Pamoja na mapungufu yake kwa ujumla, Mzee Kikwete alikuwa bora kuliko Rais Magufuli

A
Sasa ikawaje tena mkaenda kumshtaki ICC.??
Akili zimewakaa sawa, chezea mwamba wewe🤣
 
Hilo halina ubishi, kuwa Kikwete alikuwa bora zaidi kuliko huyu Magufuli

Kigezo pekee cha kumfanya kiongozi kuwa bora ni namna anavyoruhusu Uhuru wa kutoa maoni na kuruhusu vyama vya kisiasa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba

Huyu tuliye naye hivi sasa haruhusu Uhuru wa mawazo na vyama vya kisiasa vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa kwa mujibu wa Katiba ya nchi

Kwa maana hiyo ni lazima yeye aonekane mbovu, kwa kuwa anaisigina Katiba na kuruhusu wateule wake wajimwambafai kwa hiyo waishi wakiwa na "impunity"

Refer kesi za akina Paul Makonda, Albert Chalamila, Ole Sabaya, Mrisho Gambo na Alli Hapi
Wewe utakua walewale waliokua wanufaika kipindi hicho na sasa mfereji umekatwa na utawala imara wa sasa hivi
 
Nchi hii imebahatika kuwa na Marais wawili tu
Mwalimu Nyerere na Benjamin Mkapa
Hizi takataka zingine hovyo kabisa.
Enzi za JK
-Hakuwahi kupiga ufisadi wa trilioni 2.4 hata kama ungeunganisha EPA, ESCROW na RICHMOND

-Hakuna mfanyabiashara aliyehamisha biashara kama hivi sasa.

-Watumishi wa umma waliongezewa mishahara na kupandishwa vyeo kila mwaka tofauti na ilivyo leo. Wakat anawaaga Mei Mosi 2015, aliwaambia atawaacha vizuri. Na kweli July aliwaongezea mshahara ambao ndo wanatembela hadi leo.

-Wakulima wa korosho hawakuwahi kudhulumiwa na serikali.

-Ajira za moja kwa moja kila mwaka wala si za kuomba kama leo.

-Deni la taifa halikupaa kwa spid ya bombadia.

-Bei za bidhaa mtaani zilikuwa chini tofauti na hii leo.

-Hotuba za kila mwisho wa mwezi zilileta matumaini.

-Wapinzani walifanya mikutano na maandamano bila kizuizi.

Yapo mengi, ni bora angerudi awamu hii hata kwa miaka miwili tu!
View attachment 1228232
Hadi watoto walimpenda
 
Hivi JK angekuwa Mkatoliki watu wangekuwa wanaandika haya leo hii? Samahani kwa wale watakaoona najaribu kuleta udini, hapana lengo langu sio udini bali kuna vitu naviona Tanzania hapa vina uelekeo wa udini na hii upelekea watu kuukwepa ukweli na kuandika au kushutumu watu kwa makosa ambayo hata wengine wanafanya au wamefanya. Udini wa Tanzania uko nafsini mwa watu na sio wa kusema au kuonekana bali matendo ya watu juu ya mambo mbalimbali huashiria hilo, Hii ni hatari sana na mbegu hii inaweza kuleta shida sana baadaye isipofanyiwa kazi na secret services.

Leo hii JK anaonekana takataka kwenye nchi hii, eti MKAPA anaonekana kafanya wonders kuliko JK ni kweli hapa tunasukumwa kuongea haya kwa fact au hisia binafsi?, Leo hii MWINYI anaonekana takataka kabisa kana kwamba umasikini na ujinga wa Tanzania umesababishwa na yeye bila kuangalia fact kwa kipindi alichoongoza na namna alivoachiwa hii nchi. Jamii amesahau kabisa kwamba JK NYERERE ameiongoza Tanzania zaidi ya miaka 20 huku wenzie wote mpaka sasa wameongoza miaka 10.

Binafsi kwa mtizamo wangu pasipo kuongozwa na fikra binafsi, aliyeongoza 20yrs alikuwa kwenye kipindi kizuri cha kuweka msingi ambao ndio ungekuwa muongozo karne na karne. Muongozo huo ungetumika na watanzania kizazi na kizazi bila kuteteleka, JE HUO MSINGI ULIACHWA.

Ili Tanzania ije kuendelea kuna vitu kadhaa watanzania tubadirike, TUACHE UNAFIKI (hili liko wazi kabisa),
TUWE WATANZANIA - UTANZANIA ndio agenda namba moja, misukumo ya kidini isiwe sehemu ya maisha, mpenda mtanzania mwenzio pasipo kuangalia kabila au dini yake, akishakuwa mtanzania awe nduguyo kwa hali na mali ISRAELI au SAUDIA au VATICANI au OMAN hao sio watanzania weusi bali niweupe na hawako kwa maslahi yako mweusi wa Tanzania. Kuipenda kwako ISRAELI au SAUDIA na kuchukia watanzania wenzio eti kwa sababu wao sio wa Isaeli au Saudia tambua huo ni ujinga maana hao ISRAELI au SAUDIA hawana urafiki na wewe na hawana shida na mtu mweusi bali wako kama wao kwa masahi yao hapa duniani.
 
