Pamoja na uimara wake, CCM sasa inabidi ipumzike! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na uimara wake, CCM sasa inabidi ipumzike!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Sep 5, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,098
  Likes Received: 1,483
  Trophy Points: 280
  Toka tuanze mfumo wa vyama vingi nimekuwa nikivifatilia vyama vyote lakini chama tawala bado kimeendelea kuongoza kimuundo kwani kimekuwa na mizizi toka ngazi ya chini kulinganisha na vyama vingine pia ni chama ambacho kimeweza kusambaa tanzania nzima na ndio maana imeweza kuvishambulia vyama vingine ni vya kikabila au kidini.

  Uimara wa CCM umechangiwa na kuwa chama pekee ambacho kina makada waliofundishwa ingawa baada ya kuingia vyama vingi walianza kupokea wanachama wa papo hapo mtindo ulioanzishwa na mrema huko kigoma wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani vyama vingine vimeendelea kukusanya wanachama ambao wengi hawajui hata itikadi ya vyama husika kwani hawapewi mafunzo yoyote.

  Pamoja na sifa zote hizo chama hicho kilianza kupoteza mwelekeo pale kilipovunja azimio la arusha na kuja na azimio la zanzibar ambalo kwa kiasi kikubwa kiliua maadili ya uongozi. Ingawa kiliua maadili ya uongozi kilizidi kupoteza mwelekeo pale kilipotengeneza mtandao wa kumwingiza rais aliyeko sasa madarakani.

  Kwa sasa wale makada waliokuwa wakitetea chama hawapewi nafasi badala yake wapambe wa viongozi wamekuwa ndio wana sauti mtindo uliopewa nguvu wakati wa uongozi wa yusuph makamba.sasa hivi viongozi wengi wa CCM wamekuwa wakiwaza kutengeneza safu ya uongozi kwa ajili ya urais (mitandao) badala ya kutumikia wananchi na kwa wale waliopewa dhamana wamekuwa wakiwaza namna gani watajinufaisha wao binafsi, familia zao na jamaa zao imekuwa kawaida mtu anapoteuliwa kiongozi muda mfupi anakuwa na ukwasi wa ajabu. Pamoja na yote hayo bado chama hicho kimebaki na hazina ya viongozi kwani hata wakati wa uchaguzi wabunge wengi wa upinzani ni wale walioenguliwa toka ccm tukianzia na yule anayeisumbua CCM kwa sasa Dr. Slaa.

  Pamoja na kuelewa vyama vya upinzani bado vichanga lakini kwa hali tuliyoifikia hivi sasa CCM haiwezi kujirekebisha mpaka tuiweke pembeni ili wajue ni nini wananchi walichokuwa wanahitaji toka kwao. Kwani sasa hivi nchi inaendeshwa kienyeji mno kuanzia ugawaji wa vyeo hauzingatii sifa bali kujuana na nani ni mpambe wangu.

  Rushwa imehalarishwa kuanzia rushwa ya ngono sasa hivi tunashuhudia dada zetu na mama zetu wanavyojirahisi ili tu wapate nafasi za uongozi au kisiasa pamoja na rushwa nyingine na tatizo hili ni kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu (mfumo mzima umeoza) wizi umehalalishwa kwa ngazi zote juu hadi chini leo hii ni fahari mtu kuoneka au kuwa tajiri bila kujulikana huu utajiri ameupata kihalali au la.serikali kuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua hata pale inapoonekana makosa dhairi yametendeka kwa kutaja machache meremeta, kagoda,tbs, pesa zilizofichwa uswisi, rada.

  Mmonyoko mkubwa wa kimaadili kupitia baadhi ya vyombo vya habari, kushindwa kulinda na kusimamia rasilimali za taifa kama madini, maji, gesi na ardhi na pia kushindwa kutoza kodi stahili kwa makampuni ya migodi na simu. Kuruhusu uchochezi wa kidini na pia kushindwa kusimamia muungano. Kuendelea kwa mauaji yanayofanywa na polisi bila kuchukua hatua za kimsingi.

  Makosa yaliyopo yapo mengi sana lakini tukifanya kosa kuendelea kuichagua CCM haaitajirekebisha kamwe badala yake inabidi tuiweke kando ili wale walioivamia CCM wajichuje na kikirudi kiwe chama kilichozaliwa upya.
   
 2. m

  mamajack JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hawna uimara wowote,sema udhalimu umekuwa ukiwapa nafasi ya kuwakandamiza wananchi wa tz.umaarufu uliisha tangu walipomuua mwalimu julius kambarage nyerere.
  Wakaharalisha wizi na mauaji ya hadhalani.
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Dr. Azavael Lwaitama alisema kuwa, tutafute namna ya kuwaelewesha ccm kwamba jambo la kupisha chama kingine madarakani ni jambo la kawaida tu.

  Hivyo basi, ccm wasijiskie vibaya kukaa pembeni na kushuhudia chama kingine kikishika dola kwani siasa za leo ni tofauti na za jana,
  Ni vema ccm wasikwazike kukaa bench kwani sio muda wote wanaweza kuwa sawa, wakubali kukaa pembeni ili wajipange upya.
  Kupisha chama kingine kushika dola sio swala la kejeli, ni mfumo wa kawaida kabisa ktk demokrasia.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Watanzania wote tulio kwenye judicial reform movement tunaishi kwa wasiwasi na mashaka kwani hatujui nini hasa kinachojadiliwa ndani ya vikao vya ccm ili kuifanya iendelee kutawala. Sio siri tena Ccm imekumbwa na kiwewe baada ya kushtuka inaweza kutolewa madarakani mwaka 2015 au ikiwezekana kabla ya hapo kwa jinsi mambo yanavyokwenda.Mauaji yanayoendelewa kuhasisiwa na Ccm na Polisi wake yametutia mashaka makubwa kama kweli Ccm ipo tayari kuondoka Madarakani kwa amani kama Majirani zetu Kenya na Zambia walivyofanya.

  Mimi binafsi nimezungukwa na wimbi la wana Ccm wasioaminika na kwa upande mwingine ninajipa moyo nikimtumainia Mungu kuniokoa mimi na familiya yangu kutoka mikono miovu ya hawa wasaliti wa Taifa letu.Kama wewe ni mmoja wa wazalendo wa taifa letu utasoma hii,na kama wewe sio mzalendo wa taifa letu basi utakuwa mmoja wa wasaliti wakubwa wa taifa letu,ujumbe wangu kwako chimbia kichwa chako kwenye mchanga ili usisikie kilio cha wapigania haki wan chi hii!

  Kila kukicha ninajiuliza inakuwaje wapiga kura ambao ndio wenye nguvu ya kuiongoza serikali wanashindwa kuiwajibisha serikali iliyoundwa na wao wenyewe?hivi wapiga kura wana nguvu ya kuiondoa serikali madarakani?hivi serikali ingejuwa wapiga kura wana nguvu ya kuindoa madarakani wangefanya mambo wanayofanya?Nini kinatokea pale walio madarakani wanakwenda kinyume na makubaliano waliowekeana na wapiga kura?hivi kuna vitu Serikali wanafanya ambavyo kama wangejua wapiga kura wana nguvu wasingevifanya?

  Inakuwaje pale waandishi wa habari wanaposhindwa kuandika taarifa za ukweli kuhusu serikali inavyoendeshwa?wapiga kura wanabakia gizani!matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona,waandishi wa habari wanaojitahidi kuueleza umma ukweli wanauwawa,mfano mzuri Daudi Mwangosi,na ikiwa serikali inapata nguvu ya kutosha inafungia magazeti mfano mzuri Mwanahalisi! Serikali hii inajua wazi ikiachia uhuru wa waandishi wa habari kuandika ukweli watanzania wengi wataelewa na wataamka kutoka usingizini na itakuwa ndio mwisho wao,kwa hilo napenda kufikisha ujumbe kwa hawa wadhalimu is too late!watanzania walishaelewa nini kinaendelea!

  Ukiangali jinsi TBC ambayo ni mali yetu wote watanzania inavyoendeshwa utagundua jinsi wanavyojitahidi kutuweka gizani na kutaka tusielewe jinsi serikali hii inavyoendeshwa,ndio maana waziri anaweza kwenda ulaya na kusaini mikataba ya nchi yetu akiwa bar!ni jambo la kawaida kwa serikali yetu!

  Napenda kuitangazia serikali ya ccm hatupo tayari kuwaachia waendelee kutawala nchi yetu kwa ubinafsi wa kukabidhiana madaraka na kulindana huku wakitamani kuendelea kutawala na kusahau taifa letu lina idadi ya watu million45, kwa idadi hii ya watu tuna haki ya kuchagua wale wenye sifa za kutosha kuongoza nchi yetu kwa faida ya vizazi vijavyo na vya sasa
   
 5. m

  mamajack JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wananchi inabidi tuwe macho na hawa wezi wa raslimali zetu,kampeni zitajaa rushwa na mambo mengi ya ajabu,huki vijijini wananunua kadi za kupigia kura,ananchi katika kijiji fulnani waliuza shahada zao kwa 2000.ona walivyotumia umaskini wetu!!!!!makosa yale ya mwaka 2010 yamezaa mateso makubwa sana kwa watanzania.naamini hayatajirudia tena.
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ipumzishwe tu.
   
 7. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uimara upi wa CCM au umekosea heading?
   
 8. S

  Stabilaiza JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 1,672
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Sasa ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi na serikali yake kimepoteza nguvu na ushawishi wa kuongoza nchi yetu. Dhamiri za wana-CCM sasa zimeshawahakikishia kuwa wamepoteza uhalali wa kuongoza nchi yetu. Mauaji ya raia waisokuwa na hatia yanayofanywa na polisi ni mkakati wa CCM wa kukataa kukabidhi madaraka kwa wananchi kwa amani. Wananchi wameshaamua kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kidemokrasia. Lakini CCM inaonekana haiko tayari kuachia madaraka hata kama wananchi hawakitaki tena CCM.

  Kulishawahi kutolewa mada ikibashiri kuwa kabla CCM haijatoka madarakani itasababisha mauaji ya watanzania wengi. Bahati mbaya uzi huo haukudumu ukanyofolewa sijui ni kwa maslahi ya nani. Lakini niseme tu kwamba wahariri wa jukwaa hili la siasa wafahamu kuwa mada zinazowasilishwa kuikosoa CCM zinania njema ya kuepusha mauaji ya halaiki yasitokee Tanzania. Sababu ziko nyingi za CCM kung'ang'ania madaraka. Sababu kubwa ni kwamba wanasiasa wa CCM wamegeuka kuwa mafisadi na mawakala wa ubeberu. Hawako tayari kuachia madaraka kwa amani kwa sababu wanataka kulinda mali zao walizochuma kwa wizi. Nachowaambia CCM ni kuwa Tanzania ni nchi ya watanzania siyo mali binafsi ya CCM. Hivyo CCM wajiandae kukabidhi madaraka kwa njia ya amani kuanzia sasa, wasing'ang'anie madaraka na kutumia vyombo vya dola kunyanyasa, kutesa na kuua raia wa Tanzania wasiokuwa na hatia yoyote.
   
 9. S

  Stabilaiza JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 1,672
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Mods tafadhali uzi huu ukae pekeyake, usinganishwe
   
 10. S

  Stabilaiza JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 1,672
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Sasa ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi na serikali yake kimepoteza nguvu na ushawishi wa kuongoza nchi yetu. Dhamiri za wana-CCM sasa zimeshawahakikishia kuwa wamepoteza uhalali wa kuongoza nchi yetu. Mauaji ya raia waisokuwa na hatia yanayofanywa na polisi ni mkakati wa CCM wa kukataa kukabidhi madaraka kwa wananchi kwa amani. Wananchi wameshaamua kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kidemokrasia. Lakini CCM inaonekana haiko tayari kuachia madaraka hata kama wananchi hawakitaki tena CCM.

  Kulishawahi kutolewa mada ikibashiri kuwa kabla CCM haijatoka madarakani itasababisha mauaji ya watanzania wengi. Bahati mbaya uzi huo haukudumu ukanyofolewa sijui ni kwa maslahi ya nani. Lakini niseme tu kwamba wahariri wa jukwaa hili la siasa wafahamu kuwa mada zinazowasilishwa kuikosoa CCM zinania njema ya kuepusha mauaji ya halaiki yasitokee Tanzania. Sababu ziko nyingi za CCM kung'ang'ania madaraka. Sababu kubwa ni kwamba wanasiasa wa CCM wamegeuka kuwa mafisadi na mawakala wa ubeberu. Hawako tayari kuachia madaraka kwa amani kwa sababu wanataka kulinda mali zao walizochuma kwa wizi. Nachowaambia CCM ni kuwa Tanzania ni nchi ya watanzania siyo mali binafsi ya CCM. Hivyo CCM wajiandae kukabidhi madaraka kwa njia ya amani kuanzia sasa, wasing'ang'anie madaraka na kutumia vyombo vya dola kunyanyasa, kutesa na kuua raia wa Tanzania wasiokuwa na hatia yoyote.

  Mods please, this is a stay alone thread, do not combine with other threads, it has distinct message communicated. Thanks
   
Loading...