Pamoja na kuwakosea Watanzania, msamaha wa CCM ni kuruhusu Uchaguzi Huru

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Kwa hulka yao ya ubishi na kiburi wanaweza kudharau maono haya nisemayo, lakini msamaha mkubwa wa dhambi nyingi walizo watendea Watanzania na hasa viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani ni kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu 2020 unakuwa huru na haki huku ukisimamiwa na chombo makini chenye kuhushimu raia.

Kwa uchaguzi huru, hata kama CCM itashinda itaheshimiwa na maisha yatasonga mbele bila kikwazo chochote kile.
Lakini kujifanya ujuaji, umwamba na ubabaishaji hasira za wananchi zitazidi na sio ajabu mambo ambayo hayajawahi kufikiriwa yakatokea.

Wenzetu yaliyowakumba walijifikiria wajanja lakini waliishia kupoteza maisha, kupata vilema, ukimbizi na maisha duni yasiyo amani.

malisa_gj___CAAflDfgAMe___.jpg


 
Mkuu Mbona tuna tume huru ya Uchaguzi

Hii tume ndio imekuwa ikiwatangaza kina Mbowe kushinda ubunge toka 1995 je tunataka tume gani?

Au Chadema tunatafuta mtu wa kumlaumu kutokana na chama kufa ?
 
Back
Top Bottom