Panacea?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,022
112,707
Katiba mpya...katiba mpya...katiba mpya!! Neno katiba siku hizi limekuwa kama wimbo flani unaotamba kwa wakati flani.

Sasa limenijia swali hapa. Je tukishaipata hiyo katiba mpya tunayoililia sana ina maana matatizo yetu ndio yataisha?

Katiba mpya ndio panacea ya hali duni ya maisha tuliyonayo?
 
Matatizo hayataisha. Tutatatua baadhi halafu yatokea mengine na tutaendelea kuyatatua, ndio maisha ya kibinadamu yalivyo, huwezi maliza matatizo. Katiba mpya tunaitaka ili kutatua udhaifu na matatizo yaliyopo kwenye KATIBA YA SASA. Katiba ikishakaa vizuri, tutakuwa na uwanja mpana wa kutumia njia mbadala wa kutatua matatizo mengine ya nchi hii.

Natumaini umenielewa ki-utu-uzima!
 
Katiba mpya...katiba mpya...katiba mpya!! Neno katiba siku hizi limekuwa kama wimbo flani unaotamba kwa wakati flani.

Sasa limenijia swali hapa. Je tukishaipata hiyo katiba mpya tunayoililia sana ina maana matatizo yetu ndio yataisha?

Katiba mpya ndio panacea ya hali duni ya maisha tuliyonayo?

We mbwiga kwelikweli!!
 
Hebu uelezee basi huo umbwiga wangu kwa kinagaubaga..
Tupo kisimani na mtungi wetu tuupendao kuteka maji.
Lakini kila tunapojaza maji mtungini, maji yanavuja na hatufiki nayo maji nyumbani kwa kiwango tulichotarajia.
Mtungi wetu UMETOBOKA na tumekuwa tukijitahidi kuziba lakini matundu bado yapo!
Viraka ni vingi mpaka inatia KINYAA!!!!!
Kuna ubaya gani tukitafuta Mtungi MPYA!
Kweli hapo sio mwisho wa matatizo, sababu hata njia tupitayo ina MBIGIRI kibao!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom