Pamoja na mapungufu yake kwa ujumla, Mzee Kikwete alikuwa bora kuliko Rais Magufuli

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Enzi za JK
-Hakuwahi kupiga ufisadi wa trilioni 2.4 hata kama ungeunganisha EPA, ESCROW na RICHMOND

-Hakuna mfanyabiashara aliyehamisha biashara kama hivi sasa.

-Watumishi wa umma waliongezewa mishahara na kupandishwa vyeo kila mwaka tofauti na ilivyo leo. Wakat anawaaga Mei Mosi 2015, aliwaambia atawaacha vizuri. Na kweli July aliwaongezea mshahara ambao ndo wanatembela hadi leo.

-Wakulima wa korosho hawakuwahi kudhulumiwa na serikali.

-Ajira za moja kwa moja kila mwaka wala si za kuomba kama leo.

-Deni la taifa halikupaa kwa spid ya bombadia.

-Bei za bidhaa mtaani zilikuwa chini tofauti na hii leo.

-Hotuba za kila mwisho wa mwezi zilileta matumaini.

-Wapinzani walifanya mikutano na maandamano bila kizuizi.

Yapo mengi, ni bora angerudi awamu hii hata kwa miaka miwili tu!
Screenshot_20190106-114210.png

Hadi watoto walimpenda
 
Hilo halina ubishi, kuwa Kikwete alikuwa bora zaidi kuliko huyu Magufuli

Kigezo pekee cha kumfanya kiongozi kuwa bora ni namna anavyoruhusu Uhuru wa kutoa maoni na kuruhusu vyama vya kisiasa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba

Huyu tuliye naye hivi sasa haruhusu Uhuru wa mawazo na vyama vya kisiasa vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa kwa mujibu wa Katiba ya nchi

Kwa maana hiyo ni lazima yeye aonekane mbovu, kwa kuwa anaisigina Katiba na kuruhusu wateule wake wajimwambafai kwa hiyo waishi wakiwa na "impunity"

Refer kesi za akina Paul Makonda, Albert Chalamila, Ole Sabaya, Mrisho Gambo na Alli Hapi
 
Nyie ndio mliyekua mkisema Kikwete ni Rais dhaifu haijawai tokea. Ata mlisahau uo uhuru wakuongea mliokuanao, mlivuka mipaka ya Matusi na dharau. Nchi ilifunga na kuomba kumpata JPM.ila kwasasa mmekuja na swaga zingine.
 
Sikuwahi kusikia JK akiagiza serikali isipange nyumba sector binafsi, hili agizo la juzi ndani ya mwezi wahame!? Sijui hizo nyumba ni za Wageni ama Watanzania. Mbali ya ofisi watumishi wangapi wanapanga makazi binafsi!? Kwanini chuki na sector binafsi!? Hata kandarasi za ndani , wajenzi mbali ya bei elekezi miradi bado hawalipwi kwa wakati.Hii roho mbaya inadumaza taifa,ile dhana ya "multiplier effect " nadhani amekariri msemo pekee.
 
Wewe ni mjinga! Rais anataka badala ya hela nyingi hivyo kwenda kwenye pango badala yake wajenge majengo yao au wapange kwenye majengo ya selikali ili hizo hela ziende zikafanye mambo mengine ya kiselikali.
 
Wewe ndiyo mjinga, usibishane kitu ambacho hukijui. Serikali makini haipaswi kufanya biashara, ila inakuwa kuweka mazingira bora na kusimamia biashara. Serikali inapifanya biashara inasimamisha Mzunguko wa fedha hauwahusishi wananchi. Jeshi linapojenga nyumba za Magereza linapunguza Mzunguko wa hela.
 
Wakati Kukwete akisemwa wapo waliomtetea sana. Ila Magufuli alipoingia walimgeuka na na kumsema na wanamtetea sana huyu wa sasa kama kawida yao watamgeuka akiondoka. Na huu ni unafiki pia.
Wawili hawa wana sifa tofauti na mapungufu ni tofauti pia. Pia wanasemwa kwa namna tofauti.
Nyie ndio mliyekua mkisema Kikwete ni Rais dhaifu haijawai tokea. Ata mlisahau uo uhuru wakuongea mliokuanao, mlivuka mipaka ya Matusi na dharau. Nchi ilifunga na kuomba kumpata JPM.ila kwasasa mmekuja na swaga zingine.
 
Watu binafsi wakifanya biashara watalipa kodi. Serikali ni mteja mzuri wa kuhamasisha biashara katika sekta binafsi. Chukua mfano wa hoteli.
Wewe ni mjinga! Rais anataka badala ya hela nyingi hivyo kwenda kwenye pango badala yake wajenge majengo yao au wapange kwenye majengo ya selikali ili hizo hela ziende zikafanye mambo mengine ya kiselikali.
 
Kikwete alikuwa bora zaidi kwenye social issues, sherehe, Musiba, burudani na safari za nje.
Kulikuwa na ubadhirifu makubwa sana kipindi cha mtawala wake, alihalalisha matumizi mabaya ya fedha za umma
Kaka Bujibuji unamaanisha kwamba kipindi hiki cha magufuli hakuna matumizi mabaya ya fedha za umma
 
Sikuwahi kusikia JK akiagiza serikali isipange nyumba sector binafsi, hili agizo la juzi ndani ya mwezi wahame!? Sijui hizo nyumba ni za Wageni ama Watanzania. Mbali ya ofisi watumishi wangapi wanapanga makazi binafsi!? Kwanini chuki na sector binafsi!? Hata kandarasi za ndani , wajenzi mbali ya bei elekezi miradi bado hawalipwi kwa wakati.Hii roho mbaya inadumaza taifa,ile dhana ya "multiplier effect " nadhani amekariri msemo pekee.
Wa sasa ni coward. Anaogopa upinzani kama tetekuwanga!!
 
Nyie ndio mliyekua mkisema Kikwete ni Rais dhaifu haijawai tokea. Ata mlisahau uo uhuru wakuongea mliokuanao, mlivuka mipaka ya Matusi na dharau. Nchi ilifunga na kuomba kumpata JPM.ila kwasasa mmekuja na swaga zingine.
Watanzania sifa moja wapo kubwa tunayo ni unafiki mkuu.

Kwaiyo mleta uzi atudhihirishia bayana
 
Nyie ndio mliyekua mkisema Kikwete ni Rais dhaifu haijawai tokea. Ata mlisahau uo uhuru wakuongea mliokuanao, mlivuka mipaka ya Matusi na dharau. Nchi ilifunga na kuomba kumpata JPM.ila kwasasa mmekuja na swaga zingine.
Wewe ni boya mmoja tu, eti nchi ilifunga ili kumpata JPM baada ya kumpata kafanyaje?
Unadhani Mungu anasikia maombi ya watu wapumbavu?
Ukivuta taswira ya Mungu alivyo, Unadhani Mungu anavaa suti?
Mungu hawezi kuweka kiongozi Dikteta, muuaji, katili Kama JPM wako, viongozi wanaowekwa na Mungu ni viongozi wenye hekima, Hitler, Saddam, Mobutu ,Idd Amin na JPM wako ni zao la Ibilisi
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom