Panapo Tume Huru: CHADEMA hata wakisimamisha sura mpya kwa asilimia 70 bado watashinda viti vingi tena kuliko ilivyokuwa mwaka 2015

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Tunachopaswa kutambua ni kuwa CCM imechokwa na watanzania walio wengi na ndio maana tangu enzi za NCCR, CUF na leo CHADEMA upinzani umeendelea kukua sababu kubwa ni watu kutafuta vyama mbadala vya kuviunga mkono na kuachana na CCM.

Walipoivuruga NCCR watu hawakurudi CCM bali walitafuta vyama mbadala na pia na hata leo hii wakivuruga CHADEMA (ingawa sioni uwezkano)wafuasi wa CHADEMA hawatarudi CCM bali watatafuta vyama /chama mbadala. lakini sio kurudi CCM.

Hata hawa ambao leo hii wanajiuzulu na kuhamia CCM, wengi wao hawakuwa na majina ya kuwafanya wauzike bali wengi walibebwa na chama kwasababu wananchi walitaka watu kutoka chama tofauti na CCM(mabadiliko) na ndio maana kwa baadhi ya maeneo kulikuwa na kauli za kuchagu hata jiwe kuliko kuchagua mgombea anaetokana na CCM.

Ni kwasababu hii, hata mwaka wa 2020 CHADEMA wakisimamisha sura mpya kabisa hata kwa asilimia 70 na tukawa na Tume Huru au tukawa na sheria mpya ya uchaguzi, nina hakika CCM itashindwa vibaya tena katika maeneo mengi kuliko ilivyokuwa mwaka 2015.

CCM hii chini ya Magufuli ni poor sana katika kufanya siasa na ni poor vile vile katika kuvutia wapiga kura na CCM hii ya Magufuli kwa kauli na matendo ni mtaji mzuri sana kwa wapinzani mara kumi kuzidi CCM iliyokuwa chini ya Kikwete.

Hivyo, wanachohitaji CHADEMA leo hii ni watu wachache tu waendelee kuwepo katika chama na hawa bila kuficha ni watu kama Lisssu, Mbowe, Lema na wengineo ambao watotosha kabisa kubeba image ya chama na kukifanya kishinde.

Wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, wanafunzi wa vyuo, wastaafu, matajiri,n.k, hawatakauwa na hamu na CCM wala mgombea wa CCM hata kama mwanzoni alikuwa CHADEMA.

CCM ya Magufuli haina mtaji wa watu kwani imejitenga na matatizo na shida za wananchi na badala yake serikali yake yote sasa imegeuka kuwa ni wizara moja tu ya Miundombinu na Uchukuzi kutokana na vipaumbele vyake.

Kwa mazingira haya,ni vigumu CCM hii kukubalika na wananchi wanaoteseka na hali ngumu ya maisha huku wakiona drama za watu kupiga picha kwenye dreamliner na vitu vya aina hiyo.

Tarime na Buyungu teyari wameonyesha picha halisi mbali na utafiti wa Twaweza.
 
Last edited:
Tunachopaswa kutambua ni kuwa CCM imechokwa na watanzania walio wengi na ndio maana tangu enzi za NCCR, CUF na leo CHADEMA upinzani umeendelea kukua sababu kubwa ni watu kutafuta vyama mbadala vya kuviunga mkono na kuachana na CCM.

Walipoivuruga NCCR watu hawakurudi CCM bali walitafuta vyama mbadala na pia na hata leo hii wakivuruga CHADEMA (ingawa sioni uwezkano)wafuasi wa CHADEMA hawatarudi CCM bali watatafuta vyama /chama mbadala. lakini sio kurudi CCM.

Hata hawa ambao leo hii wanajiuzulu na kuhamia CCM, wengi wao hawakuwa na majina ya kuwafanya wauzike bali wengi walibebwa na chama kwasababu wananchi walitaka watu kutoka chama tofauti na CCM(mabadiliko) na ndio maana kwa baadhi ya maeneo kulikuwa na kauli za kuchagu hata jiwe kuliko kuchagua mgombea anaetokana na CCM.

Ni kwasababu hii, hata mwaka wa 2020 CHADEMA wakisimamisha sura mpya kabisa hata kwa asilimia 70 na tukawa na Tume Huru au tukawa na sheria mpya ya uchaguzi, nina hakika CCM itashindwa vibaya tena katika maeneo mengi kuliko ilivyokuwa mwaka 2015.

CCM hii chini ya Magufuli ni poor sana katika kufanya siasa na ni poor vile vile katika kuvutia wapiga kura na CCM hii ya Magufuli kwa kauli na matendo ni mtaji mzuri sana kwa wapinzani mara kumi kuzidi CCM iliyokuwa chini ya Kikwete.

Hivyo, wanachohitaji CHADEMA leo hii ni watu wachache tu waendelee kuwepo katika chama na hawa bila kuficha ni watu kama Lisssu, Mbowe, Lema na wengineo ambao watotosha kabisa kubeba image ya chama na kukifanya kishinde.

Wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, wanafunzi wa vyuo, wastaafu, matajiri,n.k, hawatakauwa na hamu na CCM wala mgombea wa CCM hata kama mwanzoni alikuwa CHADEMA.

CCM ya Magufuli haina mtaji wa watu kwani imejitenga na matatizo na shida za wananchi na badala yake serikali yake yote sasa imegeuka kuwa ni wizara moja tu ya Miundombinu na Uchukuzi kutokana na vipaumbele vyake.
Endelea kuota eti CCM imechokwa na watu wengi!!! Nafikiri uelewa wako mdogo sana na umekaa kwenye mitandao tuuu mkuu jaribu kutembea kidogo huku mikoani ndiyo utajua usahihi wa mambo!
 
Kama mnajiamini, kubalini Tume Huru.
 
Back
Top Bottom