Pamoja na yote huenda Tundu Lissu akafukuzwa CHADEMA kama Zitto

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Tundu Lissu ni nani ndani ya CHADEMA? nani wanaomuunga mkono ndani ya CHADEMA? Pengine nianze kwa kujibu maswali hayo hapo juu. Tundu Lissu ni Mwanachama na Mwanasheria wa CHADEMA na kwa sasa amejijenga kwa kuibua utata kila uchao si tu dhidi ya serikali bali utata wake ni mkubwa sana ndani ya chama chake cha CHADEMA husuasani kwa viongozi na wafadhili wakuu.

Tundu Lissu ndani ya CHADEMA anaungwa mkono kwa dhati kabisa na wafuasi wasiofungamana na kundi la Mbowe na marafiki wa EL kwa lugha rahisi Tundu Lissu anaungwa mkono na wanachadema wanaotaka Mbowe na EL waondoke CHADEMA kwa sababu ya makandokando yao.

Kundi la marafiki wa EL, kundi hili kamwe haliwezi kumuaini Tundu Lissu japo wanamtumia katika harakati za kuwasafisha na kuwatafutia huruma ya wananchi. Ikumbukwe kuwa hawa ni wana-CCM kindakindaki ila wametafuta pahala pa kuuguza ''vidonda vyao''.

Japo Tundu Lissu alinukuliwa akiwananga miaka kadhaa iliyopita huku akitamani serikali ya JK iwafunge gerezani bila hata kuwafungulia mashitaka kwani Tundu alijigamba kuwa na ushahidi ndani na nje ya bunge dhidi ya watu hawa.

Kundi hili linamtumia Tundu Lissu kama fimbo lakini kamwe halimwamini na wala hawamshirikishi kwenye mipango yao ya siri kwa sababu wanajua ni kigeu geu, siku wakikosana hubadilisha maneno na kuongea hadharani. Kwa kifupi hawawezi kukubali Tundu Lissu awe Mkuu wa Chama.

Kundi la ''Kamanda'' Mbowe, kwa mnaofuatilia mambo mtagundua kundi la wafuasi wa Mbowe limekaa kimya likitafakari jinsi ambavyo Mwenyekiti akipingwa mitandaoni na kwenye media, hawa hawakubali. Kundi hili wamo akina Lema, Msigwa nk...hawa muda ukifika wataongoza mapambano dhidi ya Tundu Lissu kuhakikisha hapati fursa ya kuwa mwenyekiti.

Watahakikisha anasomewa mashitaka kwa hati za uongo na kutolewa hukumu. Hawa dhumuni lao kubwa ni kubaki na ''status quo'' kuhakikisha chama kinashiriki uchaguzi na kujihakikishia ruzuku na si kutwaa madaraka. Kwa kundi hili endapo Tundu Lissu akifanikiwa kuwa Mwenyekiti huenda wakakosa ushawishi kwani kundi kubwa la watu wasio mrengo wa Mbowe au Lowassa ndio watapata madaraka ya Chama ndio watakao kuwa na sauti na watchukua nafasi za uongozi hivyo hawataruhusu Tundu apenye.

Muda ndio jibu, Mustakabali wa Tundu Lissu ndani ya CHADEMA haswa katika harakati za kuukwaa uenyekiti huenda ukasababisha kuundiwa zengwe na kufurushwa chamani kama Zitto Kabwe.
21167122_1582408581821324_1689352552512160316_o.jpg
 
Chadema wanamuunga mkono Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu katika vita vya kupinga udikteta uchwara kwenye nchi yetu kila mtanzania mwenye akili timamu tunatakiwa kumuunga mkono Tundu Lissu.

Hayo mambo ya kufukuzana ningeanza huyo mwenyekiti wenu huko lumumba ameshindwa kila kitu mpaka sasa amebakia kutafuta kiki
 
Lissu hana ndoto ya kuwa mwenyekiti. Arudi jimboni kutatua shida za wananchi. Yeye kila siku anatumikia mahakama na makesi ya uchwara yasiyo na tija jimboni.
 
Si kweli,
Wanachadema wanakamatwa kila siku na Polisi.
Tundu lisu naye hayuko nyumba. Ni ajabu unamuona Tundu lisu, una wasahahu wakina bulaya and the like..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya umeshamaliza kumuota Lissu..
Muote na Fisadi aliyeiletea Nchi hasara kwa kuuza nyumba za serikali na kununua Kivuko kibovu.
 
[

Wewe acha mhemko. Kamtabirie huyo anaewanyanyasa watanzania wanaishi kama wakimbizi. Afadhali hata wakimbizi wanajua wanako kwenda kunusuru maisha yao na misaada wanapewa. Achana na kichwa cha Lissu na Chadema. Mwambie ajiandae 2020. Hapo ilitumwa msg.
 
Back
Top Bottom