Pamoja na kauli zenye ukakasi, RC Albert Chalamila amefaulu kuidhibiti Mbeya na kusimamia miradi ya maendeleo vyema kuliko watangulizi wake

Habari zenu wakuu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mkoa wa Mbeya ni Kati ya mikoa yenye wakaazi wanaishi na watukutu na ujuaji mwingi. Watu wenye sifa hizi huwa ni changamoto sana kuwatawala ikizingatiwa wana elements za upinzani na kuhusu kutengwa kimaendeleo.

Kwa miaka mingi iliyopita Mkoa huu ulijaa wapigaji wa pesa za serikali na kuhukumu miradi kwa wizi.Mifano iko mingi baadhi ni kama soko la Mwanjelwa na mradi wa TSCP ambapo barabara zilijengwa chini ya Kiwango ndani ya mwaka 1 tu zilianza kufumuka na kuwekwa viraka.

Lakini toka Mh. Rais amteue ndugu Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,amejitahidi kuwadhibiti watukutu na wahudumu wa miradi ya maendeleo. Ndani ya uongozi wake miradi mingi inetekelezwa na value for money inaonekana na ndio maana mh.Rais anamuelewa sana Chalamila.

Siwezi kutaja miradi yote maana ni mingi but mlioko Mbeya bila shaka mnaona saizi barabara zinajengwa kwa viwango, mahospitali nk nk hata mradi wa ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya mkuu wa Mkoa sasa liko mbioni kukamilika baada ya kusimama kwa mda mrefu na yeye mkuu wa Mkoa kuwapiga biti moja matata wakandarasi wa jengo.

Ukiona wanaomchukia hao ni wapigaji tu ambao mirija yao imebanwa, lakini yeye kama binadamu ana mapungufu ya kawaida ila kwenye kuchapa kazi namkubali na anafaa kwenye mikoa dizaini ya Mbeya, Arusha na Dar.

Niwaeleze tu watu wa Mbeya kwamba Rais anamuamini sana huyo jamaa ndio maana miradi inamiminika vinginevyo mngekuwa na Hali mbaya. Kwanza huwa hana ego na yuko honest, open and straight, nataman ahamishiwe mkoa wa Songwe Ili awanyooshe pale Tunduma mpakani kuna wapigaji wengi.

Chalamila na Bashite ni sampuli aina moja wazee wa amsha amsha. Siku akihamishwa Mbeya mtamkumbuka kutapoa kama Dar. Mnyonge nyongeni ila haki yake mpeni.

Heko Mzee wa kuwachana live makavu, bila chenga na hupepesi macho.
Rc punguani
 
Back
Top Bottom