Sisi watanzania tumebarikiwa unafiki yaani kikwete awe Bora Zaid ya jpm? Huyu huyu kikwete chini ya utawala wake tumeshuudia twiga anapanda ndege,safari za nje Sana,vyeti feki makazini wengi,hajawahi hata kukemea ufisadi,usimamiz mbovu,anasign mkataba wa madini tz inapata 3% the rest anapata company ya nje,mradi wa gesi unauzwa,mgawo wa umeme mkubwa n.k
 
Kikwete alikuwa bora zaidi kwenye social issues, sherehe, Musiba, burudani na safari za nje.
Kulikuwa na ubadhirifu makubwa sana kipindi cha mtawala wake, alihalalisha matumizi mabaya ya fedha za umma
Bujibuji/ujiuji
 
Nchi hii imebahatika kuwa na Marais wawili tu
Mwalimu Nyerere na Benjamin Mkapa
Hizi takataka zingine hovyo kabisa.

Mkuu huo ni mtazamo wako.

Wako wanayemuona JPM is the best.
Wapo wanayemuona JK was the best.
Wapo wanayemuona Nyerere ndio bora na hajawahi kutokea.
Wapo wanayemuona Mwinyi alikuwa ni bora pia.

Hii nchi imepitia vipindi vingi tofauti tofauti toka uhuru, na Marais wote watano kila mmoja amekutana na kipindi chake ambacho kitamlazimisha kutenda kulingana na wakati aliopo..

JK NYERERE, alitawala nchi ikiwa imetoka kwa mkoloni na haikuwa na chochote kama msingi wa maisha wa Watanzania kifupi ilikuwa kipindi cha kuanzisha Taifa. Kwa wakati huo ilimpasa Nyerere atenda ambavyo azingeweza kutenda wakati huu, Unafikiri JPM angetawala wakati ule angaejenga SGR na flyover? kila kitu huenda kulingana na mahitaji. KAZI KUBWA YA NYERERE ILIKUWA KUJENGA MISINGI NA KUWEKA NJIA ITAKAYOTUMIKA KAMA PILOT..
 
Kikwete alikuwa bora zaidi kwenye social issues, sherehe, Musiba, burudani na safari za nje.
Kulikuwa na ubadhirifu makubwa sana kipindi cha mtawala wake, alihalalisha matumizi mabaya ya fedha za umma
Wizi au matumizi mabaya ya fedha za umma ni zaidi awamu hii. Tofauti na awamu ya Kikwete, wanufaika sasa ni wachache sana kuna ka inner circle fulani. Wakati wa Jakaya walikuwa wengi sana toka messanger hadi top most.
Kwenye nganda ni hivyo hivyo. Wengi wameondolewa Kwenye biashara. Wamebaki wachache wenye connection na Bashite. Lakini biashara iko pale pale.
 
Nyie ndio mliyekua mkisema Kikwete ni Rais dhaifu haijawai tokea. Ata mlisahau uo uhuru wakuongea mliokuanao, mlivuka mipaka ya Matusi na dharau. Nchi ilifunga na kuomba kumpata JPM.ila kwasasa mmekuja na swaga zingine.
Dhambi iliyoje kumwabudu na kumsujudia mwanadamu mwenzako huku ukimuacha Mungu peke yake! Hakuna dhambi iizidiyo unafiki kwa Mola. Na itakutafuneni kabla ya umauti wenu ili mmrejee Munga wa kweli!
 
Wewe ni boya mmoja tu, eti nchi ilifunga ili kumpata JPM baada ya kumpata kafanyaje?
Unadhani Mungu anasikia maombi ya watu wapumbavu?
Ukivuta taswira ya Mungu alivyo, Unadhani Mungu anavaa suti?
Mungu hawezi kuweka kiongozi Dikteta, muuaji, katili Kama JPM wako, viongozi wanaowekwa na Mungu ni viongozi wenye hekima, Hitler, Saddam, Mobutu ,Idd Amin na JPM wako ni zao la Ibilisi
Alimuua nani?
Au ndoto za mchana!
 
Kwanini nasema hivyo.

Nyerere kwangu anabebwa suala moja tu la kujenga taifa na kuimarisha utaifa ambalo wafuasi wake walikuta taifa tulivu hivyo jukumu la kuleta maendeleo ilikuwa rahisi zaidi kwao kutokana na misingi ya maendeleo kuwepo.

