Pamoja na Madaktari kufanya kazi wa-Tanzania wanakufa sana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na Madaktari kufanya kazi wa-Tanzania wanakufa sana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kalaghesye, Jun 28, 2012.

 1. kalaghesye

  kalaghesye Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hata nikibaki peke yangu .... ninaunga mkono madai ya madaktari kuhusu kuboresha huduma mahospitalini. Wengi wetu tunalalamika pasipo kujua uchungu wa kufiwa mikononi na mtu ambaye ulikuwa na uwezo wa kuokoa maisha yake endapo tu ungekuwa na kifaa ambacho thamani yake haizidi shilingi elfu moja! Say kifaa cha kuzuia bleeding!

  Pale Ocean Road watu 100 wanakufa kila siku kwa kukosa huduma za kawaida tu .... msikilizeni Dr. Ngoma wa ORCI kwenye advert ya Channel10. Mke wangu alijifungulia Muhimbili na mtoto alikuwa na matatizo ya kupumua; pale kuna mashine zisizozidi tano kwa ajili ya watoto kama hao ... hivyo inabidi Daktari awe ana-alternate hizo machine! Watoto wengi hufa kwa kukosa huduma hii!

  Taarifa za uhakika kutoka Wizara ya Afya ni kuwa kwa mwaka jana Hospitali sita kubwa nchini (Muhimbili na ORCI included) zilitengewa bajeti ya kiasi cha Tzs. 5 bilioni/- ili kutibu mamilioni ya walala hoi (ambao ni walipa kodi) lakini hapo hapo takribani Tzs. 7bilioni/- (ambazo zimezalishwa na walala hoi) zilitumika kuwatibu vigogo wa Serikali nje ya nchi!

  Ni mengi jamani .... Madaktari kila siku wanashuhudia vifo vya watu amabao wangeweza kuwaokoa endapo yale mashangingi zaidi ya 300 pale BUNGENI yangeuzwa .... posho za watu pale TRA, Benki Kuu, EWURA, SUMATRA, n.k. zingepunguzwa au kuondolewa tukaboresha huduma za afya.
   
Loading...