Pamoja na kukubali katiba mpya Kikwete ni bata-Warema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na kukubali katiba mpya Kikwete ni bata-Warema

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Alfu Lela Ulela, Jan 4, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pamoja na rais Kikwete kukubali sera ya katiba mpya lakini ataendelea kuwa bata kwa mujibu wa mwanasheria mkuu (AG) Fredrich Warema.

  Warema wiki jana alisema kuwa wote wanaojadili katiba mpya wanaongea tu kama bata maana hawana utaratibu.

  Lakini Warema hakufafanua kama bata ni wale wanaojadili kuipinga au kuikubali. Kwa maana hiyo wote wanaojadili katiba mpya either kwa kuipinga au kuikubali wote ni bata.

  Na ikumbukwe wakati anayasema hayo Pinda alikuwa ametoka kukutana na wahariri na wakazungumza suala la katiba mpya. Hivyo Pinda aliingia kwenye press comference akiwa Waziri mkuu lakini akatoka akiwa BATA.

  Na waziri mkuu (baada ya kuwa bata, so yawezekana alikuwa anatumia akili zake za bata) akaahidi kwenda kumshirikisha rais Kikwete suala hilo (bila kuchukua tahadhari yoyote kwa vetenary officers ya kumwepusha rais na ubata wa Warema) Hivyo walipoanza kujadili tu, rais nae akawa bata maji on spot.

  Muda si muda bata maji Kikwete akaja kujadili suala lilelie aliloonywa na Warema asijadili maana atakuwa bata. Lakini kwa kiburi cha ubata maji alichokuwa nacho JK akaamua kulijadili suala la KATIBA MPYA wakati anahutubia kufunga mwaka. Hivyo kwa kujadili suala la katiba mara mbili (wakati alishaonywa na Warema) JK amepanda cheo na kuwa BATAMZINGA.

  Hivyo kwa mujibu wa Warema, pamoja na JK kukubali suala la katiba mpya ataendelea kubaki kuwa BATAMZINGA hadi itakapotangazwa vingine.
   
Loading...