Pamoja na Elimu yangu ya Darasa la Saba, acha nimfundishe Magufuli

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,879
8,800
Magufuli amekuwa akionesha kutokutosha kwake kwenye kiti cha urais na ukuu wa Nchi yetu kwa kauli na matendo mbalimbali, hivi karibuni hasa akiwa Bunda na kule Lindi alikaririwa akisema hatapeleka maendeleo sehemu ambazo hazijachagua CCM, hii maana yake ni kuwa Magufuli amekaa miaka mitano Ikulu na bado hajajua kuwa yeye ni mkuu wa nchi na kiongozi mkuu wa serikali.

Magufuli hajajua hiyo serikali anayoiongoza ni ya nani na kwanini sasa anafanya kampeni, kwa kifupi Magufuli sio tu binafsi hajielewi bali pia hajui anachokifanya. Sasa acha nijaribu kumfundisha.

1. Magufuli anatakiwa aelewe kuwa Maendeleo ya watu wa nchi husika na nchi yao yanaletwa na watu wenyewe kwa kushirikiana na serikali yao either kwa kulipa Kodi, kufanya kazi zinazotoa ajira na kuongeza uzalishaji au kufanya kazi za kujitolea.

2. Magufuli anatakiwa ajue kuwa serikali si mali ya Rais wala chama chochote Cha siasa including CCM, serikali ni mali ya watanzania, Magufuli na CCM yake wamepewa tu dhamana/ ridhaa ya kuiongoza na ndio maana sasa hivi anahangaika huko kwa wenye serikali wampe dhamana ya kuendelea kuiongoza kwa kipindi kingine Cha miaka mitano. Kitendo Cha kusema hatapeleka maendeleo kwenye eneo lolote la nchi hii kwa sababu yoyote ni kielelezo cha namna asivyotosha, ni kielelezo cha namna asivyojua why yupo Ikulu. Maendeleo hayapelekwi na CCM Wala Magufuli bali watu na serikali yao.

Ndugu zangu watanzania kumkabidhi mtu asiyejielewa Kama Magu serikali yetu na nchi yetu kwa kipindi kingine Cha miaka mitano ni usaliti mkubwa kwa mama yetu Tanzania
 
Porojo zako tu.. wakiongea wapinzani.. munashangilia.. akiongea wa Hapa kazi tu.. munaweweseka.. vizuri munamufatilia kila sekunde.. inaonyesha munapenda yake yooooote.. tano mingine mutafurahia vizuri..

Magufuli 2020💯
 
PhD dake unategemea atapata wapi Cha kuongea? Hapo ndiyo mwisho wake wa kufikiri.
 
Porojo zako tu.. wakiongea wapinzani.. munashangilia.. akiongea wa Hapa kazi tu.. munaweweseka.. vizuri munamufatilia kila sekunde.. inaonyesha munapenda yake yooooote.. tano mingine mutafurahia vizuri..

Magufuli 2020💯
Mbebaji Mkapa hayupo mjibebe wenyewe
 
Magu ni moja ya Marais wajinga Sana kuwahi kutokea Duniani


Ni kituko tuna Rais kituko Ikulu na hii nchi ina laana Sana kama Mungu karuhusu haya yatokee.

PhD holder hawezi kujuwa kwamba miaka 5 imepita amerudi kuomba ridhaa ya miaka mingine Tena yupo anatisha watu wanaotakiwa kumchagua.

Narudia Tena nchii hii ina mkosi mkubwa.
 
Mzee hajui kujenga hoja zenye ushawishi, wala kupangua hoja kutoka kwa washindani wake. Hajui kubembeleza wala kujishusha chini mbele ya wapiga kura, walau hata 2015 alikuwa akipiga "push ups" na kuwapa burudani.

Yeye sasa kimbilio na tegemeo lake kubwa ni mbeleko ya vyombo vya dola. Kwa ufupi ni kusema analazimisha mambo pamoja na kuujua udhaifu wake binafsi. Anaona njia ya vitisho na matumizi mabaya ya madaraka ni yenye tija kwake kwa kuwa ana kinga ya kutokushtakiwa endapo atatoka madarakani.

Imekuwa ni mazoea yake na imegeuka kuwa tabia yake sufu, kwa kutokusheshimu katiba, sheria, kanuni na hata taratibu zilizowekwa kisheria. Hii inaotokana na kiburi cha uzima na nguvu za madaraka aliyokabidhiwa kikatiba.

Hatambui tena kuwa yeye ni mtumishi tu mbele ya wapigakura wake. Na pia hatambui kuwa hiki ni kipindi cha kuomba kazi mbele ya waajiri wake. Anamtisha muajilri wake ni lazima ampe ajira kwa sababu ya ulevi wa madaraka.
 
Jamaa mweupe kichwani hata ukimfundishaje hataelewa

Jiwe hajui kuwa hiyo ajira yake ya URAIS ameajiriwa na wananchi sio yeye kawajiri wananchi!! Hizo pesa anazosema hawezi kuwapelekea hao wasiomchagua sio fedha zake ni za kutokana na kodi ya hao hao anaowaambia hatawapelekea maendeleo!!! Jiwe hajitambui na hiyo ndio hasara ccm inayoiletea nchi yetu. Inshallah MOLA atasikia kilo chetu!!!
 
Porojo zako tu.. wakiongea wapinzani.. munashangilia.. akiongea wa Hapa kazi tu.. munaweweseka.. vizuri munamufatilia kila sekunde.. inaonyesha munapenda yake yooooote.. tano mingine mutafurahia vizuri..

Magufuli 2020💯
Hakuna mpinzani asiyejielewa Kama magufuli,hata wenyeviti wa ccm waliomtangulia hawajawahi kufanya au kuongea upuuzi huu unaogongewa na huyu incompetent
 
Back
Top Bottom