Pamoja na Msimamo wa Tanzania kuhusu Urusi vs Ukraine; Ushauri wangu kukabili matokeo

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Baada ya Mataifa makubwa dunia Marekani na Ulaya kuamrisha Afrika iseme msimamo wake na ilaani oparesheni ya Urusi huko Ukraine. Tanzania imetoa kauli ya kwamba sisi HATULAANI, wala HATUUNGI MKONO vita hivyo. Tunachoshauri ni meza ya majadiliano tu. Tanzania ni mwanachama wa kikundi cha nchi masikini zisizofungamana upande wowote kilichoanzishwa enzi za Vita Baridi.

Kauli ya Tanzania inafanana kidogo na msimamo wa China, lndia, na baadhi ya nchi za kiarabu, Hii inamaana kwamba mashirikiano yetu na Urusi hayatasitishwa kwasababu ya vita hivi, Na wala mashirikiano na Marekani na Ulaya hayatasitishwa kwasabu tunashirikina na Urusi pia. Binafsi msimamo huu wa Tanzania huwa siuungi mkono. Nataka nchi iseme kama ni nyeupe iseme na kama ni nyeusi iseme. Lakini yote ni kwasababu ya utegemezi wetu hatuna namna kama nchi, lakini mtu mmoja mmoja anaweza kuwa huru. Huwa naamini unafiki wa Tanzania na Watanzania asili yake ni huu mrengo. Kijasusi kuna dhana inasema, If you are neutral in a situation of injustice, it means that you are supporting the oppressors. Hivyo tumeelewana🤣

Ok leo tuache hayo, Naomba kui-challenge serikali ya Rais Samia, Imejiandaaje kukabili matokeo ya vita hivi? Kila nikiwasiliza watawala wanatoa matamko tu kuwa bei za bidhaa zitapanda, lakini serikali haisemi inachukua juhudi zipi kukabi hayo.

Naishauri serikali kwanza itambue vita vya Urusi na Ukraine ni tofauti na Vita vyovyote vilivyowahi kupiganwa duniani tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili duniani. Utofauti huu unajengwa na sababu kuu tatu zifuatazo;

Mosi, Ni vita inayoihusisha Urusi ambyo ni mdau mkuu wa uchumi wa gesi na mafuta duniani ambao ndio msingi wavuchumi wote duniani.

Pili ni vita inayoihusu Marekani moja kwa moja kuwa upande unaopigana na Urusi na hivyo kushinikiza mataifa mengi duniani yashiriki kuweka vikwazo ambavyo sasa vinaathiri hata nchi ambazo hazihusiki na vita. Tafsiri rahisi nikuwa ni vita kati ya Marekani vs Urusi

Na tatu hii ni vita ambavyo Umoja wa Ulaya kwa ujumla upo kinyume na Urusi inayoendesha vita hivyo, ukilinganisha na vita zingine zote ambapo EU kila vita iliyoendeshwa na Marekani ilikuwa upande wa Marekani au ilikaa kimya na kufanya vita hivyo visiathiri dunia, Sasa leo umoja wa Ulaya nao umeweka vikwazo kwa urusi ambayo ni mzalishaji na msafirisha wa 40% ya mshitaji yote ya gasi na mafuta Ulaya. Tafsiri yake ni vita kati ya Urusi vs USA+EU+Ukraine.

Hapa ndipo unaona sasa kupanda kwa mfuta na gesi duniani kunatokea kwa nguvu kubwa baada tu ya hivi vikwazo, Ulaya na Marekani sasa wanaugulia makali hayo, na jana galoni ilifika dola 6 ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya Marekani. Lakini naamini Wazungu wao wanaweza kupata alternative mapema, lakini sio hapo tu, baada tu ya vikwazo, Urusi imeshikilia ndege zaidi ya 600 za Mataifa ya Marekani na Ulaya ambazo zilikuwa zinafanya biashara katika anga la Urusi nyingi zilikuwa za kukodi na za matajiri kadhaa wa Marekani na Ulaya, hali hiyo imeyumbisha uchumi na na soko la anga ulimwenguni. Kwa namna yoyote vita hii itakavyoisha ukiachiliambali kwamba itaondoa utawala wa Zelensk, nafikiri itabadili mwelekeo wa dunia kisiasa na kiuchumi,

Je Tanzania ambayayo uchumi wao unastawi kwakutegemea mwelekeo wa mafuta na gesi katika soko la dunia, nini Serikali imejipanga kukabili? Nafikiri option ya kwanza kwa makusudi, ili kuzuia mfumko wa bei, gharama ya maisha na uhaba wa bidhaa hasa za majumbani, serikali ichukue jukumu la dharula la kuyalinda makampuni makubwa ya ndani ya uagizaji mafuta, na viwanda vikubwa vya uzalishaji bidhaa muhimu za ndani. Mfano serikali inaweza kutenga 1.5trilioni tu na kuyapa makapuni hayo kama stimulus package ili yaagize na kuhifadhi akiba ya kutosha angalau hata miezi 18 mbele.

Pili serikali itazame viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa za ndani ambabazo ni mahitaji ya lazima ya kila siku ya Watanzania (mafuta yakula, sukari, chumvi, cement, nondo, bata nk) navyo vipewe stimulus package kwa utaratibu maalumu ambao return yake inaweza kuwa katika kodi badae au katik muindo wowote ambao serikali itaweza kuthibiti upotezvyo wa stimulus package hiyo.

Kwakufanya hivyo serikali itadhibiti mfumko wa bei na ukali wa maisha utakotokana na kupanda kwa bidhaa duniani.

Pata Kitabu cha Ujasusi kwa bei ya 80,000/= tu. Dar ni free delivery,
Nje ya Dar nauli ni 8,000/=

Nunua sasa kwa;
LIPA NAMBA TIGO 7489022
LIPA NAMBA VODA 5352627

Wasiliana nami kwa 0715865544

Pia Soma vitabu vyote (Soft copy) vya Yericko Nyerere kwa 5,000/= tu kwa wiki kupitia App bora kabisa ya Vitabu Tanzania. Pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote kupitia Play store Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play


IMG_20220324_122633_483.jpg
 
Umenena ukweli mkuu,hata mimi sipendi msimamo wa kinafiki kama huu ambao unasema mimi hayanihusu..

Tanzania ilaani uvamizi wa Nchi huru ..

Daima nitasimama upande wa beberu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom