Pamoja na maandamano kuzuiwa na polisi, CUF kuandamana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na maandamano kuzuiwa na polisi, CUF kuandamana.

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Police, CUF spar on demonstration Monday, 27 December 2010 21:22
  Wednesday Dec 29, 2010
  [​IMG] THE demonstration that never was. A section of CUF members and supporters shout pro-new constitution slogans outside their party headquarters at Buguruni in Dar es Salaam on Tuesday before their planned demonstration was dispersed by the police. (Photo by Robert Okanda)

  By Rosemary Mirondo
  The Citizen Correspondent

  Dar es Salaam. Police in Dar es Salaam have banned a demonstration by CUF members calling for a new constitution, which was scheduled to take place today.
  The demonstration was planned to end at the ministry of Justice and Constitutional Affairs offices where they would have presented a draft copy of the said constitution to the government.

  Addressing journalists in his office, Special Zone Police Commander Suleiman Kova said that the Police Force reached the decision because the demonstration had no merit and would only create chaos.

  But in response to the ban, the CUF acting deputy secretary general, Mr Julius Itatiro, said yesterday that the demonstration would go on as planned, adding that it would begin at the CUF headquarters at Buguruni at 8am. He stated that the law provides that if one plans to hold a demonstration, one has to inform the police 48 hours prior to the event, adding that CUF wrote a letter to the Police on December 21, this year, to that effect.

  "The police want to destabilise democracy in this country and we are not prepared for that," said Mr Itatiro, wondering why it had taken the Police six days to reply to them, adding that the demonstration would be peaceful.

  Mr Kova, however, said that the two letters concerning the matter, which were addressed to his office and the ministry, contradicted each other.
  He revealed that the letter held by the Police indicated that there would be a demonstration while the minister's letter stated that a team of party (CUF) members would visit his office to discuss constitutional matters.

  According to Mr Kova, the minister was not prepared to receive the demonstrators.
  Commander Kova further said that according to the letter, the CUF members were aware that Prime Minister Mizengo Pinda had already announced that the government was working on ways of revising the Constitution.

  Being aware that the government had agreed to act on the matter, he said, meant that there was no need for a demonstration as the latter is always a last resort, something that the government or other organs were refusing to accept.
  He further stressed that the demonstration had been planned at an inconvenient period, which would only bring chaos to residents of Dar es Salaam.

  Meanwhile, Commander Kova revealed that Christmas celebrations were carried out in peace and harmony, inspite of a few incidents that occurred in Kimara, Kinondoni District, which the police were able to contain. According to Kinondoni police commander Charles Kenyella, they were able to arrest six people in connection with a murder incident that occurred during Christmas.

  He said that a group of people attacked the house of Kusileila Njau on December 25, this year, around 9.45pm, killing his wife and shot him in the left shoulder and leg.

  the chest, killing her instantly. The husband is currently admitted at the Muhimbili National Hospital.
  Meanwhile, the Police have apprehended the suspected robbers and investigations are being carried out.
  However, the Police declined to name them for fear that it could interfere with their investigations.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu bado wanafanya kazi kama enzi za mkoloni ambapo vyama vya siasa vilihitaji kibali cha polisi ili kufanya maandamano......na hawa wa kwetu miaka karibu 50 tangu tupate uhuru bado wanaendeleza ubabe huo huo pamoja na mahakama zetu kuweka wazi polisi hawana mamlaka ya kuzuia raia kukutana na kufanya maandamano.......................

  Polisi wetu hudai kuwa wana sera ya ulinzi shirikishi lakini hiyo ni soga tu.....kwa sababu kama polisi hawaheshimu Katiba na maamuzi ya mahakama zetu sasa wanamshirikisha nani katika ubabe wao kama huu wa kutotoa vibali kwa maana ya kuwahakikishia ulinzi....................

  Si kazi ya polisi kuamua kama mikutano ya vyama vya siasa ina tija au la hiyo ni kazi ya raia kwa kuamua kwenda kuhudhuria mikutano na maandamano hayo au la...............
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa ni CCM B, hiyo katiba yao wanayotaka kuiwasilisha kwa nini wasizungumze na washikaji zao CCM A kwanza? Mnyika ambaye anatoka upinzani halisi kapeleka hoja yake binafsi ofisini kwa spika, hatuhitaji katiba iliyoandikwa na kikundi kimoja isolately. Katiba mpya ya kweli ianzie kwenye karatasi jeupe la Judge Kisanga. Vinginevyo ni kutafuta umaarufu tu.
   
 4. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nchi hii inasemwa kuwa ni huru lakini SI KWELI KABISA!!! Jamani UHURU wa KWELI unahitajika!!! Huyo Kova is nothing but the PAW OF THE OPPRESSOR... JK and his dubious government!!!! For how long shall we be under oppression!!!
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana-JF, mimi ningeomba kidogo nitofautiane na baadhi yetu katika point hiyo hapo juu kwenye wino mwekundu.

  Ningewaomba kabisa tusiendelee kutumia hiyo lugha tunapoizungumzia mwenzetu CUF kama chama cha upinzani nchini. We really need each other today and tomorrow for a success together.

  I would want to believe that Prof Lipumba, Maalim Seif, Mtatiro, Mama Maghimbi na Mhe Haji Duni Haji lazima WANAYO A STRATEGIC-THINKING moja kubwa sana, sana tena sana katika kuchukua hii hatua kufanya kazi pamoja na CCM huko visiwani.

  Hiyo hali itaiwezesha CUF kupata kuifahamu VIZURI ZAIDI CCM kiutendaji na katika utendaji huko Visiwani. Fundisho hilo huenda ikaisaidi kambi zima ya upinzani kuikunja the DRUGON kiurahisi zaidi na katika muda mwafaka nchini. Hebu kumbukeni yale ya chama cha Bwana Odinga na anguko la chama cha Moi huko nchi jirani.

  Hebu imagine CUF na CHADEMA ambavyo ni nguvu maradufu Visiwani na Bara respectively, vikiamua kutafuta UNITY IN A DIVERSITY of their different political perspectives and approaches after a systematic harmonisation - picha gani unaipata hapo tangu sasa katika kila walitendalo dhidi ya MAFISADI nchini na kusimamia huko UTAIFA ZAIDI????

  Tafadhali, tutofautiane na kupongezana penye kustahili bila kubezana; CUF, TLP, NCCR-Mageuzi na CHADEMA kama kweli tuko serious na safari yetu hii ndefu.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ..... kuna vitu nakubaliana na wewe..... kuna kitu kimoja tu kinachofanya mada hii iwe valid....... swali moja tu la kizushi.... hivi Maalim Seif kama katibu mkuu wa CUF anaweza kuthubutu kuhudhuria kwenye maandamano haya akiwa na motorcade na secirity ya serikali? mkuu please........ their is proportional relation btn CUF and CCM ndio maana kuna doubt
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nani amekudanganya kuwa CUF ya Lipumba na TLP ya Mrema ni vyama vya Upinzani? Kwa jinsi wasivyoelewa suala zima la mchakato wa kutafuta Katiba mpya eti wanawasilisha tu rasimu ya katiba ambayo imetungwa na watu wachache tu ndani ya chama, badala ya kuacha jambo lenyewe lijadiliwe ili rasimu ipatikane! Na hiyo rasimu yenyewe inapelekwa "kwa maandamano ya Chama!" Huoni kwamba hakuna cha utaifa hapa ila ni kujitafutia tu cheap popularity?

  CUF pia ni CCM-B, hilo halina ubishi tangu ilipoundwa serikali ya UMOJA WA VYAMA VIWILI (sio umoja wa kitaifa kama inavyodaiwa) huko Zanzibar, tumeshaona jinsi "ndoa" yao ilivyo ya furaha na amani!
   
 8. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  BUSARA, HEKIMA & SUBRA tunavihitaji saana katika mustakabali mzima wa hatma ya nchi yetu. Kwa hapo juu...ni moja ya angalizo makini sana tunalopaswa kulitazama tena kwa visionery, Nimependa mchango wako endelevu kwa hili.
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Maandamano ya CUF yazimwa
  • Polisi yasema yatahatarisha amani

  na Waandishi wetu


  [​IMG] JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezuia maandamano ya Chama cha Wananchi (CUF), yaliyokuwa yafanyike leo kwa lengo la kuwakilisha pendekezo la Katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba. Uamuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, ambapo alisema yanaweza kuleta uvunjifu wa amani.
  Aliongeza kuwa viongozi wa CUF walimpelekea barua iliyokuwa ikionyesha nia yao hiyo lakini ile waliyoipeleka Wizara ya Sheria na Katiba haikueleza jambo hilo.
  "Viongozi wa CUF, waliniletea barua yao yenye lengo la kuandamana, lakini wakati huo huo walipeleka barua tofauti kwa Wizara ya Sheria ambayo haikueleza juu ya maandamano yao," alisema Kova.
  Alisema wamesitisha maandamano hayo kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo, kifungu cha (43) sheria ya kwanza hadi ya 6, vifungu vinavyowapa mamlaka ya kufanya hivyo mara wanapohisi uvunjifu wa amani.
  "Tumepata wasiwasi na maandamano ya CUF, kwa sababu ya utata wa barua zao, tunahisi hayatakuwa ya amani, tumeyafuta.
  "Tunaomba wananchi na wafuasi wao wasishiriki kwa sababu ni batili, watakaokaidi tutapambana nao," alisema Kova.
  Kamanda Kova alionyesha barua iliyopelekwa kwake na ile ya Wizara ya Sheria na Katiba yenye kumbukumbu namba AK/DSM/NKM/B/001/AZ/2010/105, ya Desemba 21.
  Aliongeza kuwa iliyopelekwa kwao na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatilo, yenye kumbukumbu AK/DSM/NKM/B/001/AZ/2010/104/, ilielezea juu ya lengo la kuandamana tofauti na ile iliyopelekwa wizarani.
  Alisema kuwa ile iliyopelekwa kwao ilielezea kuwa chama hicho kitafanya maandamano kuanzia Buguruni kupitia barabara ya Kawawa, Morogoro na makutano ya barabara ya Bibi Titi kuelekea barabara ya Ohio na hatimaye Wizara ya Sheria na Katiba.
  Aliongeza kuwa maandamano hayo baada ya kutoka wizarani hapo yangemalizia katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
  "Kwa kuwa hawakutoa taarifa zao kwa waziri kama watawasilisha kwa maandamano, ni dhahiri asingekuwa huru na kungekuwa na uvunjaji wa amani, tumekaaa nao zaidi ya saa moja na kufikia muafaka na wametuelewa," alisema Kova.
  Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, alisema leo watafanya maandamano yao ya amani kwa ajili ya kuwasilisha rasimu ya Katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba.
  Mtatiro, aliliambia Tanzania Daima, kuwa maandamano hayo yatafanyika leo hii licha ya Jeshi la Polisi nchini kuyazuia.
  Alisema CUF, iliandika barua kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, ambayo iliweka wazi maandamano hayo lakini wanashangazwa na Jeshi la Polisi kuyazuia maandamano yao.
  Aliongeza kuwa kamanda Kova, alimuita ofisini kwake na kumtaarifu zuio la kufanya maandamano hayo ambayo wao hawaoni kama yanaweza kuleta uvunjifu wa amani.
  Alisema licha ya zuio hilo kwa CUF, wanachama wake na wapenzi wa mabadiliko wameshajiandaa kushiriki maandamano hayo.
  "Maandamano yako palepale kuanzia saa mbili asubuhi; hilo ndilo tamko letu kwa sasa. Ni lazima Katiba mpya ipatikane na tunachopeleka kwa waziri ni draft ya Katiba hiyo," alisema Mtatiro.
  Wakati huohuo, Mwanasheraia Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amesema hakuna haja ya kuwapo kwa Katiba mpya bali iliyopo ifanyiwe marekebisho.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana muda mfupi baada ya kuapishwa Jaji Mkuu, Mohamed Othman, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, Werema alisema marekebisho ya Katiba ni ruksa kwa kuondoa baadhi ya mambo ya zamani na kuweka mambo mapya.
  Alisema mwaka 1994 yalifanyika marekebisho ya Katiba kwa kuingiza vipengele vinavyohusu haki za binadamu na kueleza kuwa mabadiliko hayo yalifanyika kutokana na matakwa ya wananchi.
  "Marekani yamefanyika marekebisho Katiba yao mara ngapi? India nayo inafanyika marekebisho ya Katiba yao mara ngapi? Nadhani zaidi ya mara 50 na Marekani wanafanya mabadiliko yao kutokana na masuala ya maana yanayojitokeza," alisema Jaji Werema.
  Aliwataka wananchi kupeleka maoni yao na si kila mmoja kuzungumza kama bata.
  "Kwa nini tulumbane? Tufanye marekebisho kwa kuwekwa mapya na kuondolewa ya zamani...kiraka sawa hata nguo si unaweka kiraka?" alihoji Jaji Werema.
  Hata hivyo, alihoji upya wa Katiba ni nini na kutoa msemo kuwa ‘ukuukuu wa kamba si upya ya ukambaa'.
  "Upya wa Katiba ni nini, unaweka kipya nini? Ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa. Nadhani hapa mmenielewa!" alisema.
  Aidha, alisema hakuna haja ya kulumbana kama itafanyiwa marekebisho au mpya na kubainisha kuwa hali hiyo itategemea na matakwa ya Watanzania.
  "Watu wana mawazo mazuri kuhusu suala hili na hata kijijini kwangu, tunaweza kutofautiana lakini si katika suala la Katiba. Suala hili tutalijadili," alisema.
  Alisema ajenda hiyo ni lazima iwe na mbebaji na kwamba anaweza kuwa mtu yeyote na chama chochote cha siasa.
  "Sisi Wakurya tunasema vita ni vita, huwezi kumlaumu aliyebeba ajenda hii, kwani mtu yeyote angeweza kuibeba hata ikiwa ni vyama vyama vya siasa, kwani Katiba ni siasa.  [​IMG]

   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Fukuto la Katiba mpya


  CUF waandamana Dar
  *Polisi wawatawanya kwa mabomu
  *wenyewe wawapiga chenga ya mwili
  *Wawasilisha rasimu yao wizarani


  Rabia Bakari na Athumani Mpochi
  MABOMU risasi na ving'ora vilitawala baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam jana polisi walipojaribu kuzima
  maandamano ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), walioandamana kupeleka rasimu ya mabadiliko ya katiba mpya, Wizara ya Katiba na Sheria.

  Kuanzia saa moja asubuhi magari ya polisi namba T 337 AKV na PT 0890 likiwemo gari la upupu yalianza kuvinjari maeneo ya TAZARA na Buruguni kudhibiti mikusanyiko ya wafuasi wa CUF waliopania kuandamana.

  Maandamano hayo yalipangwa kuanza saa mbili asubuhi, Buguruni Shell, ambapo hadi kufika saa tatu, kulikuwa hakuna dalili za watu kukusanyika lakini ilipofika saa nne asubuhi magari kutoka makao makuu ya CUF yalipita mitaani kuhamasisha maandamano na kueleza kuwa yataanza saa 4.30

  Akizungumza na gazeti hili, Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw. Julius Mtatiro alisema awali waandamanaji waliogopa kujitokeza kwa kuhofia vitisho vya polisi.Matangazo hayo yaliibua morari kwa wafuasi wa chama hicho, na kadri muda ulivyozidi kuyoyoma, idadi yao ilizidi kuongeza ofisi za makao makuu chama hicho maeneo ya Buguruni.

  Wanachama hao walijikusanya makundi huku wakiimba hawaogopi polisi wanataka katiba mpya. Ilipotimu saa 4.45, walianza kuingia barabara ya Uhuru kwa ajili ya kuanza maandamano hayo huku polisi wakitoa matangazo ya kuwasihi kuacha kuandamana, kwani wanaweza kusababisha vurugu.

  Licha ya matangazo ya polisi, lakini wafuasi hao wa CUF hawakutii amri hiyo na kuzidi kuingia barabarani wakiwa na mabango huku moja likisomeka 'Kikwete muige Karume, katiba mpya ni lazima.' Waandamanaji walitumia barabara ya Uhuru na njia za mitaani ili kutimiza azma yao ya kufika Wizara ya Sheria na Katiba.

  Polisi walilazimika kupiga risasi juu kuwatawanya huku wakifukuzana nao katika mitaa mbalimbali ya maeneo ya Ilala na kufanikiwa kuwakamata watu wanne ambao walidaiwa kuwa ni miongoni mwa waandamaji.

  Kutokana na kuzidiwa na idadi ya waandamanaji, polisi ilibidi waongeze magari na askari waliozunguka maeneo yote ambayo walihisi wafuasi wa CUF wangepita.

  Majira lilishuhudia polisi wakiwatia mbaroni baadhi ya waandamanaji, akiwemo mwanamke mmoja na mzee aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 70-75 na vijana wawili, na kuwabeba katika gari la polisi lenye namba PT 1858 na kuwafikisha katika kituo kidogo cha Karume.

  Pamoja na heka heka hizo viongozi wa CUF, walifanikiwa kufikisha rasimu ya hiyo wizarani ambapo ilipokelewa na Katibu Mkuu, Bw. Andrew Mhaiki, huku magari takribani sita ya polisi yakitanda nje ya wizara hiyo , huku mengine yakizunguka mitaa ya Kivukoni.
  Bw. Mtatiro alizungumza na waandishi wa habari na kuwafahamisha kuwa utaratibu waliokuwa wamepanga umeshakamilika, licha ya kusikitishwa na vitendo vya jeshi la polisi, vinavyokiuka haki na misingi ya haki za binadamu.

  "Nchi hii inaendeshwa kiimla, kulikuwa hakuna sababu kuzuia maandamano ya amani, ambayo msingi wake ni kusimamia demokrasia. Sisi tumeshatimiza wajibu wetu kikatiba, tunashukuru na tutaendelea kupambana kudai demokrasia bila kuogopa polisi kwa sababu polisi nao ni watu kama sisi, ni wenzetu,"alisema.

  Aliongeza kuwa rasimu hiyo ya katiba ina kurasa 88, ambapo iliandikwa kutokana na mchango wa mawazo kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa masuala ya siasa na wananchi wengine. Alisema rasimu hiyo itakuwa wazi kwa wadau wote hivi karibuni na mapambano kudai katiba mpya yataendelea.

  [​IMG]
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  CUF wawazidi ujanja polisi, waandamana
  Tuesday, 28 December 2010 21:34

  [​IMG]Wafuasi wa CUFwakiandamana Buguruni jiji la Dar es Salaam jana kuelekea ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria kuwasilisha Rasimu yao ya Katiba mpya. Picha na Michael Jamson

  Salim Said na Elias Sichalwe
  CHAMA Cha Wananchi (CUF) jana kiliwazidi ujanja polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano yao baada ya kufanikiwa kuyafanya na kuwasilisha rasimu yao sifuri ya katiba kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Polisi hao walikuwa wanazuia maandamano hayo kutekeleza agizo la Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova aliyolitoa juzi kuzuia maandamano hayo kwa kile alichoeleza kuwa ni batili.

  Katika maandamano hayo yaliyosimamisha kwa muda shughuli za kiuchumi na kijamii, wafuasi na wapenzi wa chama hicho wakiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, walifanikiwa kuingia barabarani na kuwasilisha rasimu yao ya katiba kama walivyopanga. Hata hivyo maandamano hayo yaliyoanzia Buguruni Sheli hayakuanza saa 2:00 asubuhi kama yalivyopangwa kutokana na mvutano ulioibuka baina ya waandamanaji hao na polisi wenye silaha ambao walifika ofisini hapo kuwadhibiti.

  Kabla ya kuanza maandamano hayo, polisi waliwatangazia wananchi hali ya hatari na kuwataka wajifungie majumbani mwao huku wakifyatua risasi za moto na kurusha mabomo kuwatawanya. Gazeti hili lilifika Buguruni Sheli saa 2:00 asubuhi na kukuta eneo hilo limetapakaa askari wa kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) huku wengi wakiwa wamejipanga katika maeneo mbalimbali ya barabara ya Uhuru kuwazuia waandamanaji.
  Ilipofika saa 3:30 asubuhi lilipita gari la matangazo la CUF lenye vipaza sauti na ndani yake kulikuwa na mtu aliyekuwa akitangaza kuwa maandamano yapo palepale na yataanzia Makao Makuu ya Chama, saa 4:30 asubuhi badala ya Buguruni Sheli.

  Mara baada ya tangazo hilo, wananchi walianza kukusanyika kwa wingi nje ya makao makuu ya chama hicho wakiwa na mabango mikononi na vitambaa vilivyoandikwa ujumbe mbalimbali wa kudai katiba mpya. Baada ya mabadiliko hayo ya ghafla polisi waliamua kuwafuata kwenye na kuwaonya, "Wanachama wa CUF, maandamano yenu ni batili.

  Tafadhali fuateni sheria kuwasilisha madai yenu." Kauli hiyo ya Dereva wa gari la Polisi aina ya Defenda aliyevalia sare za FFU ilirudiwa mara tatu lakini, wanachama hao hawakusikia badala yake wakaendelea na azma ya kutaka kuandamana huku wakiimba, "Chinja ua, Katiba Lazima."

  Tangazo hilo lilifuatiwa na tangazo la hali ya hatari lililotangazwa na Dereva huyo ambaye alisema "Naomba wenye magari ya kiraia mwende mbele, waandishi wa habari mwende mbele, wananchi ingieni majumbani mwenu na wafanyabiashara fungeni biashara zenu, tunataka kufanya kazi." Lakini licha ya tangazo hilo la hatari, waandamanaji waliendelea kuimba na kusogelea magari hayo ya FFU zaidi ya matano yaliyokuwa mbele yao.

  "Mara ya mwisho, narudia wananchi wa CUF maandamano yenu si halali, fuateni sheria kuwasilisha madai yenu," alisema dereva huyo ambaye jina wala nambari yake haikujukana huku wanachamahao hao wakimjibu, "Hamtufanyi lolote ninyi.

  Kama ni mabomu na maji ya kuwasha tumezoea." Baada ya hapo magari hayo ya polisi yaliyokuwa yamesheheni askari wenye silaha nzito za moto na mabomu ya kutolea machozi, yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika makutano ya barabara ya Uhuru na barabara ndogo inayoingilia Makao Makuu ya CUF eneo la Rozana.

  Baadaye waandamanaji walianza maandamano na walipofika Rozana, magari ya polisi yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika kituo cha mabasi cha Buguruni Malapa, ambako gari maalumu la kumwaga maji ya kuwasha maarufu kama deraya, lilikuwa limeegeshwa. Baada ya kuona hivyo waandamanaji walijipa moyo na kuona labda polisi wanawaogopa na hivyo kuingia moja kwa moja katika barabara kuu ya Uhuru kuelekea mjini.

  Lakini, walipofika Malapa, walikumbana na kizuizi cha magari ya polisi zaidi ya sita ya FFU na deraya nyingine. Hapo ilikuwa kama mchezo wa kuigiza baina ya FFU na waandamanaji, baada ya kila upande kumtunishia msuli mwingine. Wakati polisi wakiwataka wanachama hao wasalimu amri na kusitisha maandamano yao, wanachama hao wanajibu "Kuandamana ni haki yetu kikatiba."

  Wakiwa wanatunishiana misuli katika kituo cha mabasi cha Malapa, gari moja la FFU lilikaa katikati ya barabara na dereva wake alitangaza tena "Tafadhali hili gari usilipite, ukilipita hili gari unatafuta shari." Lakini pamoja na tangazo hilo, wanachama hao waliendelea kulipita gari hilo na mkuu wa operesheni ya polisi hao akaruhusu gari la maji ya kuwasha kuanza kuwarushia maji.

  Wakati hayo yakiendelea, daladala na magari yote yanayotoka na kwenda Buguruni yalikuwa yamezuia kupita na kupaki pembeni ama kwa amri au kwa hofu yao wenyewe. Baada ya kuona kizuizi hicho waandamanaji hao waliamua kuingia mitaani na kwenda kuibukia katika mitaa ya Amana na Ilala Boma na kuendelea na safari ya kuelekea Wizarani. Wakati huo polisi walikuwa wameachwa Malapa. Polisi hao walisituka kwamba maandamano yanaendelea wakati waandamanaji hao walipokuwa tayari wamefika eneo la Karume na Mchikichini.

  Maandamano yalipofika kati ya mitaa ya Ilala Boma na Karume, polisi hao ambao walikuwa tayari wameshajawa na hasira kwa mchezo wa sinema waliokuwa wakichezewa na waandamanaji, waliamua kufyatua risasi za moto kuwatawanya. Pia mabomu kadhaa ya kutoa machozi yalilipuliwa katika mitaa hiyo jambo ambalo lilisababisha waandamanaji hao kuanza kupoteza mwelekeo huku baadhi ya viongozi wao, wakifanikiwa kupita kwa gari la chama lenye bendera.

  Baadaye maandamano hayo yalifanikiwa kufika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria ambako viongozi wa CUF walikabidhi rasimu yao ya katiba. Akizungumza baada ya kukabidhi rasimu hiyo, kiongozi wa maandamano hayo Julius Mtatiro alisema maandamano yalikuwa halali na kwamba licha ya kupigwa mabomu na kutishwa kwa risasi za moto, wamefanmikiwa kufikisha ujumbe kwa serikali na wadau wote wa katiba.

  "Tumefanikiwa kufikisha ujumbe wetu ingawa maandamano yetu yalikatiswa na polisi hali ambayo inaonyesha wazi ubakaji wa demokrasia nchini kwani maandamano ni haki ya kikatiba ya kila raia," alisema Mtatiro. "Tumekabidhi rasimu yetu sifuri ya katiba wizarani, ingawa waziri hatukumkuta lakini tunashukuru imepokewa na katibu mkuu wa wizara hiyo," aliongeza Mtatiro. Hata hivyo katika makabidhiano ya rasimu hiyo, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi na kushuhudia.

  Mwisho Juzi Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Al-hajji Suleiman Kova aliwaeleza wanahabari kuwa maandamano hayo ya Chama Cha Wananchi (CUF), ameyazuia na kwamba ni batili, huku kwa upandeo wao CUF kupitia Mtatiro wakisisitiza kutimiza azma ya kuandamana hadi kwa Waziri Kombani na kumkabidhi rasimu hiyo.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Wednesday December 29, 2010 Local News

  Police disperse CUF demo, Mtatiro presents draft constitution

  By Christopher Majaliwa, 28th December 2010 @ 23:24, Total Comments: 2, Hits: 566

  More than four people have been arrested, and about seven shots fired on air in police efforts to suppress demonstration by the Civic United Front (CUF) members and followers held on Tuesday mid-morning.

