mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Chadema wanamuunga mkono Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu katika vita vya kupinga udikteta uchwara kwenye nchi yetu kila mtanzania mwenye akili timamu tunatakiwa kumuunga mkono Tundu Lissu. Hayo mambo ya kufukuzana ningeanza huyo mwenyekiti wenu huko lumumba ameshindwa kila kitu mpaka sasa amebakia kutafuta kiki
Francis12, unajua maana ya Udikteta uchwara!. Au kwa maana ya Lissu ambaye anataka uhuru usio na mipaka, lakini wakati uleule:
1) Uhuru alionao wa kutisha vyombo vya habari na kuropoka hovyo na akarudi nyumbani kwake salama, ati hautoshi!
2) Uhuru tulionao humu JF wa kuandika upuuzi, kutukana na kubandika picha za hovyo, na tukabaki salama, pia hautoshi!
Wahenga walinenena ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA, bali anataka wengine wasipate kabisa. Uhuru aliokuwa nao Lissu, kwa nafasi zake kama kiongozi, hajui uhitaji wa uhuru wa watu wengine japo kero zao zitekelezwe na Serikali iliyoko madarakani. Lissu, atembelee vijijini aone hali halisi ya maisha ili apate cha kuikosoa Serikali - UZEMBE, RUSHWA, UFISADI, na wanasiasa uchwara kama yeye Lissu, ambaye yanayomgusa apate umaarufu ndiyo utawala usio wa kidikteta. Anataka uhuru wa kuzunguka nchi nzima kwa mikutano na maandamano awalishe wananchi maneno, huku matumbo yao yakibaki na njaa!
Pia imeandikwa kwenye maandiko matakatifu, Methali 27:7 Aliyeshiba hata asali huikataa, lakini kwa mwenye njaa kila kichungu ni kitamu. Kwamba ajuaye maumivu ya kiatu ni yule aliyekivaa. Lissu hajui shida na kero za wananchi bali umaarufu wake kisiasa. Watu hawatashiba kwa kuwa na uhuru wa kuongea usio na mipaka.
Kitabu hicho hicho cha Methali 27:1,2 imeandikwa 1Usijisifie ya kesho, hujui nini kitatokea leo mpaka kesho. 2Acha watu wengine wakusifu, kuliko mdomo wako wewe mwenyewe. Lissu amesema sana mazuri, mabaya, uwongo na ukweli, uzushi na umbea. Imefika wakati sasa, kama msomi kiongozi, kutafakari matokeo ya kidomodomo chake.