Pamoja na ufaulu kidato cha Nne kuongezeka zaidi ya nusu wamepata div 4

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Wakati matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa Januari 15 mwaka huu yakionyesha ufaulu kupanda kwa asilimia 5.19, zaidi ya nusu ya waliofanya mtihani huo wamepata daraja la nne.

Kulingana na takwimu na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) watahiniwa 221,049 sawa na asilimia 50.74 wamepata daraja la nne, kati yao wasichana ni 126,773 na wavulana 94,276.

Wakati takwimu zikiwa hivyo kwa daraja la nne, jumla ya watahiniwa 61,696 walipata daraja sifuri.

Bila ya serikali kuja na mpango mahususi wa kulisaidia kundi hili kuna hatari ya kila mwaka kuzalisha vijana wengi wasio na shughuri maalumu mitaani, kwa sababu daraja la nne halimuwezeshi mtu kuchaguliwa katika shule ya Serikali.
 
Ujanjaujanja Tu
Hakuna Lolote Walioferi ni Nusu Tuseme Sasa Hivi Kuna Jipya
 
Wanakuambia division 4 sio kufeli, lkn cha kushangaza serikali inakuwa haina mpango wowote wa kuwaendeleza, labda wale wenye D kuanzia 4 ndio wanaweza kujiongeza na wakaenda Diploma mbalimbali.

Lkn ukweli ni kwamba wengi wataishia kukaa nyumbani na jalada linakuwa lishafungwa.

Unforgetable
 
Wakati matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa Januari 15 mwaka huu yakionyesha ufaulu kupanda kwa asilimia 5.19, zaidi ya nusu ya waliofanya mtihani huo wamepata daraja la nne...
Daraja la Nne sio failure ni pass.

Naomba tacita cheri cha mtu yeyeote aliepata daraja la nne kwa mwaka wowote kisha ukisome utajionea.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Daraja la Nne sio failure ni pass
Naomba tacita cheri cha mtu yeyeote aliepata daraja la nne kwa mwaka wowote kisha ukisome utajionea
Au nasema uongo ndugu zangu???
Sawa kwahiyo div 4 wamepass kwenda wapi.
 
Ndo ivo yaani asilimia kubwa wanaishia kuwa madereva toyo
Mie ni form four failure naujua msoto wa mtaani... Madogo wajiandae kisaikolojia, labda wale kwao mboga saba ndo wanaweza kuishi kwa raha
::umaskini ni adui mwenye roho ngumu, usiposhtuka Afrika utazikwa ukiwa hai
 
Wanakuambia division 4 sio kufeli, lkn cha kushangaza serikali inakuwa haina mpango wowote wa kuwaendeleza, labda wale wenye D kuanzia 4 ndio wanaweza kujiongeza na wakaenda Diploma mbalimbali.

Lkn ukweli ni kwamba wengi wataishia kukaa nyumbani na jalada linakuwa lishafungwa.

Unforgetable
yaani iendeleze mijitu iliyofeli? tuacheni utani ndugu zangu. Yaani jitu likae class miaka minne lifeli alafu uliendeleze.
 
Daraja la nne tunalazimisha kuiliita pass grade. Kikawaida kila grade inafaa kwa kitu fulani. Utaona grade 1 to 3 wakichaguliwa na tamisemi kujiendeleza. Hao daraja la 4 ni mihangaiko binafsi. Labda kama wana nafasi kule veta.
Kwa Kenya kila daraja linakupeleka level fulani ya masomo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom