Pamoja na kujipa ushindi CCM mbona iko kwenye bumbuazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na kujipa ushindi CCM mbona iko kwenye bumbuazi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Chakaza, Nov 5, 2010.

 1. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Wote tunaifahamu CCM na tambo zake pale inapopata ushindi wowote hata uwe mdogo kiasi gani. Ni TOT, taarabu,ngoma na kejeli kwenda mbele. Sasa wamepatwa na nini hawa jamaa? maana pamoja na kujitangaza ushindi sura zao kuanzia viongozi wa juu hadi wanachama zinaonyesha kuduwaa na kama aina fulani ya aibu, lile bashasha lao la tambo limepotea kabisa.
  Jee ni kwa vile wanaijua siri ya ushindi wao? au ni hofu kuwa wapinzani safari hii hawatakubali kuburuzwa? au wanaogopa kuwa ya Kenya yanaweza kutokea na mwishowe ni wahusika kupelekwa The Hague?
   
 2. P

  Paul J Senior Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Niliishawahi kusema hapa kuwa kuna haina tatu za watu ndani ya CCM

  1. Wenye dhamira hai
  2. Wenye dhamira zinazoelekea kufa
  3. Wenye dhamira mfu

  Wachache wamefikia kwenye dhamira mfu na hao ndo unawaona kwenye vyombo vya habari wakiishabikia CCM eti imeshinda huku wakijua si kweli lakini kwa kuwa dhamira zao ni mfu hawaoni haya.

  Kwa kuwa wengi wa CCM wako kwenye kundi la 1 na 2 na wanajua nini kimefanyika mpaka wanajiita washindi, naomba uudhurie mojawapo ya sherehe zao za ushindi utangundua kuwa wengi roho zao zinasononeka maana hawasherekei ushindi wa kweli, ni suhindi wa hira na dhamira zao zinawasuta!

  Anayeiba hawezi sahau aliyemwibia hata siku moja!

  Naomba siku moja mnipe mwonekano wa watu wa ssm katika sherehe zao na hasa subiri siku ya kuapishwa rahisi utaona atakavyokuwa akiongea, uso wake utakuwa kioo cha madhambi aliyoyatenda!
   
 3. semango

  semango JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu Paul jk nahisi yuko ktk kundi la 3.nahisi kwa upeo wake hata siku ya kuapishwa atafurahi tu maana hana upeo na utu wa kuona aibu kwa mabaya yaliotendeka.
   
 4. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzimu wa madhambi yao unawaandama na utaendelea kuwaandama kwa kadri matatizo ya nchi hii yanavyoongezeka.
   
 5. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ile badget ya TOT ilihamishiwa kwenye kuwahonga wasimamizi wa uchaguzi na usalama wa taifa! PESA YOTE KUSA ISA!!
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unajua raha ya mashindano ni kushinda hata kwa kura moja utashangilia sana na kufurahia.
  Ila ukichakachua ushangilie nini ,ni kama kujifanyia mazingaombwe
   
 7. m

  mtuporimtupori Member

  #7
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanajua ushindi si wa haki. Wakishangilia ni kama wanajibeza wenyewe.
   
 8. A

  ATENGEZEKE Member

  #8
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amakweli mchuma janga hula na wakwao,naona wapinzani mnavyopeana moyo baada ya kukosa ushindi,Slaa alisha ahidi kuwa hakunakulala mpaka kieleweke ndio kimeeleweka.Poleni sana
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ushindi wa laana huo hata mwenda wazimu anajua, vipi wao wasijue
   
 10. N

  Ntemi Member

  #10
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  never say die, mwaka huu mpaka kieleweke
   
Loading...