Panama yasitisha uhusiano na Taiwan

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
pic+panama.jpg


Panama City, Panama. Serikali imekata uhusiano wake wa muda mrefu na Taiwan na badala yake imeboresha uhusiano na China ikidai inatambua kuwa China ni moja na Taiwan ni sehemu ya nchi hiyo moja.

China inaitaja Taiwan kama mkoa wake uliojitenga miaka mingi iliyopita ambao inasema unahitaji kuunganishwa nao. Habari kutoka Taipei, Taiwan zinasema serikali imekasirishwa na hatua hiyo ya Panama kujenga uhusiano na China, lakini ikasema haitashindana na China katika kile ilichokitaja kuwa mchezo wa pesa katika diplomasia.

China ambayo hutumia mfereji wa Panama kwa safari za meli, imeongeza kuwa kiwango cha uwekezaji wake katika taifa hilo la Amerika ya Kati katika miaka ya karibuni. Desemba mwaka uliopita kisiwa cha Sao Tome kilichukua hatua kama hiyo. Mpaka sasa ni nchi 29 tu zinaendeleza uhusiano wao na Taiwan.

Kutokana na tangazo hilo la Panama, vyombo vya habari nchini China vilichapisha picha za mawaziri wa nchi za kigeni wa nchi hizo mbili wakitiliana saini. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ya China ilisema kuwa serikali ya China inakaribisha hatua hiyo ya Panama.


Chanzo; mwananchi
 
MWEZI HUU NI MWEZI WA KUSITISHA UHUSIANO,HATA MIMI NINA MPANGO NA KUSITISHA UHUSIANO WA KIDPLOMASIA NA UKWENI KWANGU
 
Back
Top Bottom