Pamoja na utandawazi kuenea lakini bado kuna watu wananunua antivirus, windows, software za kwenye CD madukani

With all due respect,from your words,there is a very clear indication that your knowledge of ICT is not only shallow but it's non existent.
Thank you very much for your contribution that has exposed how little you know about ICT and also general ethics
Smfh
giphy.gif
 
Rafiki yangu kanunua kaspersky kwa 35k yenye MB300 halafu ina user wawili.

Anaamini kwamba antivirus za mtandaoni si salama jambo ambalo si kweli kwasababu hata hizo za kwenye CD zimetolewa huko huko kwenye mitandao

Sasa kanunua CD kafanya installation halafu sasa kwenye ku activate zile licence zinagoma so mchizi kapigwa

Technolojia inakua kila kukicha na saizi hatuko kwenye soko la CD tena kulinganisha na miaka ya nyuma. Na ndio maana PC latest hata mlango wa CD nowdays haziwekwi. Kama antivirus unataka kununua unaweza uka request licence kwenye official website ya antivirus husika tena kwa bei nzuri (japo mimi hii pia nayo sikubaliani nayo)

Nishajiwekea kiapo kwamba katika huu ulimwengu wa tech wenye manguli wakucheza na cracking software sitokuja kulipia software yeyote

Au hadi humu namo kuna watu wenye spirit hiyo ya kuamini bidhaa za kwenye maduka za mfumo wa CD ni bora zaidi na kuzidharau hizi za mtandaoni?
Unapotumia software ambayo ipo Cracked that means hata zile official terms and security za software husika wewe hazikuhusu.. hata kama unaweza ona hupati virus Bado Kuna namna wanafaidika na wewe hasa kwenye kuiba taatifa zako pasipo wewe kujua.

Ndo maana ofisi za serikali huwa zinatumika software ambazo ni genuine.

Kutumia software ambazo ni cracked ni risky kama ni mtu ambae unapenda privacy.. unless ujue jinsi ya kujilinda kwenye taarifa za ulizo tunza kwenye kifaa husika.

Ni sawa na wale wanaotumia Gb What's up.. wanajionaga wameyapatia Sana maisha ila ukweli ni kwamba wao ndo wamepatikana vibaya mno..!!
 
hapo ukishakua na KRT CLUB mchezo kwisha, unaipelekesha kaspersky unavyotaka wewe

mimi nilitaka siku moja kulipia resseter adjustment ya epson baada ya kuitafuta full vrsion kwa muda mrefu bila kuipata. lakini siku hiyo baada ya kupiga misele kwenye chocho za crackers nikakutana na ma crackers hao wana balaa, mpaka leo naitumia
Jamaa tuelekezane hilo chocho man hali za kiuchumi kwetu ni ngumu
 
Kutumia cracked softs inategemeana na ni nini unachoifanyia hiyo PC yako.

Kwa mfano mtu anayeitumia PC yake kwa kuhifadhia mambo yake ya "muhimu" sana au mambo ya kifedha huwa anaepuka kutumia cracks.

Na akitumia cracks baada ya kushindwa kabisa kumudu gharama za kununua genuine software, basi huwa haendekezi cracks.

Lakini kama PC inatumika kwa mambo ya kawaida tu, wewe jaza hayo macracks.

Siyo kwamba situmii Cracks "No!" Ila ndivyo ilivyo.

NB: Kulingana na makala mbalimbali nilizowahi kupitia kuhusu kama cracks ni salama,

Niligundua kwamba kuna baadhi ya cracks hufanya kile mtengenezaji wake alichokusudia hiyo crack ifanye na kuna cracks zingine huonekana kutatua hitaji lako huku zikilenga pia kufanya uharibifu au kufanya vitu vingine ambavyo si vizuri ndani ya PC yako.

Ushauri: Kama unajiweza kiuchumi uwe na PC mbili. Moja inayotumia hayo macracks na ya pili iwe na software za kawaida.

Au PC yako iwe na "Dual OS"

Mimi hutumia hayo ma-cracks kwenye Windows 10.
Na LinuxMint naitumia kwa ajili ya Internet surfing na kuingia kwenye accounts zangu muhimu za internet maana siyo websites zote ni mobile phone friendly.


Sent from my cupboard using mug
Mkuu hii initial yako ya mwisho inanifurahisha balaa
 
Tumieni angalau hoja defensively kutetea hizo patched software, ama kweli katika hoja ambazo naziona ni very weak ni hii dhana ya kuhisi watu wanaotumia cracks hawana uwezo kifedha.

Huku ni kufikiri kizamani sana tena bila kushirikisha ubongo yaani mtu ambaye ameweza ku afford akanunua pc ya laki 5 ashindwe kununua CD ya antivirus ya 35 yenye 2 users?


Hapo umepwaya mzee kwasababu mimi sipendi kuwa limited kwenye bidhaa niliyoilipia wakati sehemu nyingine najua naweza pata full access ambayo niko huru (tena for free). Haiwezekani uniuzie godoro bei juu halafu uninyime usingizi

Mfano mimi sipendi iphone kulingana na limitation zake kwasababu kuna upande wa pili (android) hizo services ni free na huwekewi limit, sasa anakuja mtu kama wewe anasema sipendi iphone kwasababu sina gharama za kuimudu

Inawezekana kweli ni kawa sipendi iphone kwasababu sina gharama lakini sometimes sio kila anayetoa pesa bila mpangilio au kimahesabu ahesabike kama ni mkwasi, mda mwingine unaweza ukatoa pesa kwasababu hauna ujuzi wa kujua kua hicho unachokinunua kuna mahali kina patikana for free bila kujibana

Ebu icheki hii, nachukua 35k nanunua antivirus yenye 2 users tayari ishakuja na limit kwamba hata ikitokea nimepiga windows mara tatu basi sitaweza ku run hiyo antivirus tena. Wakati ukiwa na crack hauwi limited muda wowote utaojiskia kupiga window au kufanya mabadiliko yoyote haupati hiyo bugdha.


Bora hata ambao wanaosema cracks ni illegal kwasababu haina hati miliki na pia haimfaidishi official developer
Hoja ya umasikini inabaki palepale. Kunasoftwere zinauzwa m2 na hadi m4. Mfano pc nayotumia nina program moja ina gharimu 2m nyingine 1.2m nyingine dola 350. Hizo ni baadhi tu. Bila cracks hali ingekua ngumu. Umasikini shida
 
Haki ya kweli ipo kaburini, hata humu jf kuna payments kwanini usifanye hivyo ukata hata u platnam member kama kweli hutaki vya bure?

Mnajifanya hamtaki vya bure wakati kuna watu wanameza ARV ambazo zinatolewa bure

Kama kweli unazingatia itifaki utagundua hata ku stream hizo ngoma online nako ni kudidimiza haki ya msaniivile vile kwasababu ungeweza kuzinunua official


Wewe unafurahia ku stream nyimbo online bure ukihisi kufanya hivyo ni kusuport kazi ya msanii wakati mimi nimenunua album ya dizasta kwa pesa taslimu (nauhakika katika career yako hujawahi kununua album ya mwanamziki)
Uko sahihi
 
Wengine humu hata hiyo OS ya windows iko activated na KMS Autonet unless otherwise wawe wanaactivate kila baada ya miezi sita.
Ila kama mnabahatika kusoma zile Readme za crack huwa wanasema kuwa "support the developer if you use the software"
 
Software za kucrack siyo nzuri, mimi nikiwa na uwezo wa kununua software ambazo hazizidi 50 - 80$ nanunua tu, leo nimetoka kulipia software ya doodly 64$.
Asicho kijua mtoa mada ni kwamba unacho nunua kwenye CD sio software package bali ni activation keys hivyo unaweza ukaachana na package ya kwenye CD una download updated package halafu uka activate kwa hizo hizo keys

Software za wizi (cracked) sio nzuri kama unafanya kazi ya software kwa biashara.

Huwezi kumuwekea mteja wa kampuni,taasisi au shirika antvirus au operating system cracked utaaribu kazi ya watu.

Hizo wawekee watengeneza singeli wa mtaani huko kwenye pc zao na waingiza nyimbo kwenye memory huko ila sio kwa kampuni au taasisi au shirika ,
 
Back
Top Bottom