Mmexico
JF-Expert Member
- Nov 1, 2016
- 369
- 328
SIASA ZA UPINZANI zilipokelewa vizuri sana kwa kiasi ambacho hakikutegemewa na watawala wetu kuanzia mwanzoni mwa miaka 90 tulipoanzisha Vyama vingi. Kwa kuangalia tu muamko wa watu hasa hasa vijana wengi na wasomi kwenye uchaguzi wa 1995 (wachache tulioshiriki) ilionyesha dhahili kiu ya waTanzania kutaka mabadiriko kote Bara na Visiwani.
Hili liliwachanganya sana CCM na waasisi wake na ilikuwa ishara nzuri kwa upinzani, ikionyesha dhahili saa ya Ushindi imekaribia. Kwa ujanja wao wakatumia nguvu kubwa na kupenyeza vibaraka walioweza kuhakikisha upinzani hauungani na kuuvunja vunja zaidi.
Siasa za kweli ziliibuka tena 2005 -2010, Upinzani ulibahatisha kuwa na watu makini wenye kujenga hoja nzito na ikaweza kweli kuibua vugu vugu jipya la kutaka Tanzania iliyo chini ya Chama mbadala. Kuacha kule zanzibar ambako CCM wamezoea kuiba kura, inasemekana hata huku bara Upinzani ulishinda au ulikaribia sana kushinda, na hivyo kufanya matokeo yapikwe.
2015 ulikuwa mwaka wao hasa Upinzani kuchukua nchi kimahesabu sababu CCM walishavulugana, Lowassa alikuwa hawezi kubaki kule na destination yake kubwa ilikuwa kujiunga na zitto kabla ya UKAWA kufanya maamuzi ya hovyo kwa kijupendekeza kwa EL, Hivyo kujitoa kafala mambo yote walikuwa wakiyapigania,wakiamini,wameyajenga wakiamini EL atawavusha salama.
Hapa ndipo wengine waliposhuka na kuacha kabisa kuamini siasa za upinzani, viongozi makini walipokatishwa tamaa na siasa za upinzani nchi hii, Kuingizwa kwa mamluki kwenye vyama vya upinzani, Kuiuzia CCM ajenda zilizoijenga Upinzani hivyo CCM kuwa kama chama cha upinzani kwenye mikutano yao ya kampeni 2015 (Bahati nzuri CCM wamebadirika na kufanya masahihisho ya kutosha kwenye namna ya kuongoza nchi na chama chao hivyo kupata wafuasi wapya)
SASA HALI IKOJE,
*Ni kweli waTanzania wengi wanatamani mabadiriko kwenye siasa zao na katiba yao
*Wengi wamechoka kuiona CCM mabadarakani, na kutaka mbadala.
*Pamoja na kwamba huo ni mtaji mkubwa sana kwa upinzani nchi hii, Upinzani bado haujitambui, haujijui, umetawaliwa na njaa na wamelala hivyo kuwapa CCM nafasi ya kujirekebisha na kubaki kama chama bora
*Wengi wetu tunajikuta tunashindwa kuunga mkono harakati za upinzani, sababu bado tunakiona chama cha mapinduzi kama chama cha watu wanaojielewa kuliko wengi upinzani.
*Ni wapinzani wachache tu wameweza kuaminiwa na kufanya mambo safi kama ilivyotegemewa pale Chama mbadala kinapo pewa nafasi ya kuongoza, Tumeona jiji la Dar wameishia kutuongezea parking fees tu na kodi za ajabu ajabu na kugombana wao kwa wao kila siku, barabara hazijengwi na huduma zinazid kuwa mbaya. Wabunge wetu wengi wao kama kina Msigwa, Sugu ni aibu hakuna alama wanaacha kwa wananchi wao walio wachagua. Hili linatufanya tuendelee kuwaamini kina PolePole na Chama Chake maana angalau wanafanya mambo yanayoeleweka. Pongezi ziwafikie kina Heche,Lema,Zitto na Prof J wamebaki kuwa mabalozi wazuri.
*Upinzani na Viongozi wao hawaaminiki, Hivyo Raia tuonaona ni bora tuendelee kuiamini CCM ya awamu hii, kuliko lundo la wapinzani wanao endeshwa kwa tamaa zao binafsi za madaraka na pesa, Zaidi ya Nusu ya Viongozi tuliowachagua upinzani 2015 inasemekana wamenunulika, na wachache waliobaki ni kwamba CCM wamewaona si tishio. Kwanini niendelee kuamini Upinzani nchi hii? Wakipewa mamlaka ya kusaini mikataba ya gesi si ndo wataishia kutuuza na sisi?
Ni Bora kukomalia maisha yako, Upinzani nchi hii hauko tayar kuongoza nchi.
Asajile Jr