Panga laja vyama vya siasa - tendwa atishia kuvifuta vyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Panga laja vyama vya siasa - tendwa atishia kuvifuta vyama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 28, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  • TENDWA ATISHIA KUVIFUTA VYAMA

  Na Ratifa Baranyikwa

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MSAJILI wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa, amesema wanatarajia kuanza mchakato wa kuhakiki uhai wa vyama vya siasa ili kubaini kama viko hai na vile visivyokidhi malengo kufutiwa usajili.  Tendwa alitoa kauli hiyo ofisini kwake jana, wakati wa hafla ya kukabidhi cheti cha usajili wa kudumu kwa Chama cha Kijamii (CCK), hatua inayofanya idadi ya vyama vya siasa nchini kufikia 19.  Kwa mujibu wa Tendwa, kuna vyama ambavyo uhai wake ni wa mashaka na hivyo kushindwa kutimiza malengo yake na matwaka ya kisheria.


  “Sasa kwa kutotimiza kwao matakwa ya kisheria maana yake wanatuomba kimya kimya tuwafute na tutawafuta maana vipo vyama ambavyo havipo pande zote za muungano, kwa maana ya kuwa na wanachama bara bila Zanzibar.  “Nawaambia mapema kabisa, tunakuja na tutakagua bara na Zanzibar…kadiri chama kilivyosema kina wanachama sehemu fulani huko huko tutakwenda na kamwe hawatatudanganya,tutawapa taarifa,” alisema Tendwa.  Kwa mujibu wa Tendwa vyama vya siasa vilivyopewa usajili wa kudumu hadi sasa ni 19 huku kile cha Movement for Democracy and Economic Change kikiwa kwenye taratibu za kuhakikiwa.  Kuhusu CCK, Tendwa alisema kuwa hatua ya kukipa usajili wa kudumu inatokana na kutimiza masharti ya kisheria ambayo ni pamoja na kuwa na wanchama 200 pande zote za muungano.  Alikiasa chama hicho kigeni katika medani za siasa nchini kuwa na wajibu wa kupanda mbegu ya amani kwa maendeleo ya ustawi wa jamii.  “Kuna majimbo yako wazi kama Arumeru Mashariki...kuna wabunge wako nje ya vyama vyao na kesi ziko mahakamani, sitaki kuzungumza ila ikitokea majimbo hayo yanakuwa wazi, CCK wanayo nafasi ya kusimamisha wagombea wao,” alisema Tendwa.  Naye, Mwenyekiti wa CCK, Costantine Akitanda, alisema wameamua kuanzisha chama hicho kwa sababu wapo Watanzania wengi ambao hawaridhishwi na sera ya vyama vilivyopo.  Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Renatus Muhabi, alisema kuwa watafanya kazi mithili ya wabunge ikiwa ni pamoja na kumuona Rais Jakaya Kikwete kumueleza tatizo la umeme na masuala mengine

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeye aliteuliwa na Rais wa Nchi; alisajili vyama Vingi ili tu CCM kiwe na Nguvu zaidi ya hivyo vyama Uchochoro na kuvushinda kifedha, kwa idadi ya wanachama , kwa mali na mwamko hivyo wananchi wote wataona jibu ni kuchagua CCM

  Sasa, Wananchi WanaVyama Vingine Pamoja na CCM, Wamechoka na CCM Wanaangalia kipi ni kibovu lakini zaidi ya CCM na wanajiunga, sasa Msajili anatishia kuwa sasa ninataka kuvunja vyama kapata wapi hiyo amri sio toka chama tawala?

  Hivi huyu babu hatakiwi kuwa Huru? Kenya wana Vyama vingi zaidi ya Bongo vinakufa na kuzaliwa kila siku sijasikia Msajili wao Akirukia rukia hivyo vyama kwa kuvivunja

  Naona Tuende UN kumuondoa huyu Babu, ni Mzee hawezi hata kuongea Maneno matatu bila kupumua pumzi nzito... LOL
   
 3. P

  Ptz JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Aanze kukifuta ccm, maana kimewafanya Watanzania wawe fukara wa kutupwa kutokana na tabia yake ya kuwakumbatia mafisadi wanaoendelea kuinyonya nchi hadi basi huku mwenyekiti wake akichukua rasilimali chache zilizobaki kuvaa viatu vya Matonya kutembea nje ya nchi huku akiwa na msafara mkubwa kuomba omba.Hembu kama Tendwa anamaanisha akifute ccm nitamuona muungwana.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hizo zote ni njama za ccm kujipanga kwaajili ya 2015 ila wafanye walifanyalo kwa sasa maji yamezidi unga badala ya ugali sasa ni uji yafaa wakubaliane na hali halisi na kujipanga upya
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  chama kinachotakiwa kufutwa haraka ni kile kinacholea mafisadi na kile kinahotoa ahadi nyingi za uwongo ili kupata kura na kile kinachotumia serikali yake kukusanya kodi za wananchi halafu hakitoi huduma inayolingana na kodi wanayokusanya hicho kifutwe haraka sana!!!
   
 6. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Aanze na CCM kwa mauwaji waliyoyafanya hoko Igunga...
   
 7. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  chonde chonde usifikirie kukifuta DP cha Mtikila utaiona dunia chungu maisha yako yote ....
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yes this is Tanzania and Tanzanians like it
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Tendwa anafanya kazi alotumiwa na bosi wake Jk so muacheni 2 koz hajui kusoma majira na nyakati.
   
 10. cooper

  cooper JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 394
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ngoja tuone kitakachoanza kufutwa.
   
 11. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  DP mziki wake ni mnene; kesi mwanzo mwisho. Hapo hawezi jaribu
   
 12. nkawa

  nkawa Senior Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aangalie anapogusa asije akaTendwa yeye....
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Naona anajipa kazi sababu Tume Huru inajengwa isiyona uhusiano na chama cha Mapinduzi kwahiyo anaogopa kazi yeye basi na mapengo
   
 14. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sote tunajua kuwa tume ye2 si tume huru hivo hawezi futa vyama bila kupewa maelezo ya waliomchagua
   
 15. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mkuu, anamjuwa huyo mchungaji hawezi kumgusa. pia kuna siku nilimsikia kwenye redio akisema ile kesi yake ya mgombea binafsi bado anakomaa nayo, kwenye mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu.
   
Loading...