Mkapa kwangu pia anabebwa na hoja ya kujitahidi sana kuimarisha misingi ya ukuaji wa uchumi ambao rais Kikwete alinufaika nao sana.kama rais Kikwete angedhibiti ufisadi kwangu mimi angekuwa bora baada ya Nyerere.

Kwanini Nimewatoa Kikwete Mwinyi na Magufuli ?

Mzee Mwinyi kuna sehemu alijitahidi hasa kutokana na hali alivyoikuta nchi kosa kubwa la utawala wa mzee Mwinyi ni kushindwa kujenga misingi ya utawala bora katika ideolojia mpya ya uchumi yaani ubepari, lakini utawala wa.mzee mwinyi ulisimika rasmi misingi ya rushwa na ufisadi.

Mzee kikwete mapungufu yake makubwa ni kushindwa kudhibiti rushwa na ufisadi lakini utawala wake ulishiriki kuulinda na kuupalilia ufisadi, wakati wake ufisadi uligeuka kuwa mfumo rasmi wa maisha ya wanasiasa na kila mwanasiasa aligeuza siasa kama chanzo cha utajiri.

Mzee Magufuli yawezekana kuna sehemu he is doing good lakini mapungufu yake kiuongozi ni mengi kuliko mazuri, nachokiona Magufuli anacho ni uthubutu na utashi lakini hana weledi.

Magufuli hajui nini maana ya maendeleo ndiyo maana toka ameingia madarakani nchi imeparaganyika kiuchumi na hakuonekani dalili zozote za kusonga mbele.

Magufuli anachembechembe za udikteta na ubaguzi, roho ya visasi na ukosefu wa busara, kwangu mimi kiuongozi nampa Mark's 1/5
Mkuu huo ni mtazamo wako.

Wako wanayemuona JPM is the best.
Wapo wanayemuona JK was the best.
Wapo wanayemuona Nyerere ndio bora na hajawahi kutokea.
Wapo wanayemuona Mwinyi alikuwa ni bora pia.

Hii nchi imepitia vipindi vingi tofauti tofauti toka uhuru, na Marais wote watano kila mmoja amekutana na kipindi chake ambacho kitamlazimisha kutenda kulingana na wakati aliopo..

JK NYERERE, alitawala nchi ikiwa imetoka kwa mkoloni na haikuwa na chochote kama msingi wa maisha wa Watanzania kifupi ilikuwa kipindi cha kuanzisha Taifa. Kwa wakati huo ilimpasa Nyerere atenda ambavyo azingeweza kutenda wakati huu, Unafikiri JPM angetawala wakati ule angaejenga SGR na flyover? kila kitu huenda kulingana na mahitaji. KAZI KUBWA YA NYERERE ILIKUWA KUJENGA MISINGI NA KUWEKA NJIA ITAKAYOTUMIKA KAMA PILOT..
 
Alikuwa bora ya design ya watu kama kama ulikuwa miongoni mwa wapiga deal....this country needed a man of a moment ambaye ni JPM...muda wake kwishine
 
Wewe ni mjinga! Rais anataka badala ya hela nyingi hivyo kwenda kwenye pango badala yake wajenge majengo yao au wapange kwenye majengo ya selikali ili hizo hela ziende zikafanye mambo mengine ya kiselikali.
Hii ndiyo serikali iloyouza nyumba zake bei chee kabisa.

Hawa watu wanajua wanakwenda ama wanarudi?
 
Magu angeacha tu kutoshaurika na haya mambo kutetereka kwa usalama wa raia.Nadhan angetufaa sana.But ndio hvyo shubiri imeshazidi tamu.
 
Kikwete alikuwa bora zaidi kwenye social issues, sherehe, Musiba, burudani na safari za nje.
Kulikuwa na ubadhirifu makubwa sana kipindi cha mtawala wake, alihalalisha matumizi mabaya ya fedha za umma
Kama walishindwa kutoa maelezo ya kueleweka kweny 1.5 Trillion .......

Kwa jinsi walivyomkomalia CAG na kubana report yake pamoja na kumpunguzia bajeti ........

Hizo pesa akina Bashite wanazogawa mpaka 100 million wanazitoa wapi.............?

Hizo pesa zinazogawiwa kama pipi kwenye ziara zinatoka wapi ...........................?

Hivi kweli bado unauhakika pesa yetu ipo salama ............!!? Kwa sasa ni vigumu kujua kutokana na usiri wa awamu hii. Ila wakiondoka siri zitavuja na kujua ukweli.
 
Mkuu, kumbuka yeye akiwa Waziri wa ujenzi aliuza nyumba za serikali ikalazimisha Serikali ya JK awamu yake ya Kwanza viongozi waandamizi waishi mahotelini
Wewe ni mjinga! Rais anataka badala ya hela nyingi hivyo kwenda kwenye pango badala yake wajenge majengo yao au wapange kwenye majengo ya selikali ili hizo hela ziende zikafanye mambo mengine ya kiselikali.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom