Panapo majaliwa mwakani nitajiunga rasmi na siasa za nchi hii. Je, ungependa nifanye siasa na chama kipi?

Kwenye Lugha kuna kitu kinaitwa Visawe (Synonyms), yaani maneno tofauti kimatamshi na kimaandishi lakini yanayorejelea maana moja au maana inayokaribiana. Kwa mfano neno Pesa, Hela, mkwanja n.k.

Neno Ukombozi Kwa lugha ya kingereza hasa kwenyw Muktadha wa Siasa na utawala litatumika kama Liberation, ambapo litahusu kuwafanya Watu wawe huru kutoka kuwa wafungwa au watumwa na kuwapa Haki Sawa na nafasi Sawa katika kuyafanya Maisha Yao.

Katika Muktadha wa kidini, neno Ukombozi litatumika kama Redemption au Salvation. Ambapo litakuwa na maana ileile ya kuwapa Watu Uhuru lakini katika kipengele cha Nafsi au Roho.

Liberation, Redemption, Salvation ni Visawe vinavyorejelea maana ya kumuweka MTU huru, yaani kumtoa kwenye janga au tatizo au changamoto Fulani na kumfanya awe Huru.

Ukombozi unahusu fikra, Roho, mwili, na Hisia.
Pia upo ukombozi wa kijamii, kisiasa, kiutamaduni, ambao wote unategemea fikra, Roho, mwili na Hisia.

Kumpa mtu wazo, Elimu, ujuzi, maarifa, ufahamu, n.k. Utakuwa umekomboa MTU huyo kifikra, Kiakili, kimtazamo, kifalsafa ambayo mambo hayo ndio huleta mambo mengine.

Hujawahi sikia ukombozi wa Mwanamke ambao ulianza miaka ya hivi karibuni, na sasa umechanganya na Matokeo tunayaona?
Ni urembaji wa maneno na kujisogeza kwa unaotaka kuwagonga makwenzi tu.Hamna cha ukombozi wala nini!Mkombozi?Wa nini?
 
Kwema Wakuu!

Baada ya kuzifuatilia Siasa za nchi hii Kwa takribani miaka kumi sasa, nachelea kusema mwakani Mungu akipenda nitajiunga na mambo ya Siasa.

Nitajiunga CCM?
Au je nitajiunga CHADEMA?
Au je nitajiunga chama gani?

Ngoja tuone mwakani.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Karibu uwanjani, kwa Tanzania, chama cha siasa kwa maana halisi ya chama ni kimoja tuu!, Tanzania tuna chama kimoja tuu cha siasa, the one and only!, vyama vingine vyote ni mfano vyama lakini sio vyama!.
Karibu
P
 
Back
Top Bottom