Pamoja na kauli zenye ukakasi, RC Albert Chalamila amefaulu kuidhibiti Mbeya na kusimamia miradi ya maendeleo vyema kuliko watangulizi wake

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Habari zenu wakuu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mkoa wa Mbeya ni Kati ya mikoa yenye wakaazi wanaishi na watukutu na ujuaji mwingi. Watu wenye sifa hizi huwa ni changamoto sana kuwatawala ikizingatiwa wana elements za upinzani na kuhusu kutengwa kimaendeleo.

Kwa miaka mingi iliyopita Mkoa huu ulijaa wapigaji wa pesa za serikali na kuhukumu miradi kwa wizi.Mifano iko mingi baadhi ni kama soko la Mwanjelwa na mradi wa TSCP ambapo barabara zilijengwa chini ya Kiwango ndani ya mwaka 1 tu zilianza kufumuka na kuwekwa viraka.

Lakini toka Mh. Rais amteue ndugu Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,amejitahidi kuwadhibiti watukutu na wahudumu wa miradi ya maendeleo. Ndani ya uongozi wake miradi mingi inetekelezwa na value for money inaonekana na ndio maana mh.Rais anamuelewa sana Chalamila.

Siwezi kutaja miradi yote maana ni mingi but mlioko Mbeya bila shaka mnaona saizi barabara zinajengwa kwa viwango, mahospitali nk nk hata mradi wa ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya mkuu wa Mkoa sasa liko mbioni kukamilika baada ya kusimama kwa mda mrefu na yeye mkuu wa Mkoa kuwapiga biti moja matata wakandarasi wa jengo.

Ukiona wanaomchukia hao ni wapigaji tu ambao mirija yao imebanwa, lakini yeye kama binadamu ana mapungufu ya kawaida ila kwenye kuchapa kazi namkubali na anafaa kwenye mikoa dizaini ya Mbeya, Arusha na Dar.

Niwaeleze tu watu wa Mbeya kwamba Rais anamuamini sana huyo jamaa ndio maana miradi inamiminika vinginevyo mngekuwa na Hali mbaya. Kwanza huwa hana ego na yuko honest, open and straight, nataman ahamishiwe mkoa wa Songwe Ili awanyooshe pale Tunduma mpakani kuna wapigaji wengi.

Chalamila na Bashite ni sampuli aina moja wazee wa amsha amsha. Siku akihamishwa Mbeya mtamkumbuka kutapoa kama Dar. Mnyonge nyongeni ila haki yake mpeni.

Heko Mzee wa kuwachana live makavu, bila chenga na hupepesi macho.
 
Mradi gani kafanya, kumbuka huyu anasimamia mkoa na si jiji hivyo kama unataja miradi taja ya kimkoa. Achana na ya jiji.
Hiyo hiyo miradi inayotekelezwa na watendaji wa Taasisi mbalimbali na mamlaka ya serikali ziko chini yake hao wengine ni watendaji

Chini ya uongozi wake kazi inaonekana mbona hapo zamani mlikuwa mnapiga na ushenzi mwingine kibao.Mifano iko hapo juu
 
Hiyo hiyo miradi inayotekelezwa na watendaji wa Taasisi mbalimbali na mamlaka ya serikali ziko chini yake hao wengine ni watendaji

Chini ya uongozi wake kazi inaonekana mbona hapo zamani mlikuwa mnapiga na ushenzi mwingine kibao. Mifano iko hapo juu
Miradi gani kasimamia, itaje
 
mbona sijaona chochote kilichofanyika, mbeya ya 2015 ndo mbeya ya 2021.
acha kupotosha jamii
Wewe labda kama ni mjinga sawa au kama unaishi huko mikoa mingine unaishia kusimuliwa.

Wewe kwa akili zako Mbeya ya 2015 ndio ya 2020?
 
Wewe labda kama ni mjinga sawa au kama unaishi huko mikoa mingine unaishia kusimuliwa.

Wewe kwa akili zako Mbeya ya 2015 ndio ya 2020?
kuna nini kipya!?
kwa miaka zaidi ya 10 serikali hijaleta maendeleo mbeya ikisema ni ngome ya upinzani, asa uyo chalamila kafanya nini emu tueleze boss kimoja baada ya kingine...?
 
Wewe Chalamila wacha kuja hapa kujipigia debe. Mbeya mbona ni ile ile ya miaka yote? Miundombinu hovyo kabisa kule.
Mabadiliko kidogo yanayoonekana sasa sehemu kubwa ni asante kwa Sugu kutokana na pressure aliyokuwa anaipiga alipokuwa mbunge!
 
Mpaka leo sielewi kwanini barabara kuu kuanzia uyole mpaka songwe uwanja wa ndege barabara haitanuliwi. Mbeya ndio jiji pekee Tanzania ambalo halina dual carriageway (barabara mbili mbili) imeshindwa mpaka na iringa.

Highway yote haina hata taa za barabarani, stand mpya ya Nane nane ilijengwa kwa bilioni kadhaa ila ukiiangalia ni kichekesho. Jiografia ya milima na mabonde ya jiji, ilipaswa kulifanya jiji kupendeza sana, ila ajabu ni mkoa wa ajabu sana. Ni bora uishi Tukuyu mjini na si mbeya mjini, mji umekaa ovyo sana.
 
Mpaka leo sielewi kwanini barabara kuu kuanzia uyole mpaka songwe uwanja wa ndege barabara haitanuliwi. Mbeya ndio jiji pekee Tanzania ambalo halina dual carriageway (barabara mbili mbili) imeshindwa mpaka na iringa.

Highway yote haina hata taa za barabarani, stand mpya ya Nane nane ilijengwa kwa bilioni kadhaa ila ukiiangalia ni kichekesho. Jiografia ya milima na mabonde ya jiji, ilipaswa kulifanya jiji kupendeza sana, ila ajabu ni mkoa wa ajabu sana. Ni bora uishi Tukuyu mjini na si mbeya mjini, mji umekaa ovyo sana

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Wewe jua kuwa kumemwagwa mabilioni huko Mbeya hususani kwenye huduma za jamii,ishu ya barabara ilipangwa kufanyiwa kazi awamu hii ndio maana mradi wa ukarabati wa Tanzam unafanyika kwa awamu na moja ya components zake ni hizo barabara unazozitaja.
 
Back
Top Bottom