  This follows a "no" response from Special Zone Police Commander Suleiman Kova on demonstration which was planned to take place on Tuesday from CUF headquarters in Buguruni, Dar es Salaam to the ministry of Justice and Constitutional Affairs calling for new constitution.

  The CUF members begun gathering at the CUF offices in the morning and it was around 10.30 am when they started marching to the ministry's offices located at the city center, police ordering them to disperse.

  "All CUF members note that these strikes are illegal and therefore you should all separate and leave the place soon," police ordered in a loud speaker.

  Singing 'kama noma na iwe noma, sikubali narevengi mimi' meaning they are ready for anything, the demonstrators marched on, after the party's Acting Deputy Secretary General's car passed police barrier without being stopped.

  Police warned people and traders around the busy area to move away for their safety, giving way for the police to start using force, by firing gunshots on air, which dispersed the demonstrators.

  The disturbance resulted into closure of shops and bringing to a halt of all business activities from Buguruni to nearby Ilala suburbs. Daily News observed four people, including a woman, put under police custody at the Karume police station.

  Mtatiro presents new constitution proposal to the Ministry

  However CUF Acting Deputy Secretary General, Mr Julius Mtatiro, accompanied with some officials managed to present the new constitution's proposal to the Ministry of Justice and Constitutional Affairs' permanent Secretary, Mr Oliver Mhaiki.

  The new constitution proposal presented has 36 articles and more than 130 sections in 88 pages.

  "We need amendment of the constitution as the current one is not good in exercising full democracy and it also gives the president vast powers, we also plan to declare it to the public," said Mr Mtatiro adding that it took CUF more than four years for its preparation.

  One of the officials who preferred anonymity said the party's intent has succeeded, "the government got the message," adding that the party will immediately bail out the arrested members.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Wednesday December 29, 2010 Local News

  Police disperse CUF demo, Mtatiro presents draft constitution

  By Christopher Majaliwa, 28th December 2010 @ 23:24, Total Comments: 2, Hits: 566

  More than four people have been arrested, and about seven shots fired on air in police efforts to suppress demonstration by the Civic United Front (CUF) members and followers held on Tuesday mid-morning.

  This follows a “no” response from Special Zone Police Commander Suleiman Kova on demonstration which was planned to take place on Tuesday from CUF headquarters in Buguruni, Dar es Salaam to the ministry of Justice and Constitutional Affairs calling for new constitution.

  The CUF members begun gathering at the CUF offices in the morning and it was around 10.30 am when they started marching to the ministry's offices located at the city center, police ordering them to disperse.

  “All CUF members note that these strikes are illegal and therefore you should all separate and leave the place soon,” police ordered in a loud speaker.

  Singing 'kama noma na iwe noma, sikubali narevengi mimi' meaning they are ready for anything, the demonstrators marched on, after the party's Acting Deputy Secretary General's car passed police barrier without being stopped.

  Police warned people and traders around the busy area to move away for their safety, giving way for the police to start using force, by firing gunshots on air, which dispersed the demonstrators.

  The disturbance resulted into closure of shops and bringing to a halt of all business activities from Buguruni to nearby Ilala suburbs. Daily News observed four people, including a woman, put under police custody at the Karume police station.

  Mtatiro presents new constitution proposal to the Ministry

  However CUF Acting Deputy Secretary General, Mr Julius Mtatiro, accompanied with some officials managed to present the new constitution’s proposal to the Ministry of Justice and Constitutional Affairs’ permanent Secretary, Mr Oliver Mhaiki.

  The new constitution proposal presented has 36 articles and more than 130 sections in 88 pages.

  “We need amendment of the constitution as the current one is not good in exercising full democracy and it also gives the president vast powers, we also plan to declare it to the public,” said Mr Mtatiro adding that it took CUF more than four years for its preparation.

  One of the officials who preferred anonymity said the party's intent has succeeded, "the government got the message," adding that the party will immediately bail out the arrested members.
   
Loading...