Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Mgogoro wa mpaka katika ziwa kati ya Tanzania na Malawi wengi wanasema unatokana na uwezekano wa kuwapo mafuta ndani ya hilo ziwa. Hivi kweli hata mafuta yakiwapo ni busara kuyachimba toka ziwa hili linalotegemewa na maelfu ya watu kwa ajili ya maji ya kunywa, mifugo, uvuvi, kuoga, kilimo na maisha kwa ujumla?
Fikiria ikitokea kuvuja kwa mafuta kama ilivyotokea Marekani, watu wangapi wataathirika? Tuna uwezo wa kuwapa watu maji mbadala wakati tukisubiri ziwa lisafishwe, kama kweli litasafishwa? Na pia hili ni ziwa la fresh water, sio maji ya chumvi kama ya bahari yenye uwezo wa kujisafisha. Kweli tuko tayari watumiaji wa hili ziwa walishwe au kunyweshwa takataka za "oil rigs"?
Angalia picha za inavyokuwa ikitokea kisima cha mafuta ziwani au baharini kikavuja.
View attachment Oil spill katika ziwaau bahari.docx