Papa aingia Twitter rasmi

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,691
10,116
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa 16, kwa mara ya kwanza ametuma ujumbe usiotarajiwa katika akaunti yake ya mtandano wa kijamii wa Twitter.
Papa alionekana akibonyeza vitufe vya ipad yake na kuandika ujumbe unaosema: “Marafiki wapendwa, nimefurahi kuwa karibu nanyi katika Twitter. Asanteni kwa ushirikiano wenu. Nawabariki wote kutoka moyoni mwangu.”
Msemaji wake alisema kuwa mwanzoni Papa alimfikia kila mtu kwa kutumia akaumti zake za lugha ya Kiingereza.
Akaunti za Papa za Kiingereza zina zaidi ya wafuasi 660,000. Hata hivyo akaunti za Papa @pontifex zinazomaanisha ‘Papa’ au ‘Mjenzi wa daraja’ zinafuatana kila moja.
Mwaka jana, Papa alituma ujumbe wake wa kwanza Twitter kutoka katika akaunti ya Vatican na kufungua utukufu wa kuona taarifa mpya kutoka tovuti nyingi.
Kiongozi huyo wa dunia wa watu bilioni 1.2 na zaidi walio waumini wa madhehebu ya Romani Katoliki, anatarajia kujitoa kuliko kuandika ujumbe wa Twitter kwa kila mmoja.
 
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa 16, kwa mara ya kwanza ametuma ujumbe usiotarajiwa katika akaunti yake ya mtandano wa kijamii wa Twitter.
Papa alionekana akibonyeza vitufe vya ipad yake na kuandika ujumbe unaosema: "Marafiki wapendwa, nimefurahi kuwa karibu nanyi katika Twitter. Asanteni kwa ushirikiano wenu. Nawabariki wote kutoka moyoni mwangu."
Msemaji wake alisema kuwa mwanzoni Papa alimfikia kila mtu kwa kutumia akaumti zake za lugha ya Kiingereza.
Akaunti za Papa za Kiingereza zina zaidi ya wafuasi 660,000. Hata hivyo akaunti za Papa @pontifex zinazomaanisha ‘Papa' au ‘Mjenzi wa daraja' zinafuatana kila moja.
Mwaka jana, Papa alituma ujumbe wake wa kwanza Twitter kutoka katika akaunti ya Vatican na kufungua utukufu wa kuona taarifa mpya kutoka tovuti nyingi.
Kiongozi huyo wa dunia wa watu bilioni 1.2 na zaidi walio waumini wa madhehebu ya Romani Katoliki, anatarajia kujitoa kuliko kuandika ujumbe wa Twitter kwa kila mmoja.

Kama mkatoliki sikubaliani na kauli yake hiyo hapo nilipobold,labda kama kuna makosa ya kiuandishi,lakini pia kuna makosa madogomadogo mengi tu katika ukatoliki ambayo kwa akaunti yake hii ya Twitter tutaweza kumfikia moja kwa moja.Mwenye uwezo wa kubariki ni Mungu peke yake,yeye kama mwanadamu aliyepewa daraja hilo takatifu alitakiwa kutuombea baraka ya mungu mwenyezi na si yeye mwenyewe kutubariki..
 
dah...kichwa cha habari kilinifanya nishangae kwa kudhani ni PAPA samaki...
 
Kama mkatoliki sikubaliani na kauli yake hiyo hapo nilipobold,labda kama kuna makosa ya kiuandishi,lakini pia kuna makosa madogomadogo mengi tu katika ukatoliki ambayo kwa akaunti yake hii ya Twitter tutaweza kumfikia moja kwa moja.Mwenye uwezo wa kubariki ni Mungu peke yake,yeye kama mwanadamu aliyepewa daraja hilo takatifu alitakiwa kutuombea baraka ya mungu mwenyezi na si yeye mwenyewe kutubariki..

Mbona wazazi huwa wanabariki watoto wao..nadhani inawezekana na akiamua kulaani pia anaweza.. kila mtu anaweza kubariki
 
Mtoaji wa baraka ni mwneyezi mungu peke yake,mzazi anaweza akakupa baraka zote lakini kama si mapenzi ya Mungu basi ni kazi bure..Na palepale mzazi anaweza akalaani ila kama si mapenzi ya Mungu vilevile laana hiyo itakuwa ni ubatili tu...
 
Kumbe jibu unalo sasa . . . ni imani yako tu kupokea na kuamini.
Labda kama unazungumzia aina nyingine za baraka i.e zisizo mapenzi ya Mungu (na nguvu za giza ndo zinazokuwa rejected)
 
Mtoaji wa baraka ni mwneyezi mungu peke yake,mzazi anaweza akakupa baraka zote lakini kama si mapenzi ya Mungu basi ni kazi bure..Na palepale mzazi anaweza akalaani ila kama si mapenzi ya Mungu vilevile laana hiyo itakuwa ni ubatili tu...
Papa kama kiongozi wa kanisa, na kwa mafundisho ya kanisa katoliki ambayo yanaeleza kuwa yeye ni Halifa wa Petro ambaye alikabidhiwa funguo za kubariki na kulaani, basi Papa anao uwezo wa kuwabariki waumini wa kanisa lake.

Kama wewe ni Mkatoliki, aidha umesahau mafundisho, au umeasi, au huamini mafundisho, au la huwa ni mgumu kuelewa, na nakushauri ukafanye malipizi kama utakavyoelekezwa na paroko wako.

Naamini kuna watakaokubaliana nami kuwa baadhi ya makanisa , hasa haya ya Kilokole huwa wanasali wakisema "Tunakubariki Mungu"!...nadhani hapo bwana St. Paka Mweusi ndipo utachanganyikiwa kabisa!!
Usiwaangushe mapaka wenzio bana, eg. Paka mweupe na PakaJimmy, my good broda!
 
Last edited by a moderator:

Hapo tutaendeleza mjadala,sina biblia yangu hapa karibu lakini kilichosemwa ni chochote utakachokifungua duniani kimefunguliwa mbinguni na chochote utakachokifunga na mbinguni kimefungwa,na sikuona kama alipewa mamlaka ya kubariki...
Nitakapokuwa na bibilia yangu nitakutafutia huo mstari ambao nina uhakika unaujua ..
 
Mkuu St. Paka Mweusi,
Naamini kuna mtu mwenye uelewa wa chini amekuibia password yako na anaitumia kwa siri kubwa.

Kama msitari unasema nimekupa mamlaka, chochote utakachofinga duniani na mbinguni kimefungwa, unadhani maana yake nini? Si uwezo wa kulaani na kubariki? Au mwenzetu unaelewaje?
Naomba unambie uko Parokia gani ili tuwasiliane na Paroko akutafutie Katekista aanze upya mafundisho ya katekisimu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom