Pana chuo Tanzania kinatumia mfumo wa Semester wanafunzi kujiunga?

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Pana chuo tanzania kinatumia mfumo wa Semester?

Yaani kila semester pana wanafunzi wanaojiunga, na wanafunzi wanaohitimu. Masharti ya kuhitimu ni kukamilisha masomo fulani. GPA ni ya masomo, siyo kwa mwaka. Hakuna kusema huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wala wa ngapi. Mwanafunzi akitimiza masharti anahitimu. Mahafali yako kila semester. Hakuna kusema tusubiri disemba, wakati umekamilisha kila kitu Januari.

Baadhi ya vyuo vina semester jina tu. Mahafali ni mara moja kwa mwaka. Mihula wameibatiza jina kuiita semester. Kujiunga na chuo ni mara moja kwa mwaka.
 
Good to see you Mr Mlenge , zamani SAUT walikuwa na utaratibu huo, lakini kwa wanafunzi wa Post-Graduate. Utaratibu ulikuwa ni kwamba unasoma ndani ya mwaka au semester masomo kadhaa. Mfano kuna wale wanafunzi wa sheria waliosoma nje ya nchi, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali au wanasheria waliosoma zamani hasahasa mahakimu walitumia sana huu mfumo.

Unakuta amechagua masomo mawili ya mwaka wa kwanza, somo moja la mwaka wa nne na somo jingine mwaka wa tatu (Both Optional and Core Courses). Hivyo anahudhuria haya masomo yote na kufanya mitihani, akifaulu anahitimu ndani ya huo mwaka na cheti chake.

Siku hizi huu utaratibu wameufuta, sijui sababu ni nini: Binafsi nadhani ulikuwa mzuri kwasababu uliwapa watu urahisi wa kujiongeza kielimu ndani ya muda mfupi. Kuna wale wanasheria ambao walisoma miaka ya tisini na elfu mbili mwanzoni ambako mitaala yao ilikuwa na masomo machache, huu mfumo uliwasaidia kusoma masomo mapya bila kufanya Masters au Bachelor Degree.

Mfano miaka ya 90's masomo kama Public International Law, Intellectual Property Law, Tax Law, Cyber Law, Human Rights Law, Minerals+Oil+And Natural Resources Law, Legal Theory n.k hayakuwa ya lazima na hayakuwepo pale Mlimani. Hivyo njia rahisi ya wengi kuyafahamu haya masomo ilikuwa kupitia mfumo wa SEMESTER.
 
Hapa bongo kuna mfumo wa NTA level ambayo ni made up na semester 2 ambapo kuna award yake so unaweza pata cheti ukihitaji.

Kuna baadhi ya NTA level zinafika 2 years yaani 4 semisters
 
Back
Top Bottom