Pamoja na kufukuzwa kwa aibu Jangwani, Nchimbi awazidi kete wahariri; akutana nao Morogoro!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wahariri, kwa maana ya Jukwaa la Wahariri sasa linatia kichefuchefu. Naamini sasa ni kweli viongozi wa jukwaa hilo ndiyo walimualika Nchimbi.

Wikiendi hii huko Morogoro Idara ya Uhamiaji (iliyo chini ya Nchimbi) imeandaa semina na wahariri kuzungumzxia mambo mbali mbali ya idara hiyo, na Nchimbi ndani!

Kuna umuhimu wa kuanzisha jukwaa lingine lililo huru, au kuwaondoa viongozi wa sasa. Siku ya kwenda kuwang'oa tunaomba polisi wasipeleke vikosi kuwalinda kama vile walivyofanya kwa mufti!
 
Njaa mbaya sana mkuuwangu....bado tunasafari ndefu kuipata tz tunayoitaka
 
Waandishi wengi njaa hata hili la Mwangosi wanalishikia bango wakitafuta namna ya kupata chochote, sio kwamba ni wazalendo sana!!!
naunga mkono hoja bila kuirekebisha wala kuitoa kasoro kama ilivyo mibunge ya CCmabwepande
 
Badala ya kukutana na polisi anakutana na wana habari? That says all about the minister - self-serving!
 
Njaa mbaya sana mkuuwangu....bado tunasafari ndefu kuipata tz tunayoitaka

siyo njaa bali ni ile hali ya taasisi ya ushushushu aka usalama wa taifa/ccm kujipenyeza kwenye kila sekta, mimi binafsi namkumbuka home boy wangu alivyokuwa mpambanaji wa nguvu kupinga ccm na uovu wake wakati tupo wanafunzi chuo kikuu, baada ya chuo jamaa alianza kupanda vyeo chap chap na hivi ninavyo andika ni mbunge wa ccm kwenye bunge la JMT. Siyo kwamba waandishi wanasalitiana, hapana, miongoni mwao wamo mashushushu wanaowajibika kwanza kwa serkali ya ccm na kuilinda kwa kila hali na hii ndo ilivyo kwa kila taasisi ndani ya JMT, there are shushushu operatives in every institution in this country. A total system clean up is the only answer to this evil!!!!!
 
Kuna umuhimu wa kuanzisha jukwaa lingine lililo huru, au kuwaondoa viongozi wa sasa. Siku ya kwenda kuwang'oa tunaomba polisi wasipeleke vikosi kuwalinda kama vile walivyofanya kwa mufti!
Ongea ya kwako hapo kwenye red nenda jukwaa la dini
 
Yani ni aibuuu...ukiangalia hata Maandamano ya Waandish wa Habari mkoa wa Morogoro,niliwangalia taarifa ya Habari Channel Ten,Mwenyekiti wao anatoa tamko kuilaani Serikali na Jeshi la Policcm huku aliposimama mgongoni kuna Picha kuubwaaa imeandikwa "CHAGUA CCM,CHAGUA KIKWETE"...Na pembeni yake picha ya Mbunge wa Moro Mjini...sasa unajiuliza bwana Aziz Msuya hakuwa na jukwaa lingine?We hav long way to go!
 
Kwani hilo jukwaa nini? Ni NGO kama NGO nyingine! Tena ni mali binafsi!waandishi wangekuwa na hekima wangeimarisha Tanzania Union of Journalism ambacho kipo kisheria na kuachana na NGOs kama UTPC na vilabu vya mikoa
 
Waandishi wa habari walisema hawataandika habari za jeshi la polisi tu. Na huko walipoitwa ni kwenye issue za uhamiaji ambapo ni idara mbili tofauti.
 
hilo ndio tatizo la tz, mamluki kila kona. sasa sikui tutafanya nini kabla ya kufanya total overhauling ya system nzima?
siyo njaa bali ni ile hali ya taasisi ya ushushushu aka usalama wa taifa/ccm kujipenyeza kwenye kila sekta, mimi binafsi namkumbuka home boy wangu alivyokuwa mpambanaji wa nguvu kupinga ccm na uovu wake wakati tupo wanafunzi chuo kikuu, baada ya chuo jamaa alianza kupanda vyeo chap chap na hivi ninavyo andika ni mbunge wa ccm kwenye bunge la JMT. Siyo kwamba waandishi wanasalitiana, hapana, miongoni mwao wamo mashushushu wanaowajibika kwanza kwa serkali ya ccm na kuilinda kwa kila hali na hii ndo ilivyo kwa kila taasisi ndani ya JMT, there are shushushu operatives in every institution in this country. A total system clean up is the only answer to this evil!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom