Habari wana Jamvi, Mbunge wa jimbo la Rorya mh.Lameck Airo ni miongoni mwa wale waheshimiwa ambao ni nadra sana kusikia michango yao bungeni, haya ni mapungufu yake. Nimesikitika kusoma habari kuwa jirani yake mbunge wa Tarime mh.Nyambari Nyangwine ameshindwa hata kusaidia ktk ukarabati wa vyoo vya shule ya sekondari Nkende iliyo karibu na nyumbani kwake hadi kupelekea shule kufungwa, kisa na mkasa eti hakupata kura maeneo hayo, huyu ni tofauti na mh. Lameck ambaye husaidia bila kujali ili mradi tukio liko ndani ya jimbo lake, katika hili napenda kumpa heko mh. Lameck Airo