Pamoja na kuzungukwa na mameneja wengi bado Zuchu analalamika kutapeliwa na makampuni? Mameneja wake wanamzunguka?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
51,960
41,432
Msaniii Zuchu ameyalalamikiaMakampuni Ambayo ameyatuhumu kuwadharau Wanawake/ Wasanii Wa Kike Hasa Kwenye Upande Wa Malipo kwani anasema wao wamekuwa wakipewa hela ndogo

Ikumbukwe kwamba ni mwezi umepita watanzania walitangaziwa Zuchu ameingia mkataba mnono wa kulipwa hela nyingi sana na mtandao wa simu wa Zantel lakini kwa maandishi haya ni wazi yaliyokuwa yanasemwa Zuchu kulipwa hela nyingi ni uongo mtupu au pengine hela hizo hazijamfikia kabisa.

Maswali ya kujiuliza
Zuchu amezulumiwa vipi ikiwa ana mameneja wanao tajwa ni bora sana hapa Tanzania?
Zuchu aliposaini huo mkataba hakujua kuwa hela ni ndogo?
Zuchu ana uhakika gani kama mziki wake uan thamani mbele ya hao makampuni na wanaona itawalipa?
Mameneja wake walikuwa wapi hadi zuchu ana tapeliwa?

Zuchu Amesema haya na nukuu..

"Nasikitishwa Sana Na Baadhi Ya Watu/ Kampuni Ambao Tunafanya Nao Kazi, Ifike Muda Msanii Aheshimiwe Kwa Status Na Platfom Yake Inayotumika Kutangazia Kitu Fulani.

Hii Sio Favor Wala Sio Msaada, Tunafanya Kazi Kwa Makubaliano Basi Ifike Hatua Mjifunze Kuheshimu Wasanii...

Na Kinachonikera Zaidi Ni Kwamba Wanajua Umefanya Kazi Kubwa Ya Kushikilia Bango Kwa Kiasi Kikubwa Kuchangia Ushawishi Kwenye Matumizi Ya Kampuni Zao.

Watu Wengi/ MAKAMPUNI Mnadharau Sana Wanawake Kwenye Upande Wa Malipo, Respect A Woman Who Has Worked To Build Her Career/ Platform - Zuchu
 
Amefanya maamuzi ya kitoto sana hata kama Kuna ukweli juu ya swala hili ilibidi atumie busara kwenye kulisolve sio kwenda kwenye social media

Makampuni mengi yataanza kumuogopa kutokana na huo Uswahili aliofanya.

Inabidi elimu ianze kutolewa kwa hawa vijana wanaopata umaarufu wa haraka jinsi ya kulinda reputation yao na kupiga hela
 
Mbona kama unashindwa kuelewa ulichonukuu mwenyewe?!

Mwenyewe unadai amesema:-
Hii Sio Favor Wala Sio Msaada, Tunafanya Kazi Kwa Makubaliano Basi Ifike Hatua Mjifunze Kuheshimu Wasanii...
Sasa hivi hapo unahitaji kuwa na shahada kufahamu kwamba kinacholalamikiwa ni ukiukwaji wa makubaliano?!

Na suala la ukiukwaji wa makubaliano unaona ni jambo geni kwa Wabongo?

Btw, mbona sijaona popote kutoka uliposema "nanukuu" panapoonesha "hao jamaa wamemlipa pesa ndogo"?

Mbona sijaona popote kutoka inapoonesha anawalalamikia Zantel unaodai mameneja wake walitamba "alilipwa pesa nyingi kumbe ni uongo mtupu?"

Unaonaje basi ukituwekea SCREENSHOT ya hicho alichoandika, na kama ni audio/video, unaonaje basi ukiweka source/link ili tuone wenyewe?!
 
Sio wanawake tu, wasanii wengi hususani bongo fleva wana vinyongo moyoni

ila kwasababu walisha tengeneza image mitaani kuwa aminisha raia kuwa wao maisha yao ni ya ghali wamejikuta wanashindwa kudai hadharani haki zao


Kwasababu hao mameneja wanaweza wakaanika kiwango ambacho kinadaiwa na huyo msanii alafu katika macho ya raia kikamshushia credibility kuonesha jamaa sio wa hadhi ile aliyotuaminisha

Wasanii wanaishia kutabasamu usoni huku hasira wakiikumbata moyoni, hapo zuchu kaamua kuwa wakilisha tu
 
Ukiwaamini hao wasanii utapotea tu hao wasanii ni wazee wa kuongeza sifuri kuna msanii mmoja nyumba aliyopanga ghalama yake ni laki mbili na nusu lakini kwenye mtandao anawambia wenzie analipa milioni tena kodi yenyewe Unga Unga mwana lakini anajitapa analipa kodi ya mwaka hawa sio wa kuwamini kabisa
 
Amefanya maamuzi ya kitoto sana hata kama Kuna ukweli juu ya swala hili ilibidi atumie busara kwenye kulisolve sio kwenda kwenye social media

Makampuni mengi yataanza kumuogopa kutokana na huo Uswahili aliofanya.

Inabidi elimu ianze kutolewa kwa hawa vijana wanaopata umaarufu wa haraka jinsi ya kulinda reputation yao na kupiga hela
Basi ni wazi kabisa walikuwa wanadanganya kusema mkataba wake na zantel alilipwa mapesa mengi
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom