Panda miti ya mbao na nguzo unufaike baadaye

AGRIWORTH TZ

Member
Sep 20, 2020
40
72
PANDA MITI YA MBAO NA NGUZO UNUFAIKE BAADAE

Kilimo cha miti kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na Katika Tanzania mikoa ya Njombe ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa kuzalisha mbao, nguzo za umeme, nguzo za simu za majumbani na nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa vitu vya thamani .

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii ya upandaji miti.

Hii ina maana inapofikisha umri wa kuanzia miaka saba huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita 500,Kwa shamba la miti ya mbao na kwa upande wa miti ya nguzo hupandwa miti 600 kwa ekari moja, Wastani wa chini wa mti mmoja wanguzo ukikomaa in sh.50,000/= na bei ya mwisho kwa mti wanguzo kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu sabini (Tsh 70,000 /=) inategemea na ukubwa wa mti).Hii ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni 42,000,000/=

Nakwa upande wa miti ya mbao unaweza kuuza msitu wako ukisha komaa kwa watu wa naojihusisha na biashara za mbao wakavuna wao pia unaweza kupasulisha mbao na ukaziuza mbao zako kwa bei ya jumla.Ukiuza msitu wa mbao kwa ekari moja haipungui sh.milioni kuminanane (Tsh.18,000,000/=)

Na ukipasulisha mbao nakuziuza utapata kiasi kisicho pungua Tsh.32 milioni.

Uponunua mashamba , kinacho fuataa ni upandaji Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua mikubwa kuanzia umri wa miaka 4 (prooning).

Hata hivyo wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila siku.

HUDUMA ZETU Agriworth Tanzania NI KAMA IFUTAVYO

Tunatoa huduma ya upatikanaji wa mashamba ya kupanda miti ya mbao na Miti ya Nguzo kwa bei ya Tsh.150,000/=Tu kwa ekari moja mkoani Njombe.

Tunatoa huduma ya kuzalisha ya miche ya miti ya mbao na kupanda mashambani bei ya mche ni sh 500 aina ya Mikaratus na Pine

Pia tuna toa huduma ya kusimamia shamba kwa mteja aliye mbali na shamba lake.
Website: AGRIWORTH TANZANIA COMPANY ~ MESSAGE FROM THE GENERAL MANAGER
Email; agriworthtz@agriworthtanzania.com
Agriworth Tanzania"Helping people help others"

FB_IMG_1602302460385.jpg
FB_IMG_1602302443229.jpg
FB_IMG_1602302448296.jpg
FB_IMG_1602302475609.jpg
FB_IMG_1602302486111.jpg
 
Huo upatikanaji wa shamba kwa 150,000 ni malipo ya kukodisha, kununua au?
Hapo unanunua shamba mkuu but kwa hiyo pesa inategemeana na

1. Eneo ambapo shamba linapatikana
2. Aina ya mtu na uhitaji wake wa fedha. Hapa kuna wengine wanauza kwasababu ya shida hvo utanunua kwa bei ndogo
 
Mnayo mashamba darasa yenu tuje tujifunze kwanza kwa nyie wataalamu?
 
Hizo bei za ekari moja za mbao ungefafanua ni softwood, 18m kwa hardwood kwa eka moja ni ndogo sana.
 
Mnayo mashamba darasa yenu tuje tujifunze kwanza kwa nyie wataalamu?
Hapa ndipo wengi wanapokwama
Nadhani uelewa ni wa muhimu kabla hatujapeleka vihela vyako vya ngama
Baadae mnakuja humu mnaanzisha vi-thread vyenu 'tuliowahi kulima mashamba ya miti tukafikia pua tukutane hapa'

Jaman uwekezaji wa kwanza ni wa maarifa, ufahamu, weredi na mbinu za kufanya hiyo biashara kabla hata hujaanza kuwekeza. Kuwekeza ni hatua za mwisho kabisa
Mtakuja kutuletea shida baadae kwa kufuata hawa 'motivation speakers' bure
 
Hao jamaa wao wanataka kudalalia mashamba (ardhi), na pia kufanya biashara ya kukuuzia miche ya mimea mbalimbali wanayootesha kwenye vitalu vyao, bila kusahau na kula pesa ya trainings mbali mbali
 
Huyu mtu ameukimbia uzi wake au ni masuala ya COVID19? Maswali hajibu kabisa.
 
Hapa ndipo wengi wanapokwama
Nadhani uelewa ni wa muhimu kabla hatujapeleka vihela vyako vya ngama
Baadae mnakuja humu mnaanzisha vi-thread vyenu 'tuliowahi kulima mashamba ya miti tukafikia pua tukutane hapa'

Jaman uwekezaji wa kwanza ni wa maarifa, ufahamu, weredi na mbinu za kufanya hiyo biashara kabla hata hujaanza kuwekeza. Kuwekeza ni hatua za mwisho kabisa
Mtakuja kutuletea shida baadae kwa kufuata hawa 'motivation speakers' bure
Ni hakika.

Watu wawe waangalifu huu uzi upo kibiashara zaidi yeye mwenyewe mleta uzi roho inamdunda hiki alichoandika.

Subirini wazoefu wa hiki kilimo waje wawape ukweli halisi. Sio rahisi vile alivyoandika japo biashara ya kilimo cha miti ina faida.

Tuwekeze kwenye utafiti
 
Karibu Nehemia One Pvt Co Ltd. Kampuni yenye wataalamu wenye uzoefu wa masoko na uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Kampuni inapenda kukukaribisha kwenye fursa ya uzalishaji wa MDALASINI tunazalisha miche ya mdalasini na kuhamasisha watu kupanda zao hili kwasababu tunafahamu soko lake jinsi lilivo kubwa na linazidi kukua Kwa kasi. Ni zao lenye matumizi mengi hasa kama kiungo kwenye Aina mbalimbali za vyakula. Jambo jema ni kuwa soko lake ni kubwa mnoo katika nchi zote duniani lakini uzalishaji wake ni mdogo mno!

MASOKO NA UHITAJI

Kwa mujibu wa taaasisi ya utafiti ya persistance market research, thamani ya soko la MDALASINI duniani itafikia Dola za kimarekani bilioni 1.15 mwaka 2030. Matumizi kwenye viwanda vya dawa na vipodozi, viwanda vya chakula ndio ambayo yanafanya uhitaji wake kua mkubwa. Yako makampuni mengi kama Csi na mengine mengi ambayo yanahitaji mdalasini kutoka Tanzania Kwa bei kubwa kwenda nchi za falme za kiarabu, ulaya, na America lakini upatikanaji wake ni wa chini.

Uhitaji kwenye soko la kimataifa unaongezeka Kwa kasi kwasababu ya matumizi yake kama kiungo cha chakula, dawa chenye antioxidants, ant inflammatory properties, also helping in heart and stroke, blood sugar, diabetes etc.

Kampuni yetu yenye muunganiko na makampuni zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani huwa inapokea oda nyingi za magome ya mdalasini zaidi ya tani 20 Hadi 500 mara Kwa mara lakini tunakosa mdalasini wa kutosha kutimiza oda hizo.

SOKO LAKE KWA TANZANIA

Mdalasini unaozalishwa Tanzania haukidhi kabisa mahitaji ambapo ni kiasi cha asilimia 20 Hadi 28 ya uhitaji hivyo kufanya asilimia kubwa ya mdalasini kuagizwa kutoka nchi za bara la Asia kama India, Vietnam, Malaysia na China.
Baadhi ya wawekezaji kwenye viwanda vya chakula wameonesha nia ya kujenga viwanda Vya kuchakata zao hili lakini ukosefu wa MDALASINI wa kutosha imekua kikwazo.

Licha ya viwanda. Kuna makampuni zaidi ya 100 ambayo yanahitaji zao hili ili kusafirisha kwenda nchi za ulaya, America lakini wanakosa kwasababu ya uzalishaji ni mdogo mnoo!.

Aina ya miche ya mdalasini inayooteshwa na kampuni ni (Cinnamomum verum) picha ziko mwishoni baada ya maelezo.

UZALISHAJI NA MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO HIKI

✓Mdalasini ni jamii ya mti ambao hukua Kwa urefu wa kuanzia Mita 8 Hadi 15 kutegemeana na eneo mmea ulipooteshwa.
✓Hupendelea eneo la wazi kwenye kiasi cha wastani cha jua.
✓huoteshwa kwenye udongo wenye rutuba ya asili na maji ya wastani. Eneo lenye maji mengi au lenye asili ya kutuamisha maji halifai Kwa uzalishaji wa MDALASINI.
✓zao hili halihitaji mbolea wala dawa katika ukanda wa kitropiki kama Tanzania
✓udongo wa tifutifu, kichanga -tifutifu wenye wastani wa unyevu nyevu unafaa saana,
Na maeneo yenye wastani wa mvua wa mm 2000 mpaka mm 2600 Kwa mwaka. Hustawi kwenye mwinuko kuanzia Mita 10 Hadi 1500 kutoka usawa wa bahari na joto kiasi cha wastani wa digrii 27 za sentigredi
✓mmea hustawi au unaweza kustawi kwenye mikoa ya Morogoro, tanga, pwani, mtwara, Lindi, rukwa, tabora, rukwa, tabora, Kagera, mara, (maeneo yanayo zunguka ziwa Viktoria) mbeya, katavi, kigoma na Zanzibar.
✓ ekari moja hupandwa miche 380 mpaka 400

MAVUNO

1. Mdalasini huanza kuvunwa kuanzia umri wa miaka miwili. Jambo zuri ni kuwa, baada ya kuvuna, mmea unachipua tena na huvunwa Kwa mwendelezo Kwa kila baada ya miaka miwili Hadi mitatu mpaka baada ya miaka 30 Hadi 45
2. Majani, na mbegu hutumika kuzalisha mafuta ambayo Yana thamani kubwa. Magome hutumika kutengeneza viungo vya chakula, dawa na hata vipodozi.
3.jinsi mmea unavo kaa shambani miaka mingi ndivo ambavyo thamani yake inapanda kutokana na uwingi wa magome yatakayo patikana, kuongezeka Kwa ladha na harufu nzuri ya magome.
4. Kama ikiwekezwa Kwa miaka kuanzia 8 hutoa mapato makubwa Sana kama ifuatavyo .
Mti mmoja hutoa kilo 40 za magome yaliyo komaa , majani kiasi cha kilo 200 ambayo pia unaweza kuvuna kila mwaka baada ya mwaka wa tatu tangu kupanda, pamoja na mbegu zake.

Kwa idadi ya miti 380 Kwa ekari, kiasi cha magome ni kilo 15200 (tani 15.2).
5. Bei Kwa kilo moja ya magome ya mdalasini ni shilingi za kitanzania 8500/kg (bei ya wanunuzi wa ndani) bei huwa ni 9500/kg Kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi ambao ni wengi na wa uhakika.
6. Makadirio ya mapato ghafi Kwa ekari ni shilingi milioni miamoja na ishirini na tisa (129,000,000 Tshs).

Gharama za miche ni shs 2600 Kwa kila mche ambayo huuzwa Kwa oda.

Tunatoa huduma bure (Kwa wateja wa miche) Kwa msaada wa namna ya kuotesha shambani, kuhudumia, kuvuna na MASOKO ambayo yanasuburi Kwa hamu kubwa.

Wasiliana nasi kupata miche Kwa namba
+255762967548
+255699589177
Website: Для просмотра нужно войти или зарегистрироваться
Email. nehemiahedward7@gmail.com
Morogoro mjini, Mjimpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom