Pamoja na vyombo vya habari kutoripoti Yanga kubebwa, Azam waiandikia barua bodi ya ligi

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
15,183
20,137
Katika msimu ambao Simba wameandwamwa na vyombo vya habari kuwa wanabebwa na waamuzi ni msimu huu.Waandishi bila kujadili maadili yao ya kazi waliweka ushabiki mbele kuwa Simba inashindwa kwa kubebwa bila kuangalia upande wa pili ambao mechi zao nyingi zimekuwa na maamuzi yenye utata.

Ilifikia kipindi simba imecheza badala ya kuelezea mpira ulivyokuwa walijikita kujadili waamuzi hali ambayo ilijenga uwoga kwa waamuzi waliokuwa wanachezesha mechi za Simba na kupelekea Simba kunyimwa penati au magoli ya wazi kwa hofu ya kisakamwa au kufungiwa.

Kwa wale walioangalia mechi ya juzi kati ya Azam na Yanga walishuhudia waamuzi wakikataa magoli mawili ya wazi pamoja na kunyimwa penati baada ya Mchezaji wao kuangushwa ndani ya eneo la penati.

Vyombo vingi vya habari vilikaa kimya lakini timu ya Azam iliamua kuandika barua bodi ya ligi na kupeleka clip za mchezo huo kuonyesha jinsi waamuzi walivyoihujumu.
Bodi ya ligi imethibitisha kupokea malalamiko yao na kuahidi kuyatolea maamuzi pamoja na matukio mengine yaliyotokea toka ligi ianze baada ya kusimamishwa kwa janga la Corona.
Huu ni wakati wa kujulikana ni nani anatumia pesa ili apate matokeo
 
Ni Yanga pekee mabingwa wa kihistoria wasiolalamikia magoli ya makosa ya marefa. Zeruzeru alikuwa maarufu na screen kuuonyesha goli walizonyimwa na marefa. Binamu yao Azam kaiga.

Hivi hayo mambo hayatokei kwa Yanga? Mechi tatu za mwisho Yanga imenyimwa goli ngapi? Kelele ziko wapi?
 
refa alikuwa tayari ameisha puliza filimbi ya offside baada ya kuona kibendera kipo juu, lakini yule mchezaji mjinga akafunga tuu, alafu wajinga wengine wakiongozwa na wachambuzi wa azam sport wanalalamika eti lile ni goli halali, ila penati ya molinga hawaizungumzii…………………….
 
Utopolo walibebwa sana. Kwa vile tu utopolo hawana madhara ila msimu huu wamebebwa sana
 
Azam Wanzanzibar Chadema ikichukua Ikulu wataenda kucheza na wenzao Mlandege nk
 
Back
Top Bottom