Pamoja na elimu yao, je uzoefu kwa ma-DC na Wakurugenzi wateule ni muhimu?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Watanzania wenzangu hivi karibuni Mh.Rais amefanya teuzi mbalimbali za viongozi wetu. Tunampongeza na nimefurahishwa na teuzi hizo kwani amezingatia elimu japo hazikuwekwa wazi kwa wateule lakini hatukuelezwa uzoefu wao kutokana na madaraka makubwa waliopewa.

Naomba kuuliza, hivi elimu tu inatosha kwa viongozi hao bila ya kuwa hata na uzoefu japo wa miaka miwili katika Utumishi wa umma?

Naomba tulizungumzie japo kidogo.
 
Watanzania wenzangu hivi karibuni Mh.Rais amefanya teuzi mbalimbali za viongozi wetu.Tunampongeza.Nimefurahishwa Na teuzi hizo kwani amezingatia elimu japo azikuwekwa wazi Kwa wateule lakini hatukuelezwa uzoefu wao kutokana Na madaraka makubwa waliopewa.Naomba kuuliza hivi Elimu tu inatosha Kwa viongozi hao bila ya kuwa hats Na uzoefu japo wa miaka miwili katika Utumishi wa umma?Naomba tulizungumzie japo kidogo.
Haya masuala ya uzoefu haya ndo yanawanyima na kuwaogopesha vijana wetu wengi kazi na kuapply hzo kazi....

Nafikiri elimu inatosha kabisa kwa mtu kuwa kiongozi wa mahali husika, kwa sababu akifika pale kwenye idara kwanza kuna mafunzo atakayopata kuhusiana na kazi husika, pili kuna makabidhiano ya kiofisi.
 
Watanzania wenzangu hivi karibuni Mh.Rais amefanya teuzi mbalimbali za viongozi wetu. Tunampongeza na nimefurahishwa na teuzi hizo kwani amezingatia elimu japo hazikuwekwa wazi kwa wateule lakini hatukuelezwa uzoefu wao kutokana na madaraka makubwa waliopewa.

Naomba kuuliza, hivi elimu tu inatosha kwa viongozi hao bila ya kuwa hata na uzoefu japo wa miaka miwili katika Utumishi wa umma?

Naomba tulizungumzie japo kidogo.
Halafu kesho utakuja ukilalama kuwa hupati ajira kwa sababu kila mahali wanahitaji uzoefu wa miakas kadhaa. Wazoefu ndio waliotufgikisha hapa, we need a new breed. Jiamini kijana!
 
Hivi kile Chuo cha Uongozi hakina Hiyo Kozi yao? Maaa tuwe watu ambao tubabobea professionalism ebooo sio kubahatisha
 
Nafasi ya ukurugenzi haitaji uzoefu yey ni mratibu wa shughuli zote za Halmashauri ziwe za utawala bora, miradi ya maendleleo, ukusanyaji na utumiaji wa mapato, huduma za kijamii, huduma za kiuchumi nk na sekta zote hizi zina wataalam kwa hiyo ni kuwasimamia wafanya kazi zao kwa juhudi na maarifa yaani weledi utumike ipasavyo!! Sioni kama inahitaji uzoefu juu ya taaluma gani masna ukurugenzi hausomewi ni sawa na mbunge kwenda bungeni umwambie apate uzoefu!
 
Uzoefu wa mkurugenzi utapatikana mara tu akikaa kwenye kiti kila kitu kitamhitaji a kifanyike anahitaji kujituma kufanya kazi kwa maarifa na juhudi
 
Back
Top Bottom