani kabisa na padri.

Watoto wa kike wadogo wasimsogelee kabisa padri au askofu.

Padri mmoja mseng.e wa nyakato mwanza alikua anamtongoza demu wangu, nikakusanya ujumbe wake wote baadae nikaamua kumsamehe. Alivyo taahira alikua akichati na mimi huku akujua anachati na manzi wangu. Namuomba hadi video za uchi ananitumia. Sema hizo mambo bado ninazo ingawa huyo binti tulishaachana. Siku nikiamua nazipublish online.qumamae.
 

mwasengo

Senior Member
Nov 27, 2017
189
500
Naona great thinkers hapa wapo kimya, ndio kwanza 18 saivi. Ila ingekuwa inasema shekh fulani amelawiti, hakika page ingeshafika 200 hapa na kashfa za kutosha,.

Ule uzi wa unguja jamaa kushtakiwa kwa kutaka kumuingilia mkewe kinyume cha maumbile, watu walidhihaki sana, wakahusisha hadi Qur ani, kuwa eti ni sunna. Lakini hapa toka nianze kusoma sijaona sehemu biblia inahusishwa, hii ni kwa sababu upande ambao unahusika kukosoa unaheshim sana vitabu vya Mungu, tukumbuke, kitendo kikifanywa na mtu, awe wa dini fulani, shekh, mchungaji, ustadh, padri. Naomba isihusishwe dini yake, hakuna dini hata moja inayoruhusu zinaa au kuingiliana kinyume na maumbile.
Kwa sababu tendo hilo limefanywa na mtu na sio dini.
Mfano kwa hili, padri katenda uovu na sio kanisa katoliki, wala sio ukristo.

Tuache kukashfiana humu, itakuwa haina umuhimu jamii Forum kuwa ni sehemu ya jamii kukerana, kudharauliana, kutiana hasira na kukebehi upande mmoja utadhani hatuishi pamoja huku mitaani, utadhani hatufanyi kazi pamoja, utadhani hatushirikiani kwa lolote lile. Tuna nn hii jamii.

Nahakika, hii forum ina watu wasomi na wastaarabu, hebu msifikie kuharibu usomi na utu wenu kwa kukashfiana humu. Tunataraji busara na elimu zenu zitusaidie, mtuelimishe na kutukosoa kwa busara, na si kuendeleza comment zinazozidi kutengeneza chuki kwenye jamii.

Nawatakia siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom